Nikisikia kahamishwa kituo cha kazi, au kushushwa cheo, nitajua Serikali haina mpango wa kutokomeza ukatili kwa Watoto

OLS

JF-Expert Member
Oct 12, 2019
419
670
Maneno ya utangulizi katika Mpango Kazi Wa Taifa Wa Kutokomeza Ukatili Dhidi Ya Wanawake Na Watoto (MTAKUWWA), una maneno ya kuazimia kufanya Watoto wote wakue bila kukumbana na ukatili wa aina yoyote. Na kimsingi wameweka kuwa ukatili unaingarimu Tanzania takriban dola za kimarekani bilioni 7.1 sawa na 7% ya GDP.

Kimsingi MTAKUWWA imeweka wazi suala la sheria inayorasismisha adhabu kwa Watoto kitu ambcho kinafanya ukatili uweze kutokea dhidi yao. Kuna haja kubwa ya kufanya marekebisho katika kipengele hiko kwa kuwa mwalimu Mkuu waliyempiga mtoto kule Kagera anaweza kuonekana amefanya jambo jema kwa jina la kumfunza nidhamu mtoto.

Tumeshazika Watoto kwa ukatili, tumeshawatibu Watoto wengi kwa ukatili. Na kwa kuwa Watoto wanatakiwa kukua bila ku-experience namna yoyote ya ukatili ni vyema tukaonesha kwa vitendo kwa kuwafukuza kazi watu hawa ambao hawaoni haja ya kustaarabika katika karne hii ya sayansi na teknolojia.

MTAKUWWA imeweka sentensi kwamba Tanzania kama nchi nyingine iliyoingia makubaliano mbalimbali ya kimataifa, inaheshimu haki za binaadam, sentensi hii itakuwa unafiki ikiwa hatuna hatua kali zinazochukuliwa dhidi ya hawa wachache wanaofanya ukatili kwa Watoto.

Wala sitasema mwalimu yule aende jel, ila akienda haina shida, lakini pia kazi ya ualimu haimfai akafanye kazi nyingine. Shule sio jeshi. MTAKUWWA umeshaona kuwa Watoto wanaopata physical abuse huwa wanakuwa na Trauma zinazowaendesha Maisha yao yote, aidha Jamii imeshaonekana kuwa na kiasi kikubwa cha Anti-Social behavior badala ya pro social ambayo yameonekana kuwa ni madhara ya ukatili dhidi ya Watoto.

Shule zinazopiga Watoto, bado Watoto hufeli kwa kiasi kikubwa huku shule za international ambazo hazina muda na adhabu za kikatili Watoto wakifanya vizuri. Suala la kuzuia ukatili sio tu italeta faida kwa Watoto bali kwa elimu nzima.

Nasema atimuliwe kazini.
Vifo vya Watoto vimetosha.
Majeraha kwa Watoto yametosha.
Ni wakati wa kutambua haki za Watoto kwa vitendo.
Yule mwalimu atimuliwe kazi
 
Siajabu mzazi huyu aliyeandika hapa ni wa kiume; nasema kwa hali hii watoto wataendelea kulawitiwa na kulawitiana na hatimaye kuwa mashoga mpaka basi. Kama angelikuwa mwanangu, akirudi nyumbani angekula mbata kadhaa za kwanini amepigwa!
 
Back
Top Bottom