Maneno haya Mochwari yanauma sana!

Maneno haya Mochwari yanauma sana!

Umenikumbusha biblia kitabu cha muhubiri

Muhubiri anasema kila kitu hapa duniani ni ubatili mtupu..Hamna Jambo la maana hapa duniani

Tunakula,tunashiba kisha tunasikia tena njaa,tunapata usingizi tunalala,tunaamka alafu tunalala tena..Unasikia genye, unagegeda unaridhika kisha baada ya Massa kadhaa unasikia tena hamu!!

Tunazaliwa,tunaishi,tunateseka na tozo alafu tunakufa..maisha yana maana gani sasa
Nawapenda sana watu wanaojifunza Biblia oya Be blessed sana.
 
Unavyokula kitoweo, iwe samaki au kuku n.k, na wewe utakuwa kitoweo kwa wadudu huko ardhini; vyote hapa duniani ni mbwembwe tu.
 
Kwa akili yako yakawaida kabisa kusifu na kuabudu 24/7 sio azabu? huko mbinguni kwenu nendeni wenyewe tu sitaki upuuzi mimi
Realm of the spirit ni tofauti sana na realm of physical bodies i.e in the spirit shouting is a weapon

Realm of this physical body ni manifestation ya spirit realm bahati mbaya mwanadamu ame base sana kwenye physical kama wewe unavyoona kusifu na kuabudu ni adhabu.

Spirit realm ina layers nyingi tofauti tofauti i.e lagalistic,light,sounds....

Again uelewa wa mwanadamu kuhusu Mungu upo katika layers tofauti ila layer ya chini kabisa ni realm of mercy,realm of love....the highest realm ni fear of God hapa ndipo Daniel alifika na alkua focal person mwenye funguo za siri za Mungu na aliambiwa azifunge aliyefanikiwa kufika hapo ni Paul baada ya Daniel.
 
Ukifikiria sana utagundua maisha hayana maana
 
HAYA MAISHA!

Siku ya kwanza nilipo ingia mochwari (mortuary), nilichokiona Ni ngumu mno kueleza. Kwanza niliona maneno yameandikwa (TULIKUWA KAMA WEWE) na kuelekea mlango wa kutokea niliona maneno yameandikwa (HIVI KARIBUNI UTAUNGANA NASI).

Kabla sijaendelea, niseme tu kwamba; Nataka kuwa Bora zaidi ya Jana yangu katika unyenyekevu, kusamehe, kupenda na kujali wengine, kumuabudu Mungu na kumtumikia. Kwa kuwa maisha niliyonayo Ni ya muda na tena kifo hakitazami status ya mtu.

Mh..! Kwa hakika niliogopa Sana kuona miili ya watu ikiwa imelazwa katika sakafu pasipo kufunikwa kitu. Miili mingine imelazwa katika vitoroli (Jerry cans), mingine katika meza za kuoshea maiti, mingine ndani ya majokofu. Kulikuwa na miili ya watu wa jinsia zote.
Tukaingia ndani zaidi kuelekea mahali ulipo hifadhiwa mwili wa ndugu yangu. Tulipoufikia mhudumu alifunua ulikuwa haujavishwa nguo na umelazwa juu ya ubao. Nilimuangalia Sana marehem akiwa amelala pale utupu, hakuweza hata kufunika utupu wake kwa mikono yake, Wala kupinga chochote kile. Nikajiuliza Sana NINI MAANA YA MAISHA.?

[emoji117]Kwanini tunatumia nguvu nyingi kutaka kumiliki kila kitu katika dunia hii na wakati mwingine hata kwa kuwaumiza wengine?

[emoji117]Kwanini tunakiburi, majivuno na ubinafsi Kama tunaimiliki dunia na pumzi ya uhai wetu?

[emoji117]Kwanini hatuwezi hata kuwasamehe watu wanaotukosea huku tukijihesabia haki kana kwamba Ni malaika?

[emoji117]Kwanini hatuwezi hata kumkumbuka Muumba wa Mbingu na nchi tunapokuwa hai?

Niliona matajiri waliokuwa na majumba, waliokuwa na degree na PhD, waliokuwa na magari ya kifahari, waliokuwa viongozi majasiri na mashupavu, matajiri na masikini, wanawake wazuri wenye mitindo mbalimbali ya nywele wote wakiwa wamelazwa humo ndani kimyaa
Nikajisemea moyoni kumbe maisha sio kitu na ni yamuda tu, cheo Ni Cha muda, utajiri na heshima vyote Ni vya muda tu.

Nimeipata mahali nikaona ni nzuri nawe uisome

C&P
 
Unavyokula kitoweo, iwe samaki au kuku n.k, na wewe utakuwa kitoweo kwa wadudu huko ardhini; vyote hapa duniani ni mbwembwe tu.
Afu unakuta kuna watu wanapiga marumaru pande zote za kaburi hawataki mbao za jeneza zigusane na udongo. Kama si uchoyo ni nini?
 
Kuna maisha baada ya kufa,tuyaamini maandiko.
Na maisha hayo ni mbinguni au jehanamu ya Moto .
Uchaguzi ni wetu,jinsi tunavyoishi hapa duniani ndo tunajiandaa kwenda mojawapo ya sehemu hizo
 
Tena dem akiwa na msambwanda na alikuwa anajichetua,akifika mochwar watu wana mnawa sanaaaa

Ova
 
Jamaa wanakuja. Wanakunywa. Wanakula. Muda unafika. Maneno ya porojo hapa na pale (wenyewe wanaita sala). Huyoo jeneza linashushwa ardhini. Wapendwa wako wanamwaga vimichanga vya uongo na kweli huyoo unafukiwa. Maneno tena ya faraja hapa na pale jioni inafika jamaa wanasambaa we unaachwa kimyaaa chini ardhini. Huko chini unajiozea na kuliwa na mafunza mpaka unabakia mifupa tupu. Inatisha sana!

Kuna jamaa niliona alizikwa jeneza lake likafunuliwa halafu akamwagiwa zege. Aliacha wosia kuwa hataki kuliwa na funza na kwa vile mummification ni gharama jamaa wakaona wamgandishe tu kwenye simenti huko huko chini. Sijui kama inasaidia kutoliwa na funza.

Yote kwa yote we uko kama mimi. Ikiwezekana nichomwe moto tu kwa wanaotaka wabakie na kimkebe cha majivu tu kazi kwisha. Tuandike will zetu mapema nkamu kungali na muda bado! 😁😁😁🖐🖐🖐
si bora uliwe na mafunza nkamu, mimi kinachoniogopesha kuwa ukiwa kaburini unaanza kutishwa sijui mavitu gani yanakuja hapo sasa ndo naishia kutetemeka.

Nkamu Watanzania unadhani hizi Will za uzikwe wapi na uzikweje wanafuata basi?? utasikia aliekufa kafa tuendelee na mazishi
 
Unaweza ku opt kuchomwa moto, ni uchaguzi unaofanya ukiwa hai. Nina experience ya ndugu alipigwa samli na kupigwa tanuru.
Naitamani sana hii kwa kweli nikizikwa nichomwe, walipewa ndugu majivu au yaliishia huko huko kwenye Tanuru??
 
Naitamani sana hii kwa kweli nikizikwa nichomwe, walipewa ndugu majivu au yaliishia huko huko kwenye Tanuru??
Walipewa kilo zao tatu za mtu wao, mke na watoto ndio walichukua. Sisi ndugu zake tukasema laanakum hatuhusiki na majivu yake, first time experience.. ila ukiifikiria kwa kweli inapunguza woga, kuzikwa, kuachwa mwenyewe six feet under, kuliwa na funza... aaggr!
 
Kama ulivyozaliwa ukiwa huna ufahamu wa jambo lolote vivyo hivyo ukifa ndio mwisho hautajua lolote na hakuna utakapoenda.

Yani ni mwisho mtimilifu. Dini hizi tu zimevuruga akili za watu.

Ukweli ndio huo.
Umejuaje wakati hujawahi kufa?
 
Heri waliokufa katika Bwana

Kristo Tumaini letu.
 
Hivi tukifa tunaenda kupumzika au ni adhabu/moto??

Maana hakuna aliyeenda akarudi
unaonaje ukaenda halafu ukatuletea mrejesho? usisahau kwenda na simu utuletee japo tupicha mkui
 
Nikiwaza kufa naona bora nisingezaliwa, naogopa sana sana hasa kufukiwa kaburini natamani hata kungewezekana mwili wangu ungechomwa moto naogopa mnooo
Wewe toa wosia tu kuanzia hivi sasa. Siku ukikata pumzi ulilosema ndilo litakalo fanyika.
 
Back
Top Bottom