Mangariba wawili maarufu kwa ukeketaji vichanga huko Moshi Kilimanjaro watangaza kustaafu

The Evil Genius

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
5,464
17,290
Mangariba wawili mashuhuri mkoani Kilimanjaro, wanaosifika kwa kukeketa vichanga na wasichana, wamesalimu amri na kutangaza kuachana na kazi hiyo, baada ya kubanwa na Kamati ya Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) katika Kijiji cha Mawala, Wilaya ya Moshi.

Nimekua nikisikia kwamba mkoa wa Mara, Manyara na Dodoma ndio wakawake wao wamekeketwa, kumbe hata Kilimanjaro ukeketaji umetamalaki kiasi hicho?

=====

Mangariba wawili mashuhuri mkoani Kilimanjaro, wanaosifika kwa kukeketa vichanga na wasichana, wamesalimu amri na kutangaza kuachana na kazi hiyo, baada ya kubanwa na Kamati ya Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) katika Kijiji cha Mawala, Wilaya ya Moshi.

Waliokubali kwa maandishi, kuacha kukeketa watoto wachanga na wasichana wa jamii ya kifugaji ya Kimasai katika ukanda wa tambarare wa Kahe, ni Ruth Merinyi na Anjelina Jackson.

Akizungumza jana katika kikao kazi cha kutoa mrejesho wa shughuli walizozifanya wajumbe wa MTAKUWWA katika kipindi kisichozidi mwezi mmoja, Katibu wa Dawati la Kupinga Ukatili, Kata ya Kahe Magharibi, Jonas Mlay, alisema mangariba hao wamekiri kwa barua (Nipashe imeiona nakala yake), kuendesha ukeketeaji kwa njia ya usiri, licha ya vitendo hivyo kuwa haramu kwa Watanzania.

Kwa mujibu wa barua hiyo, mangariba hao walitangaza kuachana rasmi na kazi hiyo Septemba 25, mwaka huu.

Kamati hiyo imepata mafanikio chanya, baada ya kupatiwa mafunzo maalum na Shirika lisilo la kiserikali la TUSONGE CDO, linalotekeleza Mradi wa Kupinga Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto, chini ya ufadhili wa The Foundation For Civil Society.

Nipashe
 
Back
Top Bottom