Mange achoma moto kadi ya CCM live

Mange achoma moto kadi ya CCM live

Kuna watu walikuwa na siri za CCM kama KINGUNGE na LOWASA? Kawaulize kilichowapata CCM na siri zao walizokuwa wakijua.Mange is a non entity.Na kwa taarifa yenu msiojua wafuasi wengi mnaosema anao kwenye mitandao asilimia kubwa walikuwa CCM wenzie kaondoka angalieni atakavyodorora kama akina kingunge na lowasa

Hayo unayoonga angalia mange si kama hao hana cha kupoteza ohooooooo
 
Mange ananguvu sana kwa upande Wa kina Dada Na kina mama Wa nyumbani kuna watu hawalali bila kumsoma mange hii kampeni amefanikiwa ccm naamini watabaki Na watu wachache sana mwisho Wa siku watapoteza majimbo mengi sana
Kwahiyo hutaki ccm wapoteze majimbo mengi sana? Umekuwa mshauri wa ccm? Kwanini usikae kimya ili ccm ikose majimbo iwe furaha kwako? Inawezekana kweli mtu kumuombea adui yake mafanikio badala ya njaa?
 
Huku kwetu Sangatuting'wa hata hatumjui Mange, in short huku watu hajui lolote kuhusu Ccm na kusababisha matatizo yao mama uhaba wa maji, kilimo duni, umeme hakuna, barabara mbovu n. k

Wanachojua ni kupigia kura Ccm tu wakati wa Uchaguzi
Ni sahihi kabisa ccm haijawahi kusababisha au kuleta matatizo umaskini n.k bali inapambana na matatizo hayo hao akina mama wako sahihi kabisa.
 
wanaomsikiliza yule kahaba anayeishi kwa kujiuza ni watu wakuwapuuzia tu hatuwahitaji ccm.
 
Hahahahahaaaaaa. Unanikumbusha ule mjadala wa ANAKATWA HAKATWI. Mwisho wa siku akakatwa na bado tukashinda Urais wabunge na madiwani


Kunywa maji Makondakta , maana vichambo anavyokupaga mange si vya kitoto
 
Wanajuta kutokumpa ubunge ili apambane na ukawa.
Sasa atawabomoa.
Sasa wakuu muwe mnasema sababu za hizi chuki mapema. Kumbe tunahangaika kuchangia mada kumbe kisa alikatwa? Ng'ombe kasoro mkia kumbe!
 
... Mange anawafuasi wengi na asilimia kubwa humuelewa.. Dada yangu alikuwa CCM pure ila Leo tu kabadilika

... PolePole ni mtu wa mitandao ya kijamii hivyo ataumia kuona anachofanya Mange ukizingatia yeye ni mtu wa Itikadi na Uenezi hivyo akiendelea kumjibu atazidi kukichafua Chama..Mange akiibua clip za Polepole kipindi cha katiba ni hatari sana kwake na Chama

... Kuna watu wanaosoma na kumuelewa kimya kimya na kulisha sumu wengine...huwa mitandao inasambaza habari exponentially ndio maana info za social network zinakuwa viral...

... Sasahivi kila mwenye shida na aliyeonewa hutuma lalamiko kwake.. Yaani Amekuwa kama sanduku la maoni hii huleta picha mbaya serikalini hata kama ni uongo...

... Alikuwa ndani ya CCM na anajua madudu yao na ana marafiki wengi wapo humo.. Wakimpa info za ndani na kuziweka public Chama kitaangamia

.. Anawavutia sana millenials ambao huwa kawaida hawapendi siasa na sasa wanapata updates kila siku... Hii ni hatari Kwa Chama cha Mapinduzi..


Mange Spring is Real... CCM tuchukue tahadhari mapema!


Ethos
Ndani ya Masaa 48 tangu hiyo Mange Spring ianze amepost video Sita tu na narudia video sita tuu. Achana na hizo video ambazo watu wameahidi kuchoma. Ili afanikiwe atleast robo ya kadi zichomwe na kwa kasi yake hiyo itamchukua takribani miaka 30. So nenda kamshauri aendelee kupoteza muda maybe ndio dawa ya KUPONA KICHAA CHAKE.

Kitu Kingine Chadema Propaganda Think tanks hizi mbinu nyingine mlitakiwa mzianzishe kupitia hao mawakala wenu kina Mange kipindi cha karibu na uchaguzi na si sasahivi.
 
Mange Kimambi amechukua hadi ya uanachama tarehe 3 Machi 2015. Pia Mange Kimambi anaishi Marekani kwa zaidi ya miaka 8 sasa. Sasa hapo utasemaje kuwa anajua siri nyingi za CCM? Alichukua kadi ya CCM kwa tamaa ya madaraka. Sasa katoswa anaanza kutukana viongozi wa CCM. Ni mpuuzi tu anaweza kumshabikia Mange Kimambi


Mkuu Ile ni kadi ya pili... Kumbe hata hujui na una orodha hapo Lumumba?
 
Mi nashangaa kwanini hadi sahivi hajakamatwa, mbona yule mmiliki wa Ze Utamu blog alipomkashifu Kikwete alishughulikiwa fasta hukohuko UK?
 
Mange ananguvu sana kwa upande Wa kina Dada Na kina mama Wa nyumbani kuna watu hawalali bila kumsoma mange hii kampeni amefanikiwa ccm naamini watabaki Na watu wachache sana mwisho Wa siku watapoteza majimbo mengi sana
Mm ni mwanaume na tokea mange aanze siasa nimekuwa namfollow na kumsoma kila nikishika smartphone yangu. Huyu vuguvugu lake limeshika watu wengi na uzuri zaidi wanapozidi kafikia mahali huwezi kumpuuza na wala kumjibu maana vyote vinazidi kumpaisha na hilo kwli kafanikiwa labda wamuue au wamfunge
 
Bora ww msema kweli.....kijana wa mtaa wa LUMUMBA
 
Mbona wakati ule huyo Mange alipokuwa akipost kumkashifu mgombea wa Ukawa, Edward Lowassa wakati wa kampeni mwaka jana nyinyi wenyewe watu wa CCM mlimshangilia sana na kumuita shujaa wenu?

Tulieni wanaccm dawa iwaingie vizuri.....

Hivi nyinyi maccm tayari mshasahau kuwa hata nyinyi kwenye mikutano yenu ya kampeni mwaka jana, mara kadhaa kwenye mikutano yenu mlikuwa mkizichoma moto kadi za Ukawa zilizokuwa zikirejeshwa kwenye mikutano hiyo?

Kumbe mkuki kwa nguruwe, kwa binadamu mchungu sanaaa!
Patamu hapo
 
Back
Top Bottom