Mange achoma moto kadi ya CCM live

Mange achoma moto kadi ya CCM live

Yaani baada tu ya Mange jana kuchoma kadi yake, kuna maelfu wamerejesha imani kwa chama hicho. Kwa sabahu Mange alikuwa anadhalilisha sana chama chetu hasa kutokana na tabia yake ya kuishi kwa kujiuza huku wakati mwingine amevalia nguo za CCM
Unapenda-ga sana kujitekenya wewee...

Hivi unajua nguvu alizonazo Mange..??

Ana more than 740,000 followers kwenye IG page yake..
Meaning that, page yake unaweza kuta inapitiwa hata na 2M viewers halafu unaona hana impact yoyote kwenye jamii!!??

Ukweli ni hivi.. Watakaotoka CCM ni wengi kupitia kampeni ya Mange kuliko watakaoingia CCM.

Unasema wengi wameanza kurudi CCM, weka facts kwa evidence sio bla bla.
 
Tatizo linakuja pale ambapo kura ya Mwenye akili sana na mnywa viroba zina hadhi sawa.
mywa viroba lini akakumbuka kupiga kura. aache pombe akapange msitari... mtasubiri sana ukiwa na wafuasi type hii subiri maumivu au umesahau safari ya matumaini iliyoongozwa na pikipiki plus viroba mikutanoni.
 
Wakati wa uchaguzi uliopita alikuwa upande wa chama alichochoma Kadi na kilishinda.
Sasa kaondoka sijui nini kitatokea uchaguzi ujao.
 
Ni wazi ataondoka na wavamizi wenzake waliokuwa wanakipaka matope chama.CCM inarudi ktk misingi yake ya ustaarabu na heshima.Ni imani yangu Polepole na sekretari yote hamtatuangusha ktk kukisafisha chama na kukirejeshea heshima yake iliyopotezwa na watu jamii ya kina Mange!
R.I.P. Yohane Mbatizaji a.k.a johnthebaptist
 
Mbona wakati ule huyo Mange alipokuwa akipost kumkashifu mgombea wa Ukawa, Edward Lowassa wakati wa kampeni mwaka jana nyinyi wenyewe watu wa CCM mlimshangilia sana na kumuita shujaa wenu?

Tulieni wanaccm dawa iwaingie vizuri.....

Hivi nyinyi maccm tayari mshasahau kuwa hata nyinyi kwenye mikutano yenu ya kampeni mwaka jana, mara kadhaa kwenye mikutano yenu mlikuwa mkizichoma moto kadi za Ukawa zilizokuwa zikirejeshwa kwenye mikutano hiyo?

Kumbe mkuki kwa nguruwe, kwa binadamu mchungu sanaaa!
a word. Wachome tu watajua wenyewe
 
Wakati wa uchaguzi uliopita alikuwa upande wa chama alichochoma Kadi na kilishinda.
Sasa kaondoka sijui nini kitatokea uchaguzi ujao.
kwani kuwa na kadi ya chama fulani ndo kukipigia kura wewe mtu wawapi? mbona lowasa hajarudisha kadi ya CCM.
 
Hata elimu huna ndio maana una andika upupu unajua maana ya KUSENGENYA KWELI? mange haisengenyi serikali bali anaiambia live maovu yake ukitaka awe blocked ndio ataisengenya maana ataongea kwa watu nawe hutasikia direct kutoka kwake, acha dawa iingie huyu alikuwa shujaa wenu 2015 yaani mwaka mmoja tu mnataka kumtoa ulimwengu wa mitandao wakati mlikuwa mnampa hata bundle 2015 ili asikosekane?1 Poleni hamkujua dunia duara ee? Kunywa maji mkuu.
 
ni sawasawa na sisimizi mmoja kufa kwenye msafara, ahaaaa haizuii wengine kuendelea, bure kabisa
 
Aisee mbona umetoa neno la leo. eti mange
kimambi anatishia nyau kutoka ccm. yaani watu kama mange wakitoka wote ccm chama kitatakata.
 
Yaani baada tu ya Mange jana kuchoma kadi yake, kuna maelfu wamerejesha imani kwa chama hicho. Kwa sabahu Mange alikuwa anadhalilisha sana chama chetu hasa kutokana na tabia yake ya kuishi kwa kujiuza huku wakati mwingine amevalia nguo za CCM
Mbona haukulisema hili mapema mkuu Lizaboni unalisema hili baada ya kuchoma kadi.
 
Wakati wa uchaguzi uliopita alikuwa upande wa chama alichochoma Kadi na kilishinda.
Sasa kaondoka sijui nini kitatokea uchaguzi ujao.
ila nikusihi tuliza mkali na omba Mungu uchaguzi ujao uwepo ili ukodoe macho vizuri tena.
 
Le madame mange kimambi, nahsi atasepa na kijiji kama sio kijiji ni mkoa kabisa kwa hii kampeni yake imekuja mda hasaa, tusubiri
 
kwani kuwa na kadi ya chama fulani ndo kukipigia kura wewe mtu wawapi? mbona lowasa hajarudisha kadi ya CCM.

Swala sio kupiga kura bali Kupiga Kampeni.Kupiga Kampeni kuna athari kubwa sana maana unaweza kuvutia wapigakura kwa Maelfu,Malaki hata Mamilioni.Kadi ni mali ya mmiliki yaani aliyeinunua na ana uwezo wa kuifanya anavyotaka kama kuichoma,kuitupa,kuitunza kama kumbukumbu,kuirudisha,kuichana nk.
Huyu dada alifanya kampeni kubwa sana kukisaidia Chama kwa kumponda Lowasa waaziwazi na kupata wafuasi wengi.
Wasiwasi wangu ni kwamba anaweza kufanya kampeni ya kukiponda chama chake cha awali alichoamua kuchoma mpaka Kadi anayoimiliki.
 
Wakiondoka wanachama kura zitaongezeka maana chama kinategemea watu wachache wenye akili za kisisiem na si wengi wenye umri wa kupiga kura.
 
Back
Top Bottom