Anita Baby
JF-Expert Member
- Oct 2, 2011
- 1,265
- 541
unasubiri nini???? ungekua umezaa nae ungekaa kulea mtoti timka utapata mwingne huenda ukazaa na mtoti ya mungu mengi.
Kuna vitu vingine tunamsumbua Mungu bure.
Toka hapa...una matatizo sana ndo maana huzai
Habari za asubuhi wapendwa,
Mimi ni member wa Jamii Forum kwa muda mrefu ila nimesajili ID mpya kwa sababu maalum na hayo niliyooyandika ni ya kweli na ndio hali halisi
''Unaroho mbaya ndio maana huzai'' ''Najuta kwa nini nilikuoa wapenzi wangu wa zamani ni bora kuliko wewe'' nilikuoa kwa kukuonea huruma''. Haya ndio baadhi ya maneno ya kejeli ambayo nilishawahi kuambiwa na mume wangu.
Mimi ni mwanamke mwenye umri wa miaka 36, nimeajiriwa na mume wangu ana shughuli zake binafsi. Nina miaka minnne ndani ya ndoa ila sijabahatika kupata mtoto kwa sababu nimegundulika nina (Polycystic Ovarian Disease (PCOD) na mume wangu kuwa ana low sparm count.
Mume wangu amekuwa ni mtu wa kurudi usiku mara nyingi kuanzia saa sita, siku nyingine analala huko bila hata kuniambia na hata ukimpigia simu hapokei. Asubuhi anakuja anakuambia tulikuwa tuna biashara tunafanya na simu niliacha kwenye gari. Tukawa tunagombana kwa ajili hiyo hadi tukalifikisha kwa wazazi akagombezwa aakaacha kwa uda lakini karudia tena.
Siku moja alilala tena nje bila taarifa, nikampigia simu hakupokea, ilipofika alfajiri nikapigiwa na mwanamke simu akaniambia acha kusumbua waume za watu, niko naye hapa. Kama ni mumeo mbona hayuko kwako? Kidogo nizimie ila nikapiga moyo konde. Alivyorudi nikamuuliza akasema tulikuwa naye kwenye biashara kwa hiyo alikuwa na simu zetu.
Khaaa nikamwabia mdanganye mtoto ile sio mimi. Baada ya mwezi mmoja akanunua mzigo kumbe ulikuwa wa wizi akakamatwa na polisi, akaniambia mke wangu nimekamatwa kesho njoo polisi kijitonayama, hapo ilikuwa usiku. Kesho asubuhi naenda polisi kumpeleke breakfast nikaambiwa mbona mkewe kaja kuleta chai! Nikwwmbie polisi mbona mimi ndio mkewe halali? Nilidhalikika kwa kweli nikaondoka na chai yangu. Bahati nzuri nilikuwana ndugu zangu ambao ni polisi tena wana vyeo hapo kituoni, nikaweza kufuatilia hadi kesi ikaishia polisi.
Siku hiyo ya kutoka ilikuwa mida ya saa kumi na mojo, muda huo nilikuwa natoka kazini, nikawapigia maafande wakasema mume wako ameshatoka. Nikajaribu kumpigia simu yake haipatikani, kesho yake anarudi nymbani ananiambia polisi waliturudisha ndani. Nikamwabia acha uongo mie ndugu zangu walinihakikishia kama umetoka, akabisha katakata, ila mtu mwenye akili unajua ukweli.
Baada ya mwezi hivi nikwambia twende kwenye send off ya mtoto wa jirani yetu akadai amechoka, akaniambia huwa unapenda kushadadia vya watu wengine mbona mjomba wangu mke wake kajifungua hujaenda kumsalimia? ''Una roho mbaya na hutaweza kupata mtoto'' mimi huyoo nikaodoka zangu na majirani wengine. Kumbe siku hiyo walitibuana na huyo hawara wake.
Nimerudi kalala fofofo, simu yake inaita tuu. Kwa sababu yule mwanamke alishanipigia na kunitolea mbovu namba yake niliishika. Sikupokea simu kwa sababu sinaga tabia ya kupokea simu ya mume wangu.
Wazo likanijia nikaangalia messege, nikakuta huyo dada anamwabia kume una mkehukuniambia mimi na wewe basi. Kesho yake nikampigia huyo mwanamke akaniambie story yoote na ile siku aliyotoka polisi kumbe alilala kwake. Akanimbia mimi nilidanganywa na mumeo kwamba hana mke, na nilishawahi kuja hapo nyumbani pindi ukiwa umesafiri. Na kwa vile nimeujua ukweli simuhitaji tena huyo mwanaume, na roho inaniuma kutembea na mume wa mtu kitu ambacho kinaniumiza ila sikujua naomba unisamehe.
Pamoja na hayo yote anakataa katakata kuwa hana uhusiano na yule dada. Eti ''huyu dada ni girl friend wa rafiki yangu wamegombana ndio ananiforwadia hizi messege.''
Na hii sio mara ya kwanza alishawahi kuwa na mwanamke mwingine akamdanganya kuwa hajaoa hadi huyo mwanamke akaja nyumbani kuhakikisha ndio akaujua ukweli. Pindi anapokuwa na michepuko kejeli haziishi mara najuta kwa nini nilikuoa, nimekuoa kwa kukuonea huruma etc. Hizi kejeli huwa nikizikumbuka nakosa raha kabisa. Na tendo la ndoa tunaweza kufanya mara mbili kwa wiki kila akija amechoka.
Niko njia panda naona nimemchukia mume wangu ghafla, majukumu mengine ya nyumbani nafanya kawaida kama mke .
Kila mara nafikiria uamuzi wa kuachana naye lakini najiuliza is it a right decision:
Naombeni ushauri ndugu zangu wenye uzoefu na haya mambo.
Nawakilisha na mnakaribiswa kwa michango yenu

Dada sepa, i am speaking from my parents experience... mamangu aliolewa mwaka 83 mimi nikazaliwa mwaka 90 miaka yote 7 mamangu alivumilia matusi na kejeli za kila aina ila wen i was 3 enough was enough my dad alianza mletea wanawake ndani live eti mamangu awapishe wao wastarehe... 1 morning mamangu alinibeba mgongoni and we left bila nguo bila kitu chochote but she left..... i know she fought hard kunisomesha mpaka leo mimi nna kazi na wakati anaondoka kwa my dad hakua na kazi but as they say where there is a will there is a way. I look back na najiuliza wat if my mum asingeamua kuondoka maybe she would be dead coz ya depression na heart attacks but am grateful she is alive and she struggled. Men will always be men sometimes anakutukana una roho mbaya ndo maana huzai wakati anasahau yeye mwenyewe ana low sperm count. God has a purpose 4 everyone.... let him go and build ur life ukimtanguliza Mungu kwenye kila jambo. In the 7 years mamangu aliletewa watoto wa4 wa nje alee coz hazai na michepuko kila kukicha ipo mlangoni inamwimbia taarabu...... run and never look back.......... if he truly loved u he wouldnt treat u that way. Jenga maisha yako na umtumainie Mungu kamwe hatokuacha......
Pole sana dada mshukuru sana Mungu amekuonyesha tabia halisi ya mchumba wako mapemaDada hakuna lisilo shindikana chini ya jua.Nina face matatizo hama hayo sema mm ni mchumba.tuligombana nikaambulia maneno ya kejeli ambayo yananiuma mpak Leo.ikiwemo nilikuchumbia kwa huruma tu, ma ex wangu walikuwa bora,huna akili, yote nimepokea kwa mikono miwili na anataka kuvunja uchumba namtakia kila LA kheri.ila kinachonipa amani ni kusali na kufunga mungu anipe wa kufanana naye.kama wewe ni mkristo au muislam funga sali mwambie mungu kama huyo no mume aliyekupa bac ambadilishe, kama siyo bac akupe wakufanana naye.pray
wewe uliyesema haya maneno kama umemaanisasha utakiwa mchawi naomba sana mungu akushughulikie apendavo.mwanadamu gani unaroho mbaya hivo.
Asante sana ndugu yangu nadhani yana mwisho haya.Nashukuru kwa ushauri
Ni kweli mdada lakini kwa kisa chako nachelea kusema uaifanye huo ujinga wa kuondoka naona bado kuna room ya kuyazungumza na mwenzi wako jitahidi baadaye atapata ufahamu.
sabu vinaamulika kirahisi, hata akienda kwa kiongozi wake wa dini atamshauri kuwa aondoke kumbuka kuwa alishaonywa na wazazi akapumzika kwa mda ila ameendelea tena. ni bora uishi mwenyewe ila uwe na amani kwenye moyo kuliko kushambuliwa kila siku kwa weakness zako.Babu unafikiri mungu anasumbuliwa na nini kwanini tusimsumbue kwa vitu kama hivi?
Msihangaike na pepo. Binadamu hawezi kuwa hivyo.No, nadhani this is the stupidiest reply ever kwenye hii mada, ishu ya kuzaa au kutokuzaa kashaeleza huyu mwanamke sio vyema kumjibu kipumbavu hivi,wanawake mliokosa wanaume mbona mnakua na majibu mabaya hivi. sio yeye aliesababisha usiolewe dada, kua na staha na wanawake wenzako.
Mwanzoni alikuwaje? Au ndo ulifosi ndoa ? Pole lakini
mh!!! ninavyojijua mimi! ningekuwa hata nilishasahaugi kuwa niliwahi kuolewa na huyo mtu! kha! kama kuna kitu siwezi vumilia duniani ni 'kudhalilishwa'. Yaan...dah! BWANA niepushe na jaribu kama hili, maana wanijua vyema kiumbe wako! loh