Mange achoma moto kadi ya CCM live

Mange achoma moto kadi ya CCM live

h
Kutokana na kuchoshwa na ahad hewa na kuzuia demokrasia na mtukufu kula pesa za tetemeko kagera na kumfungia maxence melo hii ni kampen imekuwa nzur zaid kuonesha kuchukizwa na matendo hayo kwa KUANZA na kuchoma kad za uanachama wa ccm

Ameandika hiv mange


@Regrann from @mangekimambi_ - It's official, sina chama......
.
.
[HASHTAG]#Opereshenichomakadiyaccm[/HASHTAG]
.
.
Kama na wewe unapinga udikteta wa Magufuli, kama unataka [HASHTAG]#Bungelive[/HASHTAG], kama unapinga kuminywa kwa uhuru wa vyombo vya habari, kama unapinga watanzania kunyimwa uhuru wa kujieleza, kama unapinga wabunge wa CCM kupitisha sheria zinazokiuka haki za binadamu, kama umechoka kuona wabunge wa CCM wakisaidia chama na sio mwananchi, kama unapinga MaxMelo wa jamiiforums kukamatwa, kama unapinga Lema kuwa ndani mpaka leo sababu ya maono/ndoto, kama unapinga wabunge wa upinzani kufukuzwa bungeni , kama umechoka na ahadi za CCM , kama umechoka umaskini, kama ni mwanafunzi umerudi nyumbani kwa kukosa mkopo, kama wewe ni mwalimu wa sanaa, kama unasubiria ajira ya serikalini toka mwaka jana, kama biashara yako imekufa sababu ya makodi, kama ulisikitika mwenyekiti wa CCM kupiga panga pesa za mchango wa Kagera, kama umechoka umaskini, kama unataka kuona system MPYA Tanzania in 2020. Kwa kifupi kama umechoka na ungese wa CCM basi ntumie video yako ukichoma kadi yako ya CCM.... Maana wanadhani wanaowakosoa ni wapinzani kumbe wanakosolewa na watanzania wasiojali vyama bali nchi yao..
.
.
Tukitaka kuandama wanatishia kututoa uhai. Kuna njia zingine za kuwaonyesha hatuko nao. Njia moja ndo hii [HASHTAG]#OpereshenichomakadiyaCCM[/HASHTAG]
.
.
Ntumie video yako kwa whatsapp +1 310 855 4352
.
.
.
.

PS: ni kadi ya 2015 coz nilipoteza ya zamani.... - [HASHTAG]#regrann[/HASHTAG]
Mwanamkee age yakenadhani anaitajii mumewakumpenda

Shidawanamtamani wanamkimbia
 
Huyu dada leo anasema anachoma kadi;juzi kasema tumchague Magufuli....kesho ataamka anatukana matusi ya nguoni!Mwanaharakati[emoji53]

Sio yeye tu aliyesema na kumpigia kampeni Magufuli, walikuwa wengi sana na wengi wao leo wanajuta, hivi uliona ile Harusi ambayo waalikwa walikataa kabisa wasifanyiwe comedy ya sauti ya Magufuli?

Katika hali ya kisiasa hilo ni la kawaida sana
 
Watu wanatukuza kipande cha karatasi kuliko uhuru na demokrasia.

Wanapenda " Kipande" kuliko uchumi

Wanapenda kipande kuliko ajira za walimu wa sanaa
 
Ukitaka kupendwa na watu kuwa mnafiki. Ndio anachokifanya huyo mmama.
 
Ndicho chama tawala.Km hupendi ama hama nchi au kufa!Vinginevyo pilipili isiyo yako yakuwashia nini?!
Lazima uwe taahira kufikiria kuwa kuna mtanzania ambaye anatakiwa kuhama au kuhamishwa nchi kwa sababu yoyote ile. Hakuna mtanzania mwenye haki zaidi ya utanzania kuliko mwingine. Ni lazima uwe punguani kuamini kuwa kuna watanzania wenye haki ya kuhamisha watanzania wengine.

Tutapishana na kutofautiana kiitikadi, kimtazamo na kifikra, lakini mwisho wa yote, sote ni watanzania wenye haki ya utaifa wetu inayolingana.
 
Ni jambo Jema maisha, mtu kuwa huru na kutumia akili zake kufikiri
 
huyo ni chizi tuu na hana athari.mambo yote ni kwenye boksi la mpiga kura....naomba tukutane 2020 alafu muone
wabongo wasahaulifu sana 2020 CCM inashinda tena na mtakuja na mtajipa moyo tena 2025 tushawazoea,kuwa mmshindi ni mikakati sio porojo na majungu mitandaoni.
 
Mimi sina ila kama nigekuwa mwanachama ningechoma mpaka majivu yake
 
Mange ana stress ya kuachwa na mabwana ukiungana naye hapana shaka na wewe una stress hizo hizo. Poleni kwa kuachika
Acha maisha yake binafsi jadili hoja kama haina mantiki kwako pita kushoto. Hakuna binadamu aliyekamilika nawe ukiwa miongoni mwao!
 
Who is mange kimange?? Anaishi tz hapa?? Anatibiwa hospital za tz hapa?? Alipiga kura?? Alikuwa na mchango gani ndani ya chama?? Mara ya mwisho alilipia lini kadi yake??ana mchango gani kwa taiga?? Ameshawahi kuwa hata Kiongozi wa mtaa??
Ambao hawajawahi kuwa viongozi wa mitaa au mashina wako wengi angalia kijana
 
Kuna vitu huwa najiuliza sana ,what if Mange ni double agent ? Kwa maana ya kwamba anaonyesha anapigania udhalimu wa serikali kumbe pia serikali inamtumia kupata vitu fulani ?
Hawa wanaotuma videos au pictures kupitia whatsapp wana uhakika gani taarifa zao zinaishia kwa Mange ?
 
Chama kilichooza,kisichokua na nyuma wala mbele. Mmekula hela za maafa,mnangaika na Faru badala ya kuangaika na matatizo ya wananchi?
Ww wasema lkn ndicho chama tawala kwa wakati huu ndiyo maana nimekupa chaguo la km ama hama nchi au ufe km huwezi kuvumilia hadi huo wakatiyo utapo wadia.
 
Back
Top Bottom