Forgotten
JF-Expert Member
- Jul 20, 2018
- 3,630
- 11,098
Tunarudi palepale wachezaji wa United wasingeweza kufanya vizuri kwenye mfumo wa Gegenpressing.Sio complete package , namaanisha Coaching+Talent ID , unamuona Raph Rangnik yule ni Talent ID ,ila kwenye coaching ni wakawaida
Rangnick ni kocha mzuri tatizo idea zake zisingeweza kufanya kazi kwa wachezaji wavivu.
Mechi ya kwanza ya Rangnick pale United vs Crystal Palace 1st half ndiyo tulishuhudia ile Gegenpressing yenyewe. 2nd half wachezaji wote wakakata upepo.
United wanaweza tu quick transition na counter attack. Quick transition ni kumuacha tu adui akushambulie na pale atakapopoteza tu mpira pasi zinaanza kutembea kutoka kwa mabeki, viungo, mpaka kuwafikia washambuliaji.
Counter attack haina pasi nyingi mara nyingi juu anakuwa mshambuliaji mmoja tu ndiyo mambo ya Bruno na Rashford: mara ya mwisho pale OT ndiyo mlifungwa kwa aina hii maana mlikuwa mkijisahau karibia wachezaji 8 walikuwa wanavuka mstari wa kati.
Sasa Gegenpressing inahitaji watu wenye work-rate kubwa yani mkipoteza tu mpira mnautafuta kwa lazima na mnakaa nao (possession). Wachezaji kama Ronaldo, Martial, Sancho wasingetoboa.
Rangnick ni complete package unapokuwa unam-judge kocha angalia na aina ya wachezaji aliokuwa anafanya kazi nao ni lazima angefeli kama wengine tu.










