️ Tatizo ni Ronaldo
️ solved
️ Tatizo ni Wachezaji hawajitumi
️ solved
️ Tatizo hatujafanya usajili
️ solved
️ Inatakiwa mchezaji mwingine wa kumsaidia Rashford asajiliwe (Mzee ferg alisema baadhi ya mashabiki ku bet wakaanza mponda)
️ Manchester kuna tatizo kubwa sana kuna wachezaji ambao hawatakiwi kuwepo pale kabisa,kocha akaongeza wengine
️ Tatizo Ferg anaingilia maamuzi ya kocha (Mashabiki ku bet)
️ Tuna bonge la kocha (Mashabiki ku bet baada ya kula mikeka kadhaa)
️ Europa yetu (Mashabiki ku bet baada ya kuchukua Carabao)
Alafu kuna sisi
"Ten hag ni bonge la kocha ila hawezi kuwa kocha wa United,united ni kubwa sana kwake,kocha ana Ego sana na ana dharau wapinzani na anaamini yeye ndio kila kitu amesahau hamna kijiji kinachokosa wazee,Manchester united sio Academic au Ajax,EPL sio ligi ya uholanzi huku ukiingia kwenye mfumo hata Newcastle inaweza kukupiga 7" baada ya siku chache Liverpool mbovu ikatupiga 7,
NB:Mimi naamini Ten hag ni bonge la Kocha tuendelee nae tunaweza chukua World cup