Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Pengine msimu ujao munaweza kuwa na timu nzuri ikiwa mutapata mwalimu sahihi.

Nafikiria kuwa mshabiki wa NAPOLI.


DAEMUSHIN = M Z A N Z I B A R I
Potter ni kocha mzuri anayehitaji muda potter kaja chelsea kaikuta tuna injuries ya wachezaji 8 Ngolo Kante, Kovacic Fofana, James,Chillwel Mendy RLC na Pulisic hajakaa Sana kuletewa wachezaji wapya kwenye dirisha dogo Enzo Hernandez, Mudryk, Madueke, Bachishile, dafro Fofana na jao felix kwa namna hiyo kwanini asipate matokeo mabaya? Umeona sasa hivi umeanza kupata kikosi chake Cha kwanza na unaona kabisa team imeimarika kulinganisha na Mwanzo tumeshinda mechi Tatu mfululizo Tena ngumu na tumecheza vizuri Sana. Usimuunderstimate Potter mkuu
 
Labda huwa tunawaza kutengeneza headlines kwa Fergie time au come back kings
Kuna siku unafanyiwa suprise mfano ile ya liverpool, unategemea second half kurudisha energy ya upambanaji hatimaye unaongezwa goli mbili za haraka za kukutoa mchezoni.

Mechi ya leicester
Mechi ya west ham - FA

kipindi cha kwanza tulikuwa ovyo, tukaokolewa na ubutu wa wapinzani wetu
 
Binafsi namkubali Potter,ni suala la muda tu chemistry ikikaa vema mtarudi juu.
Hata MZANZIBARI kipindi cha nyuma alikuwa shabiki wake kabla hajatoka Brighton.
 
Ile siku ya 7UP uliona kabisa tunavizia jamaa wapunguze tempo ya mchezo kwa kutuhofi form yetu,bahati miungu ya mpira haikuwa upande wetu.
 
The boss has praised the work rate of his side after playing an hour with 10 men against Southampton.

#TrustTheProcessETH

#UnitedfortheFans

#GlazerOUT

#GGMU


man utd |
 
Lakini unaisemea vipi hali ya uchovu wa mechi nyingi mfululizo pamoja na mabadiliko ya kikosi cha kwanza mechi hadi mechi kwenye kile kipigo?
Bado hatuna uwezo wa kwenda nguvu kwa nguvu dhidi ya liverpool kimpira,

hivyo hatukuadhibiwa kwa sababu ya uchovu siku ile bali liverpool waliamua kupasha kiporo chao cha ubora japo kwa asilimia 60, walikimbia zaidi yetu, walifika kwenye eneo la mpira zaidi yetu, waliharibu nguvu yetu ya kushoto (martinez amekuwa injini yetu ya kusambaza mipira)

Kuna makosa mengi sana walifanya liverpool lakini hatukuwa wakatili.
 
Nilibahatika kuangalia mechi ya arsenal dhidi ya manchester city kwa kipindi kimoja usiku ule.

Nilichojifunza ili uwe na uhakika wa kumdhibiti adui yako ni lazima uwe na uwezo wa kupambana naye jino kwa jino wakati wowote,

ni nyuma tu hapo arsenal alikuwa anakula goli 3 mpaka 5 kwa mechi dhidi ya manchester city na hata liverpool

Naisubiria mechi yao ya pili ya marejeano, kama arsenal wataweza tena kwenda head to head na manchester city kimpira basi rasmi nitamweka mikel arteta katika kundi hili:
  1. Manchester city
  2. Liverpool
  3. Arsenal
Top 3 zenye uwezo wa kuadhibiana muda wowote kimpira.

Kimatokeo hata spurs anamfunga sana manchester city
 
Kama kawaida yetu huwa tunatengeneza nafasi 5 tunafunga 1 au 2 halafu hatuangalii nyuma. Siku ile sio kwamba Liverpool walitumeza sana ila tulikosa magoli mengi ya wazi hadi pale walipopata mwanya wa kutuadhibu na kututoa mchezoni. Kama sio suala la uzalendo wa Kiingereza,Rashford hafit kwenye mfumo wa 10hag ila muda ni mwalimu mzuri.

Ile kazi ya kukaba anayoifanya Anthony haiwezi kufanywa na Bisaka halafu Pellistri akafanya kazi ya kusukuma mipira kwa Ghost Letu pale mbele?
 
Walikuwa na accuracy ya 87.5% kwenye mashuti yao langoni mwetu.

Lakini unaisemea vipi hali ya uchovu wa mechi nyingi mfululizo pamoja na mabadiliko ya kikosi cha kwanza mechi hadi mechi kwenye kile kipigo?
Hata mngepumzika mwaka mzima
Bado tungewapiga nje ndani.

Karibu seven up Mkuu.
 
Sio kwa chuki kwa gunners pamoja na mpira mzuri wanaocheza leo hii binafsi sijashawishika kama ni suala endelevu kuwakuta wakiwa juu misimu 2 mfululizo kama ilivyo kwa city na liverpool. Kwa msimu huu ubora wa city umeshuka na liverpool ndio kama unavyoona tena.
Wameimarika lakini hawajafikia kiwango cha hao wawili,falsafa yao ni umiliki na recruitment yao wanaangalia technical ability ya mchezaji ndio maana wanafanikiwa kupishana na city uwanjani. Ukija upande wetu sasa,baada ya MARTINEZ,ERIKSEN na kidogo Bruno wengine wote wanaogopa mipira kama kiazi cha moto mdomoni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…