Ni mechi nyingi sana msimu huu tumetoka uwanjani "kwa asante De Gea" , team imeoza kuanzia mabeki, viungo, huko mbele ndio viazi kabisa.
Hizo game zote ulizotolea mfano tulifeli kwasababu ya hesabu za kocha katika sub, wala haikuwa kawasababu De Gea alikuwa anapoteza possession.
Mechi kama ile tuliyopigwa goli 4 na BENTIFORD utasema ni kipa? Ila ya Liverpool tuliyokula goli 7 utasema ni kipa? Zile goli 6 za City utasema ni kipa? Ile game tuliyosuluhu na Crystal palace licha ya kuongoza goli moja tulipigwa msako mkali sana tukapona kwasaabu ya De Gea.
Mechi zetu dhidi ya Spurs, Sevilla, Barca, ARSENAL (ile ya 3-2) na nyingine nyingi, ni mechi tulizopoteza kipumbavu licha ya kutangulia kwasababu ya ujinga wa Ten Hag kwenye sub zake. Ni mara chache sana Ten Hag apige hesabu za kufanya sub kisha zifanikiwe.
Kwa mfano wa mechi ulizotoa bado sio sawa kumtupia lawama De Dea.
ITAFUTWE SABABU NYINGINE GENUINE, SIO KUSEMA DE DEA NI KIPA MBOVU.