Mandela Funeral: Live updates

Mandela Funeral: Live updates

NINAONA MGOGORO WA KANISA NA WAZEE WA KIMILA KATIKA KUANDAA MAZISHI SIJUI MMENOTICE WADAU?

Mazishi yalipaswa kuanza saa 4 ili kuruhusu hatua za kimila kufuata kuelekea njia ya kaburini, lakini Kiongozi wa Kanisa amehakikisha amekula muda wa kutosha ili tukio hili lisitokee, pia hajaondoka pale mbele inawezekana anasubiri kuchukua hatamu... sina uhakika hali itakuwaje nina hamu sana ya kujua jinsi watakavyobalanc makundi haya mawili ambayo yamekuwa yakizozana kuhusu utaratibu wa mazishi
 
Hatimaye Mwili ndo unapelekwa Kaburini... Watu maalum tu ndio watakao ruhusiwa kuhudhuria, jambo hili limeleta mgogoro mkubwa na majirani zake ambao hawajazoea kualikwa kwenye misiba wala kuambiwa eti huwezi kuhudhuria kama hujaalikwa? kidogo hili limewapa shida na bado litachukua muda kukaa akilini mwao...
 
Hivi kweli tukiziweka fikra zetu kuwa huru, Tutasema Hayati Madiba ni Shujaa wa Waafrika au Wazungu?

Ni shujaa wa wazungu kwa sababu amesimama imara kulinda maslahi yao.ndo maana wazungu wanampenda....Huyu sio Pan Africanist kama mwanaume Nyerere na Mugabe
 
Magazeti ya Tanzania ushuzi kweli, namwona Bishop Desmond Tutu anaelekea makaburini akiwa rasmi kama cleric leader. Kiko magazeti uchwara waliosema hajaalikwa?
 
Nasubiri kwa hamu kusikia yaliyojiri kaburini ambapo wazee wa kimila walijiandaa sana kwa taratibu nyingi za kiasili kwa ajili ya mazishi ya chifu wao...

Hata hivyo ninashawishika kusema kuwa Viongozi wa Kikristo wamefanikiwa kuteka nyara taratibu za mazishi... na je ule uvumi (sina vyanzo vya uhakika) kuwa Dume la Ngómbe litazikwa nae utaratibu huu utatimia????
 
Hata mie nimekodoa macho hapa ili tu kuliona hilo dume la ng'ombe!!

Kwa mbaaali nawaona wazee wa mila... au macho yangu??
 
Nimegundua pia hawa wa africa kusini kuna vitu vinawaunganisha kama taifa, Nyimbo ni kitu cha kwanza wanaziimba wote kwa pamoja. na ni za unyenyekevu na za ustadi si makelele ya kipuuzi.

Kila mara wametumia nyimbo kuvuta usikivu, hii inanikumbusha picha nilizowai ona za ukombozi wao jinsi walivyokuwa wakiimba bila shaka na naamini mchango wao katika tune ya wimbo wetu wa taifa.

Muziki si kangala, wana muziki wa tanzania jifunzeni na pia kuna wana muziki wanaoweza imba kwenye matukio kama haya ndo maana hatujaona akina mafiki zolo hapa.

Sasa Tz karibu wote ni mafiki zolo, si wa dini wala Bongo fleva.

Pili lugha yao.
 
NINAONA MGOGORO WA KANISA NA WAZEE WA KIMILA KATIKA KUANDAA MAZISHI SIJUI MMENOTICE WADAU?

Mazishi yalipaswa kuanza saa 4 ili kuruhusu hatua za kimila kufuata kuelekea njia ya kaburini, lakini Kiongozi wa Kanisa amehakikisha amekula muda wa kutosha ili tukio hili lisitokee, pia hajaondoka pale mbele inawezekana anasubiri kuchukua hatamu... sina uhakika hali itakuwaje nina hamu sana ya kujua jinsi watakavyobalanc makundi haya mawili ambayo yamekuwa yakizozana kuhusu utaratibu wa mazishi
Huu mgongano wa mila na imani kwa waafrika ni kitu cha kushangaza sana.Mila zetu nyingi zinaambatana na mauzauza.Hii huwa inajipa jibu kuwa waafrika huingia kwenye dini kama fashion tu ili tuonekane wa kisasa lakini mila ambazo zinaconflict imani huwa hatuziachi
 
hatimaye Pro wetu anafanya vitu vyake huku kwetu, asante kwa hii streaming
 
Jamani............kama ni Heshima Mandela kazikwa kwa heshima sana...............
 
Yan kijijin kwao mandela ndio kuzuri hivi over moro mjini...lol
 
Wanafamilia na viongozi wa serikali na baadhi ya watu wachache walioalikwa ndio wapo eneo atalozikwa Madiba.

Jeneza limeshawekwa juu ya kaburi, nadhani kinachosubiriwa na utaratibu wa ibada...
 
Bendera inatolewa katika jeneza, inakunjwa na wanajeshi tayari kukabidhiwa kwa mjane wa Madiba Bi Graca Machel hapo baadaye.
 
Back
Top Bottom