Mangula: Lowassa bora uondoke kuliko kuivuruga CCM

Mangula: Lowassa bora uondoke kuliko kuivuruga CCM

Hizi ni sarakasi za Ccm lakini wenye Akilini
tunajua vizuri.

Aliposema Serikali yoootee nimeiweka mfuko
wenye akili tukajua tu anatoa rushwa,nikamtia
ndani.

By JK Nyerere(Pumzika)
Hapo ukiangalia utaona wazi Mwl hakuhitaji
mpaka mashahidi ni jambo la haraka sana.
 
Nadhani huu ni wakati wa CHADEMA nao kumtumia Lowassa ili kuisambaratisha CCM!!!

Kwasababu wamewasha kwetu ngojea na sie tuwashe kwao na kwanzia leo niko upande wa Lowassa japo simpendi ila ntampigia debe ili huko CCM nako moto ushike paa ..E.L for presidency 2015!
 
Hii ni mbinu tu, Lowassa hana mpinzani katika hili ndani ya CCM, kumbe wao ni kumpa sapoti tu vinginevyo watazidisha makundi na kudhoofisha Chama, NAMUUNGA MKONO LOWASSA kwa nguvu zote, tunamhitaji mtu kama huyu kurekebisha nchi hii zaidi ya mtu yeyote aliye ndani ya CCM, kama mnabisha mtajeni yoyote toka CCM ambaye anauzika kuliko Lowassa!
 
  • Thanks
Reactions: WCM
Wazee wengine sijui vip.. yaani bila aibu eti anatoka mbele za watu kukemea harambee na michango mbalimbali ya viongozi wa chama eti ni rushwa na watachukuliwa hatua... Lowassa anasaidia sana chama kujijenga na kujitangaza mana bila harambee zake sijui ccm wangekuwa wapi??? na wakina Nape Nnauye umaarufu wangeutoa wapi.. Lowassa anasaidia sana hata Mangula kuonekana channel ten ni kwa ajili yake, isingekuwa Lowassa angeongea nini sasa!!!

Lowassa anafanya kazi za viongozi wa chama ila kwa chuki watu wanapiga majungu, kama nao wanaweza wafanye nao harambee basi tuone kama watapata watu, in short ndo kichwa ndani ya ccm kwa sasa, waondoke wote ccm itabaki ila akiondoka yeye ndo mwisho wa chama..


CCM wawe na shukrani, Lowassa anawasaidia sana kina Mangula..
 
Uoga wa viongozi magamba! Hawajaona EL makamba na membe wanavyogawa pesa ovyo ovyo?
 
Lowasa ni lini, wapi na tangu amejiuzuru u PM amepnekana ktk takrima,harambee ama hadhara kwa niaba ya CCM †Serikali. Mara zote anazoonekana ktk jamii ni yeye kama Lowasa tena hata CCM colours hazionekagi....iweje tuhusishe karipio la Makamu na Lowasa. Je wengine wenye team na wale wanaotembezwa na GS wetu nao wakitangaza nia later watasalimika na karipio hilo? Kwanini tunuona Edward tu?
 
...
...
==> Haya hayaaaaaa sasaaaaa.....namwona EL huyooo kuweka pingamizi thru his lawyer....
 
Hana jipya Mangula wala chama chake.... anajitoa ufahamu bure..!:fencing:
 
huyu babu hawezi mechi za siasa ya siku hizi,bora awe mpole kabla hajarudishwa kulima nyanya huko kijijini kwake,lowasa amedhamiria anachokifanya so siyo rahisi mtu yeyote kumzuia,he knows the tricks very well
 
[h=3]CCM × LOWASSA × MANGULA × SIASA[/h][h=1][/h]Imewekwa na Admin × 09:41
Philip Mangula makamu mwenyekti wa CCM Taifa amepigilia msumari mkali kwenye ndoto ya Edward Lowassa kwa kumwambia bora aondoke kwani hata simamishwa na CCM kama mgombea wake wa Urais kwani matendo anayofanya yanampoyezea sifa ya kuwa mgombea wa CCM labda chama kingine!



[TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD] [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption"]Philip Mangugla na Edward Lowassa (L-R)[/TD]
[/TR]
[/TABLE]


Kayasema hayo leo mchana Lumumba CCM Sub HQs!


 
Mangula hajatamka haya uloyaleta mtoa taarifa. Yeye amewatahadhari wana CCM kuheshimu kanuni na kutojihusisha kampeni in the name rushwa, kuchangia na takrima. Kama kuchangia inapasa kibali cha C yenyewe. Onyo lake liko general mno
 
Lowasa kapata msaidizi makamba nae sijui anatoa wap hela
 
Last edited by a moderator:
Ni kweli hana sifa kabisa anauchu wa madaraka kupitiliza taratibu za chama anazijua lakini yeye yuko juu ya sheria, anafanya ccm ni chama chake binafsi, akiwa na shughuli binafsi utashangaa amevaa kijani amewanunua watu wamevaa kijani aonekane anapendwa na wananchi,anawapa[sho , anatumia nguvu nyingi sana lowasa haijulikani kwanini kama anasifa siatulie tu wasiwasi wake ni nini? Toka nizaliwe sijawahi kuona rais aliyewahi kutumia nguvu kama za lowasa kutafuta urais, chama anakivururuga, anakigawa sijui 2015 itakuwaje kwakweli hongera mangula bora umesema
 
Ni kweli angeondoka tu, anatugawa kwa kila njia kwa pesa yake ni hatari sana aanzishe chama chake
 
Mkuu naona hapa kumekucha, nimemsikia Mangula Ch 10 lakini makundi yamelelewa tangu 2005 hadi leo yameshakita mzizi ndo maana hatawananchi tunaimani naye lakini ile miezi sita iliyotoa kwa watu kuondoka amabao ni wachafu imeshavuka sijui itatokea lini.

ni hivi zile siasa za 2005 zimeifikisha nchi ilipo,kuna watu lazima wahangaikie wateule wao,maana watapata u-DC
 
Tafadhali mods msiunganishe huu uzi na mwingine,
Leo hii katika kipindi cha bbc swahili walikua wanamuhoji mangula na akasikika akisema kua kuanzisha makundi ndani ya chama ni uasi na usaliti wa kanuni za chama cha mapinduzi, hivyo watu hao wanao anzisha makundi na kutangaza nia ya urais ni wasaliti na waasi.
Nikajiuliza ccm hao hao walikua wanakazana kusema zitto ameonewa baada ya kuitwa msaliti leo mangula kiongozi wa juu wa ccm ana waita wasaliti akina lowasa je! Ni nyani aoni kundule au nikuiga mfumo wa chadema wa kukemea uasi ndani ya chama.
 
Back
Top Bottom