Maneno ya kejeli ya mume wangu

Maneno ya kejeli ya mume wangu

Pole Dada kwa mitihani ilokupata. Ushauri wangu muombe Mungu Kwani yeye peke yake Ndo anaweza kumbadilisha mume wako. Kila ndoa ina mapito yake.
Na pia hilo tatizo lako linatibika kabisa. Kuna daktari nafahamu anaweza kukusaidia na ukapona kabisa
 
Ushauri mzuri sana huu.

Binti,

Unapoteza muda hapo, huyo bwana hatakufaa kwa shida wala kwa raha...

Ukizingatia kwamba bado hujapata mtoto, ni fursa safi ya ku-move on na nina imani kwamba you will get kids ukitulia na kufocus kwenye matibabu, kazi na mapenzi mapya

You'd rather be alone that a person who ruins your life

Hapo sijazungumzia hatari za magonjwa na mikosi mingine
 
Leave! Even for a while. Leave so you can find peace of mind, once you have peace of mind you can decide the direction you want to take.
Sasa unaishi under a lot of confusion and stress, it's important you have time alone my dear.
Pole yake huyo dada kwa mateso aliyonayo ndani ya ndoa yake, ujue ndoa ni upendo wa dhati kama hakuna upendo wa dhati basi hakuna ndoa, fanya uamuzi wa busara kuachana na huyo mwanaume hana upendo na wewe, anaweza kukuletea magonjwa ya zinaa. usilazimishe ndoa isiyokuwa kuwa na upendo.
 
Nacherewa hebu tupe mrejesho wa ndoa yako kwa sasa, miezi km minne sasa tangu ulete hii thread, naamini kuna mengi yatakuwa yametokea hapo kstikati...either u moved away au mmeo amejirekebisha tabia!
 
Last edited by a moderator:
Pole sana mpendwa wangu,huyo mumeo jeuri,ana dharau na kahaba wa kiume!sifa zote mbaya za mwanaume zinazoumiza wanawake anazo.kwa haraka haraka nimekusoma ni kama huyu jamaa kashakujua wewe kwake HUPINDUI,ndo mana hajali fikra,wala maumivu yako.sasa mtu kama huy ambaye ni mshenzi mbobevu,dawa yake ni ushenzi tuuu!usinielewe vibaya,kwanza NI MWIKO WEWE KUANZISHA UHUSIANO NJE YA NDOA YAKO,ila

fanya yafuatayo;

1.asubuhi mkiwa mnajiandaa kwenda kazini,wewe amka mapema sana jifanye una maandalizi flani ya mtoko maalum,halafu saa ya kuvaa hakikisha anakuona unavaa vipyaaa kuanzia ndani hadi nje,jirembe weee,halafu jifanye uko bize mno na simu as if unaogopa yeye kuishika au kusoma kitu flani ktk simu yako.ukiwa kazini mchana mchana m call mwambie mume wangu leo nitachelewa kidogo kurudi nyumbani,tuna kikao flani nataka kujiunga kikundi cha wanawake.sasa hapa usimpe muda sana kukuuliza wala usijieleze sana,jifanye kama una haraka flani hivi.wewe ukitoka kazini pitia hata kwa ndugu zako,vutavuta muda,kagiza kakiingia rudi home,tena ikiwezekana jifanye umejichokea mwaego!ukirudi simu na wewe,wewe na simu!fanya hivi mara kadhaa,sasa kama ni kwenda kwenye maombezi,huu pia huwa ndo muda muafaka kwenda ili uchelewe kurudi kidogo.

2.akichelewa kurudi usimuulize,usimkohoe,mwandalie kama kawaida chakula nknk,na asikuone unakosa usingizi kitandani,hata kama unaumia jifanye humjali,humfikirii,unalala fofoffoo!

3.simu yake iwe kituo cha polisi,yyaani usipende kuishika,na akipiga simu usitege sikio,nyanyuka kabisaa,jifanye hutaki kusikia anachosema.

4.acha.acha kabisa kujibuhovyo sms wala kuongea hovyo na mahawara zake,wakikukashifu,wajibu "asante sana,nitashukuru kama akihamia kabisa kwako,maana mie nishamchoka na wala simtaki"maana ujue ukiwajibu hovyo,wakikutana wenzako wanakunanga,we hujui tu.sasa ukijibu hivyo,akifika kwa bibie,akipewa maneno yako,itamuuma mumeo.

5.fanya hivi mara kadhaa,nakuambia ataanza mwenyewe kurudi mapema,na kuanza kuogopa kulala nje,maana mwanaume malaya hataki wala hapendi kusikia mkewe ana mchepuko,kwa kufanya hivi ataamini nawe umeopoa huko nje.na huu ndo utakuwa mwanzo wa yeye kujitambua ni nani kwako,na umuhimu wako ataujua.

Nimependa comment yako mkuu...
 
Hukupaswa kufanya hili kwa mwanaume yabisi, mkiriti,mjihibu na mlimuti

''Bahati nzuri nilikuwa na ndugu zangu ambao ni polisi tena wana vyeo hapo kituoni, nikaweza kufuatilia hadi kesi ikaishia polisi''
 
Habari za asubuhi wapendwa,

Mimi ni member wa JamiiForums kwa muda mrefu ila nimesajili ID mpya kwa sababu maalum na hayo niliyooyandika ni ya kweli na ndio hali halisi

''Unaroho mbaya ndio maana huzai'' ''Najuta kwanini nilikuoa wapenzi wangu wa zamani ni bora kuliko wewe'' nilikuoa kwa kukuonea huruma''. Haya ndio baadhi ya maneno ya kejeli ambayo nilishawahi kuambiwa na mume wangu.

Mimi ni mwanamke mwenye umri wa miaka 36, nimeajiriwa na mume wangu ana shughuli zake binafsi. Nina miaka minne ndani ya ndoa ila sijabahatika kupata mtoto kwa sababu nimegundulika nina (Polycystic Ovarian Disease (PCOD) na mume wangu kuwa ana low sparm count.

Mume wangu amekuwa ni mtu wa kurudi usiku mara nyingi kuanzia saa sita, siku nyingine analala huko bila hata kuniambia na hata ukimpigia simu hapokei. Asubuhi anakuja anakuambia tulikuwa tuna biashara tunafanya na simu niliacha kwenye gari. Tukawa tunagombana kwa ajili hiyo hadi tukalifikisha kwa wazazi, akagombezwa akaacha kwa muda lakini karudia tena.

Siku moja alilala tena nje bila taarifa, nikampigia simu hakupokea, ilipofika alfajiri nikapigiwa na mwanamke simu akaniambia acha kusumbua waume za watu, niko naye hapa. Kama ni mumeo mbona hayuko kwako? Kidogo nizimie ila nikapiga moyo konde. Alivyorudi nikamuuliza akasema tulikuwa naye kwenye biashara kwa hiyo alikuwa na simu zetu.

Khaaa nikamwambia mdanganye mtoto ila sio mimi. Baada ya mwezi mmoja akanunua mzigo kumbe ulikuwa wa wizi akakamatwa na polisi, akaniambia mke wangu nimekamatwa kesho njoo polisi Kijitonyama, hapo ilikuwa usiku. Kesho asubuhi naenda polisi kumpelekea breakfast nikaambiwa mbona mkewe kaja kuleta chai! Nikawaambia polisi mbona mimi ndio mkewe halali? Nilikasirika kwa kweli nikaondoka na chai yangu. Bahati nzuri nilikuwa na ndugu zangu ambao ni polisi tena wana vyeo hapo kituoni, nikaweza kufuatilia hadi kesi ikaishia polisi.

Siku hiyo ya kutoka ilikuwa mida ya saa kumi na moja, muda huo nilikuwa natoka kazini, nikawapigia maafande wakasema mume wako ameshatoka. Nikajaribu kumpigia simu yake haipatikani, kesho yake anarudi nyumbani ananiambia polisi waliturudisha ndani. Nikamwambia acha uongo mie ndugu zangu walinihakikishia kama umetoka, akabisha katakata, ila mtu mwenye akili unajua ukweli.

Baada ya mwezi hivi nikamwambia twende kwenye send off ya mtoto wa jirani yetu akadai amechoka, akaniambia huwa unapenda kushadadia vya watu wengine mbona mjomba wangu mke wake kajifungua hujaenda kumsalimia? ''Una roho mbaya na hutaweza kupata mtoto'' mimi huyoo nikaondoka zangu na majirani wengine. Kumbe siku hiyo walitibuana na huyo hawara wake.

Nimerudi kalala fofofo, simu yake inaita tu. Kwasababu yule mwanamke alishanipigia na kunitolea mbovu namba yake niliishika. Sikupokea simu kwa sababu sinaga tabia ya kupokea simu ya mume wangu.

Wazo likanijia nikaangalia message, nikakuta huyo dada anamwabia kumbe una mke hukuniambia mimi na wewe basi. Kesho yake nikampigia huyo mwanamke akaniambia story yote na ile siku aliyotoka polisi kumbe alilala kwake. Akanimbia mimi nilidanganywa na mumeo kwamba hana mke, na nilishawahi kuja hapo nyumbani pindi ukiwa umesafiri. Na kwa vile nimeujua ukweli simuhitaji tena huyo mwanaume, na roho inaniuma kutembea na mume wa mtu kitu ambacho kinaniumiza ila sikujua naomba unisamehe.

Pamoja na hayo yote anakataa katakata kuwa hana uhusiano na yule dada. Eti ''huyu dada ni girlfriend wa rafiki yangu wamegombana ndio ananiforwadia hizi messege.''

Na hii sio mara ya kwanza alishawahi kuwa na mwanamke mwingine akamdanganya kuwa hajaoa hadi huyo mwanamke akaja nyumbani kuhakikisha ndio akaujua ukweli. Pindi anapokuwa na michepuko kejeli haziishi mara najuta kwanini nilikuoa, nimekuoa kwa kukuonea huruma etc. Hizi kejeli huwa nikizikumbuka nakosa raha kabisa. Na tendo la ndoa tunaweza kufanya mara mbili kwa wiki kila akija amechoka.

Niko njia panda naona nimemchukia mume wangu ghafla, majukumu mengine ya nyumbani nafanya kawaida kama mke.

Kila mara nafikiria uamuzi wa kuachana naye lakini najiuliza is it a right decision:

Naombeni ushauri ndugu zangu wenye uzoefu na haya mambo.

Nawakilisha na mnakaribiswa kwa michango yenu
Ndoa na changamoto zake chagua kuwa mvumilivu...mungu Yuko na makusudi yake kukupitisha katika hayo
 
Kwaio umeamua kuja kunitangaza hapa?
Sikuulizi kitu..
Utajuta utaona vitendo tu.
Hayawani mkubwa mie.
Acha kurisha watu kima wewe, hapo ndio akutane na mwanaume mwingine muanze kulia lia hovyo.
 
Aisee kuna watu wanateseka na hizi ndoa jmn wacheni..na still mtu unaomba ushauri ufanyeje na mtu kila kukicha anachepuka subir uletewe ukimwi.
 
Aisee ila kuna watu hawana ubinadamu. Kwa mwanamke akiwa ameshindwa kupata mtoto ni vibaya sana kumtamkia maneno kama hayonya kumkejeli hali yake ya kukosa watoto.

Aiseee maisha haya yanataka sana busara na hekima.
 
Back
Top Bottom