Leo makarani wa sensa wamekuja home huku wanachekacheka, nikawakaribisha ndani na kuwapatia vinywaji walainishe koo ili zoezi lianze.
Badala ya kuanza kuniuliza maswali namuona karani yuko na furaha kinyama ikabidi nimuulize kulikoni?
Akanijibu kwani we kaka haujui kua leo mchana Manchester United ipo uwanjani?
Nikamjibu nafahamu hilo ila muda huo si mtakua mnaendelea na zoezi la kukusanya takwimu?
Akanijibu kua Tume kwa kutambua uzito wa Manchester United Vishikwambi vyote vinavyotumika kwenye zoezi zima la sensa vimeunganishwa vitakua vinaonyesha mechi live hivyo muda wa mpira ukifika wameambiwa wapumzike waangalie timu kubwa zaidi duniani inavyotoa burudani kwa ulimwengu mzima bila ya kubagua dini, kabila, rangi wala jinsia.
Hapo ndio nikaamini yale maneno ya
allypipi
"Manchester united inacheza leo na dunia nzima ina furaha


"