Moshi: Watoto wawili wa familia moja wateketea kwa moto

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Jan 29, 2021
573
2,553
Watoto wawili ambao ni wa kike na kiume, wenye umri wa miaka miwili na nusu na mwingine miaka miwili na miezi minne katika Kijiji cha Shinga, Wilaya ya Moshi, mkoani Kilimanjaro wameteketea kwa moto baada ya nyumba waliyokuwa wamelala kuungua.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo leo, Februari 28, 2023 Kamanda wa Polisi Mkoani hapa, Simon Maigwa amesema tukio hilo limetokea leo watoto hao wakiwa wamelala wakati baba yao alipoenda dukani kununua sigara.

"Baba wa hawa watoto aliondoka muda mfupi kwenda kununua sigara dukani wakati anarudi akakutana na moshi mkubwa ukitoka ndani ya nyumba hiyo, ambapo watoto wote wawili walioteketea kwa moto," amesema Kamanda Maigwa.

Mwananchi
 
Hii ya kuwaacha watoto kwenye nyumba peke yao huku viberiti viko juu juu ni hatari sana. Majuzi kati imetokea maeneo ninayotembelea (siweki picha), dogo aliachwa ndani peke yake, akaona kiberiti akawasha, alipoona moto unamuunguza akatupa ile njiti ikadondokea kwenye uvungu wa kitanda ikakutana na mavitu yanayoshika moto, ikawa balaa. Bahati nzuri raia wakawahi kumtoa lakini mle ndani..hasara tupu!
 
Siku ikifika hauwezi kuzuia hata uwe makini vipi...maisha ya duniani ni magumu Sana tena yamejaa taabu
 
Kwa hii ni mara ya ngapi? Maana hata Rombo mwaka huu nyumba iliungua.
Screenshot_20230228-204931.png
 
Back
Top Bottom