Ahmed Omar_
Senior Member
- Jul 17, 2012
- 128
- 195
Na Ahmed Omar
Utangulizi
Historia mara nyingi huwakumbuka na kuwaandika kwa wino mwekundu viongozi wanaotatua matatizo ya kisiasa kwa matumizi ya njia za amani. Wakati Nelson Mandela alivuka mstari wa uchungu wa ubaguzi wa rangi na kuiunganisha nchi ya Afrika Kusini iliyokuwa imegawanyika, Rais Dk Hussein Ali Mwinyi kwa upande wake tokea hajaingia madarakani, amekuwa na bado yungali akitetea siasa za maridhiano na jumuishi kuwa ndio muarubaini kwa utulivu wa Zanzibar.
Mpito wa Amani
Nelson Mandela na chama chake cha African National Congress (ANC), waliondoa ubaguzi wa rangi kupitia upinzani baridi, usiotumia fujo wala silaha bali mazungumzo yaliyozihusisha pande mbili hasimu. Kufuatia kuachiliwa kwake kutoka katika kifungo cha miaka ishirini na saba (27) jela mwaka 1990, Mandela aliingia rasmi katika mazungumzo magumu na viongozi wa utawala wa kibaguzi chini ya Rais FW de Klerk. Mazungumzo hayo yaliweza kumaliza mgogoro wa kihistoria na ubaguzi wa rangi nchini Afrika ya Kusini na hatimae kuingia katika enzi mpya ya kuheshimiana, huku haki na usawa ikitamalaki bila kujali tofauti za rangi na makabila.
Siasa ya Rais Hussein Mwinyi ya kuibadilisha Zanzibar kutoka katika misukosuko ya kisiasa ya miongo mingi, hadi katika hali ya kuishi kwa pamoja kwa amani, inalingana sana na ile ya Nelson Mandela. Rais Mwinyi amekuwa akidhihirisha kwa fikra na vitendo kwamba Zanzibar ni taifa la makabila na mawazo mseto (‘Rainbow Nation’), hivyo haiwezi kutawalika bila ya siasa jumuishi za maridhiano. Rais Mwinyi atakumbukwa kwa kufanikisha maridhiano na Marehemu Maalim Seif na Chama chake cha ACT-Wazalendo, baada ya uchaguzi uliokuwa na vurugu wa mwaka 2020. Tokea kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, uchaguzi ambao Chama cha ACT-Wazalendo kiliuita ‘usio wa haki’ na kugomea kuingia katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa, Rais Mwinyi bado anaendelea kuitandika meza yake ya maridhiano na kuwakaribisha wapinzania wake kuketi na kuzungumza.
Kama ilivyokuwa kwa Nelson Mandela na juhudi za kuponya makovu ya kihistoria ya Afrika Kusini, Rais Hussein Mwinyi amewaunganisha kwa ustadi watu wa Zanzibar kutoka katika migawanyiko mikubwa ya kisiasa. Kupitia Serikali ya Umoja wa Kitaifa na maelewano ya kijamii, Rais Mwinyi amethibitisha kuwa uongozi wa kweli hauko katika kuwatawala wapinzani wa kisiasa, bali katika kuwaleta pamoja kwa manufaa ya nchi.
Serikali ya Umoja wa Kitaifa (GNU)
Serikali ya Umoja wa Kitaifa nchini Afrika ya Kusini ilianzishwa mwaka 1994 kama sehemu ya Katiba ya Muda ya nchi hiyo ili kuhakikisha mpito wa amani kutoka katika zama za ubaguzi wa rangi hadi demokrasia ya kweli. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ilionekana ni jambo la lazima la kugawana madaraka ambayo iliundwa kufuatia uchaguzi wa kwanza wa nchi hiyo ambapo Nelson Mandela alikuwa Rais na FW de Clerk kuwa Makamo wake.
Kwa upande wa Zanzibar, pamoja na kambi ya upinzani kujaribu mara kadhaa kujitenga na Serikali ya Umoja wa Kitaifa ambayo ni sharti la Kikatiba, kwa sababu zinazohusiana na chaguzi, Rais Mwinyi amekuwa akisisitiza haja na umuhimu wa kuendelezwa kwa Serikali hiyo. Katika vipindi vyote viwili alivyoingia madarakani, mwaka 2020 na mwaka 2025, Rais Mwinyi amesisitiza nia yake ya kuwa na maridhiano ya kisaisa na kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa kama nyenzo muhimu ya kuhakikisha umoja na amani hapa Zanzibar. Hii bila shaka ni kwa sababu kambi mbili kinzania za kisiasa zinapokuwa pamoja serikalini, masafa baina yao huwa mafupi na fursa ya mazungumzo huwa pana.
Moyo Mtulivu na Kusamehe
Nelson Mandela katika kitabu chake alichokiita “The Long Walk to Freedom,” anaeleza mkasa wa jinsi alivyopokea mateso kutoka kwa askari jela ambae wafungwa walimwita kwa jina la Mr. ‘Suit’ kwa ‘uhabithi’ wake. Kufuatia uongozi wa gereza kubaini kuwa Mr. ‘Suit’ alikuwa akimtesa Mandela bila ya sababu pamoja na kwamba Mandela alikuwa mfungwa mtiifu gerezani, Mr. ‘Suit’ alipewa adhabu ya uhamisho wa kikazi. Mandela anaeleza kuwa alimsamehe Mr. ‘Suit’ kabla ya kuhama katika gereza lao. Kwa moyo wa kawaida na siasa za malipizano ya visasi zilivyo, wengi walitegemea kuwa Mandela baada ya kuwa Rais angelipiza kisasi chake dhidi ya jamii ya watu weupe hasa wale waliohusika na mateso makubwa na mauwaji dhidi ya jamii ya watu weusi wa Afrika ya Kusini. Kinyume chake, Mandela alitoa mkono wa msamaha kwa watesi wake na kuanzisha zama mpya ya kuishi kwa amani baina ya jamii ya watu weupe na jamii ya watu weusi wa Afrika ya Kusini waliokuwa wakikandamizwa hapo kabla.
Rais wa Zanzibar Dk Hussein Mwinyi kwa upande wake, kama alivyo Nelson Mandela, amejijengea sifa ya uvumilivu wa kisiasa na msamaha, kwa makusudi kukataa kulipiza kisasi au kuwatukana hadharani wapinzani wake. Mtazamo wake unasisitiza ushirikishwaji, umoja wa kitaifa, na upatanisho, kuweka sauti ya upatanisho hata anapokabiliwa na ukosoaji mkali wenye lugha za kejeli, matusi na ubaguzi wa kinasaba dhidi yake. Rais Mwinyi anajulikana kwa kutowahi kuwadhihaki wapinzani wake wa kisiasa. Tabia hii ya utulivu imekuwa kipengele muhimu kinachofafanua vyema mtindo wake wa uongozi tokea alipoingia madarakani mwaka 2020.
Falsafa ya Uamalia
Serikali ya Nelson Mandela, ilijifafanuwa kwa falsafa ya Umalalia (pragmatism), yaani kujikita zaidi na mambo yanayoonekana kwa mamcho na kutekelezeka. Mandela alitanguliza ujenzi wa taifa na utulivu wa kiuchumi badala ya ufuasi mkali wa kiitikadi. Licha ya imani yake binafsi na uungaji mkono wa kihistoria wa ANC katika sera ya utaifishaji, Mandela alipitisha mfumo wa uchumi wa soko huria ili kuuokoa uchumi wa nchi. Mwaka 1996, alianzisha mkakati uliolenga kubana matumizi ya fedha, ubinafsishaji, na kuvutia uwekezaji wa kigeni ili kuleta utulivu wa uchumi baada ya miongo mingi ya ubaguzi wa rangi. Alijihusisha sana na taasisi za fedha za kimataifa na alitaka kikamilifu kurejesha mtaji wa kimataifa ambao ulikuwa umekimbia Afrika Kusini wakati wa enzi ya ubaguzi wa rangi.
Rais Hussein Mwinyi kwa upande wake, amejikita na uongozi wenye kutenda badala itikadi na sera za maandishi. Utekelezaji wa miradi mbali mbali ambayo inaonekana na kila mmoja huku athari yake kwa wananchi ikipimika. Ametekeleza sera ya Uchumi wa Buluu kwa vitendo kwa kuimarisha sekta za uvuvi, usafiri wa baharini, na utalii endelevu, ili kuboresha moja kwa moja maisha ya wananchi. Utawala wake umetanguliza mtaji wa watu, kuboresha elimu kupitia ujenzi wa skuli za kisasa, majaribio za elimu kidijitali, ujenzi wa hospitali mpya na vituo vya afya, utitiri wa miundombinu ya mawasiliano na kupata uwekezaji wa kimataifa katika miradi ya maji na miundombinu.
Taasisi Madhubuti
Serikali ya Nelson Mandela iliunda taasisi madhibuti. Taasisi moja muhimu ilihusika na kuimarisha na kulinda demokrasia kwa kuchunguza na kurekebisha kasoro mbali mbali za uongozi, utawala mbovu na ufisadi katika utendaji wa serikali. Mandela alianzisha Tume ya Haki za Binadamu ili kukuza mazingatio, ulinzi, na upatikanaji wa haki za kimsingi za binadamu nchini Afrika Kusini. Alianzisha taasisi ya maendeleo ya kiuchumi ambayo iliileta serikali karibu na wananchi, na hivyo kuwa meza muhimu ya kujadili na kutatatua changamoto za masuala ya ajira na biashara.
Kwa upande wake, Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi, anajipambanua kwa uongozi wenye misingi ya taasisi imara. Mtazamo wake wa kimantiki ulihama kutoka katika utendaji mbovu wenye urasimu, uliozoeleka na serikali zilizotangulia huko nyuma, na kuelekea katika utendaji wenye uwajibikaji. Uimarishwaji wa taasisi za ukusanyaji kodi umekuwa ni uti wa mgongo wa mageuzi ya kifedha serikalini. Udhibiti wa ndani ulioimarishwa na uwekaji wa mifumo kodi ya kidigitali, umezuia ukwepaji wa kodi na kuongeza mapato ya ndani, na kuiwezesha Zanzibar hata kufadhili sehemu kubwa ya miradi yake yenyewe. Wizara ya Uchumi wa Bluuu na Uvuvi ni moja ya taasisi imara serikalini na ambayo inaendesha matumizi endelevu ya rasilimali za baharini (utalii, uvuvi, bandari na mwani) kwa mafanikio makubwa. Uchumi wa Buluu uliojengewa mazingira bora ya kisera, kitaasisi, kitaalamu na kiutendaji, umefanikiwa kwa kiwango kikubwa kuvutia uwekezaji wa kigeni na miundombinu ya kisasa ya baharini.
Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi Zanzibar, (ZAECA), imefanikiwa kudhibiti rasilimali za umma, na hivyo kusababisha urejeshaji wa fedha zilizoibiwa na kuongezeka kwa ripoti safi za ukaguzi katika sekta zote za umma. Mahakama za Zanzibar zimefanyiwa maboresho makubwa ya majengo yake, majengo mapya kujengwa, kupewa mifumo ya kisasa, kuongezwa kwa majaji maalum na usimamizi wa kesi kidijitali, zimepunguza kwa kiasi kikubwa mrundikano wa kesi na kuwafanya wananchi kujenga imani kubwa na mchakato wa kisheria wa Zanzibar. Programu ya ‘Sema na Rais’, utaratibu bunifu wa kutoa malalamiko na maoni ulioanzishwa na utawala wa Rais Mwinyi, wenye lengo la kufuatilia malalamiko ya umma kuhusu ofisi zote za serikali, ni kielelezo muhimu cha uimara wa kitaasisi katika uongozi wake.
Vita Dhidi ya Ubaguzi na Upendeleo
Nelson Mandela aliusambaratisha mfumo mzima wa utabaka na upendeleo wa kijamii wa Afrika Kusini. Alipasisha sheria maalum iliyofutilia mbali mfumo wa ubaguzi wa rangi na kusimika mfumo wa demokrasia jumuishi. Mkakati wake ulichanganya mbinu za majadiliano ya kisiasa na kuanzishwa kwa Katiba ya 1996 ili kuharamisha ubaguzi wa rangi, na kukuza maridhiano ya kitaifa ili kuziba migawanyiko ya kihistoria.
Utawala wa Rais wa Hussein Ali Mwinyi kwa upande wake, unapinga vikali aina zote za ubaguzi wa kijiografia na kisiasa kati ya Pemba (Upemba) na Unguja (Uunguja). Tangu aingie madarakani, Dk. Mwinyi amekuwa akitetea serikali jumuishi na maendeleo ya kiuchumi yenye uwiano, akiwaonya wanasiasa dhidi ya kutumia matamshi na vitendo kuchochea mgawanyiko baina ya visiwi viwili.
Katika uongozi wa Dk. Mwinyi, suala la kuchagua uongozi wa kisiasa na watendaji ni la kisera. Rais Mwinyi amekuwa akichagua viongozi na watendaji wa serikali kwa kuzingatia sifa stahiki na sio asili au ukanda ili kuhakikisha tija katika utumishi sambamba na kuhakikisha visiwa viwili vya Unguja na Pemba vinawakilishwa bila upendeleo. Ili kukabiliana na tofauti za kihistoria, kisiasa na kiuchumi, utawala wake umeelekeza uwekezaji mkubwa wa miundombinu kisiwani Pemba ikiwa ni pamoja na ujenzi wa uwanja wa ndege wa kisasa, kupanua bandari za Wete na Mkoani na ujenzi wa bandari mpya ya Shumba.
Utawala wa Rais Mwinyi’ unatetea kikamilifu maridhiano ya kitaifa ili kuondoa chuki ya kihistoria na madai ya upendeleo wa kikanda, akiendelea kusisitiza kuwa watu wa Unguja na Pemba ni ndugu moja na wanahitaji kuungana katika kuijenga Zanzibar yenye mafanikio. Rais amerudia mara kwa mara kuwataka viongozi wa dini na waandishi wa habari kuwawajibisha wanasiasa, na kuhakikisha kuwa hotuba na matamshi yao yanazingatia maendeleo na umoja badala ya ubaguzi wa kikanda.
Uongozi Unaoacha Alama
Nelson Mandela ameacha alama kubwa ya uongzi wake ambayo imekuwa ni urithi muhimu wa vizazi na vizazi. Alama muhimu iliyoachwa na Nelson Mandela ni uongozi wake unaozingatia jukumu la kuleta mabadiliko ya utawala kutoka mfumo wa kibaguzi wa Afrika Kusini kwa amani na maridhiano badala ya fujo na kulipiza kisasi. Hili ni funzo gumu kwa wanasiasa duniani kote. Mandela anatufunza kuwa migogoro ya kisiasa inatatuliwa kwa kutanguliza huruma, msamaha na ushirikishwaji.
Rais Mwinyi kwa upande wake, atakumbukwa kwa kuondoa mkwamo wa kisiasa, kuirejesha Serikali ya Umoja wa Kitaifa, kuunganisha mirengo ya kisiasa iliyokuwa imevunjika hapo awali. Ubunifu wake wa kuleta kwa mara ya kwanza Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar, iliyoanzisha utalii wa baharini, uvuvi wa bahari kuu, ufugaji wa samaki na mwani kama nguzo za ukuaji endelevu wa uchumi ili kupunguza utegemezi wa utalii, utakumbukwa milele. Utawala wake umetumia mabilioni ya uwekezaji katika kuboresha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, kujenga maelfu ya madarasa mapya, skuli nyingi za kisasa, na kujenga vituo vyenye athari kubwa katika masiaha ya watu na uchumi wa chi kama vile Bandari ya Mpigaduri, bandari ya Mangapwani na mifumo mikubwa ya usambazaji maji safi. Uongozi wa Dk. Mwinyi’ umezifanya huduma za serikali kuwa za kisasa kwa kuweka mifumo ya kodi ya kidijitali, rekodi za ardhi na usajili wa biashara.
Ameanzisha ubunifu wa uwekezaji wa kifedha kama vile mpango wa SUKUK kwenye Soko pana la Hisa la Dar es Salaam. Zaidi ya hayo, ameendesha mipango ya kuhakikisha wananchi wenyewe wanakuwa ni wanufaika wa moja kwa moja na wawekezaji katika miradi mikubwa, badala ya kubaki watazamaji tu wa uwekezaji wa kigeni. Suala muhimu la uwezeshaji wa wananchi kiuchumi limepewa nafasi na umuhimu maalum katika Serikali ya Dk. Mwinyi. Mpango huo unaolenga katika uibuaji wa ajira, ujasiriamali na ukuzaji wa uchumi jumuishi ni kielekezo muhimu cha uongozi wa Dk. Mwinyi. Sera zake za kiuchumi zimekuwa zikiwalenga moja kwa moja vijana na wanawake kupitia mipango ya kifedha, miundombinu ya kisasa, na ukuzaji wa ujuzi wa ujasiriamali ili kukabiliana na ukosefu wa ajira na kuondoa umasikini.
Hitimisho
Kama Wazanzibari tumeona sababu lukuki zinazotupa nafasi ya kutamba na kujigamba kwamba uongozi wa Rais Hussein Mwinyi unalingana sana na ule wa Nelson Mandela. Wawili hao watakumbukwa kutokana na kufanikiwa kwao kutekeleza maridhiano ya kisiasa na kurejesha siasa jumuishi. Rais Mwinyi ameimarisha urithi wa mshikamano wa kijamii ambao unalingana na maono na falsafa ya Nelson Mandela kwamba tofauti za kisiasa haziwi chanzo cha migogoro na mkwamo wa nchi. Kwa kutanguliza amani, maridhiano na maendeleo jumuishi ya kijamii, kiuchumi na kisiasa, Rais Mwinyi amedhihirisha kwamba maadili ya msingi ya Mandela ya umoja na haki yanasalia kuwa zana zenye nguvu kwa utawala wa kisasa barani Afrika.