Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

kwa sasa klabu inatafuta mshambuliaji wa kumuondoa taratibu CR7, timu yetu haina nguvu ya kusajili mchezaji anayegombaniwa na wakubwa hivyo haitowezekana kumuondoa ronaldo bila ya uhakika wa kusajili. kipaombele cha klabu ni harry kane na kama itakuwa ngumu wanamuangalia nunez au richarlison.bahati ikianguka kwetu tunakwenda kwa haaland anayewindwa na guardiola.
Kane? Duh! Why tusipumzike kwa waingereza tusake kwingine
 
hakuna chanzo chochote cha habari za uhakika kilichoripoti taarifa za CR7 kutohitajiwa na kocha ajaye, kwa kuwa hii habari imetokea upande wa ten hag nilitegemea vyanzo viwili vya habari zinazohusu uholanzi hususan klabu ya AJAX wangelitupa tetesi hii lakini mpaka muda huu wapo kimya, kwa taarifa za uhakika zinazohusu ajax na ten hag chanzo kikuu aminifu ni MIKE VERWEIJ na hata jana katika interview ya ten hag akizungumzia maandalizi ya fainali itakayochezwa hapo kesho huyu jamaa alikuwa anamchokonoa sana ten hag kwa maswali yake yanayohusu zaidi tetesi za man utd kuliko maandalizi ya ajax kuelekea fainali. Kwa asiyefahamu huyu bwana ndiye mtu wa mwanzoni kuja na taarifa zinazohusu ten hag kuwa mstari wa mbele kutakiwa na man utd na hata ishu ya ten hag kufanyiwa mahojiano na man utd ndio chanzo cha mapema kuripoti kwa waandishi wasioripoti habari za man utd, vyanzo vyengine muhimu kwa taarifa za man utd ni james ducker wa telegraph, laurie whitwell wa the athletic , david ornstein wa the athletic na simon stone wa bbc (huyu pia anaripoti habari za man city). Kati ya hao ni yupi alieripoti taarifa ya ronaldo kutohitajiwa na ten hag?... Basi hata hawa akina mark ogden wa espn,mwanadada charlotte ducker wa goal.com nao hawana ubuyu huu walionao daily...... pekee wakitiwa nguvu na sky sports?
Subiri baada iyo fainali utaona izo habari jamaa alisema ana focus na fainali haitaji kusumbuliwa na izo story
 
Ronaldo tunakusema lakini unatuokoa sana mkuu tunashukuru sana kwa msaada wako. Ronaldo haiangushi team ila timu inamuangusha Ronaldo.

Hahitaji hata kukaba kama watu huko nyuma wanafanya kazi zao inavyotakiwa akae tu pale washushe cross apige suuuuiu siku imeishaa.
Labda tupate mshambuliaji wa maana msimu ujao sawa Ila kama watabaki hawa kina Rashford ni mara mia 600 aendelee kukaa pale mbele.
IMG-20220415-WA0010.jpg
 
Mzee sijampangia, hizo sifa ulizosema ndio zinafanya tutake aondoke maana kwa hizo sifa itakua ngumu kucheza soka la muunganiko, mchezaji akikosea shuti mnaaza si angempa Ronaldo, mara mchoyo mpaka mchezaji anakosa kujiamini, Ronaldo akifunga tufungwe blame inaenda kwa wengine yaani collective responsibility inapotea sasa kwa mwendo huo Man U tutafika wapi kisoka? Lini tutacheza kitimu?
Kabla Ronaldo tulikuwa na hali gani?
 
Wewe una wenge mkuu, tulia kwanza mana unaposema rekodi binafsi sijui unataka kumaanisha nini, mtu anafunga na ana njaa ya kufunga ulitaka asifunge kuogopa nyie mtasema anataka tunzo binafsi? Takwimu zimetoka zinaonesha asipocheza Ronaldo timu inazingua, haya ulitaka afanye nini? Acheni kukariri.
Umesoma vizuri?

Nimemkataza kufunga?

Nachosema za way alivyo ni vigumu kupata timu ambayo wachezaji wapo for team kuliko wao binafsi.

Ikiwa kila mtu anataka apate sifa how about our club?

Individual brilliance vs teamwork ipi poa?
 
Maguire kwanza hapaswi kuongelewa in future tense anapaswa kuondolewa ikiwa tuna nia na kuijenga timu ya ushindani. Kumuacha ni kusababisha media za kiingereza kuwaharibu kisaikolojia kina TIMBER wapya wanaochukua no yake.
namuona akivuliwa kinga ya unahodha na baada ya hapo atagombania namba. kwa performance yake ya msimu huu hakuna timu ya maana itakayomuhitaji kwa bei nzuri.
 
kwako wewe ishu ni uingereza au uwezo wake, angalau ungelitumia hoja ya umri wake na majeruhi ingeleta mantiki kwa harry kane. dunia pia ina uhaba wa washambuliaji, chelsea wanatamani kumuondoa lukaku ila what next.
Tatizo mwingereza akija timu kama yetu kizazi hiki media zao zinamkuza kuliko uhalisia kusababisha tusipate tulichokitarajia kutoka kwake, at least tubalance.
 
Umesoma vizuri?

Nimemkataza kufunga?

Nachosema za way alivyo ni vigumu kupata timu ambayo wachezaji wapo for team kuliko wao binafsi.

Ikiwa kila mtu anataka apate sifa how about our club?

Individual brilliance vs teamwork ipi poa?
Nipe ushahidi unaoonesha kwamba cr7 anacheza kwa ajili ya tunzo binafsi, lkn hata kama anacheza kwa ajili hiyo huoni kama anatupa faida kutokana na ku fight kwake? Acheni kukariri hakuna mchezaji asiyependa tunzo binafsi.
 
Man u haieleweki mwaka wa kumi huu usijisahaulishe.
Sababu mojawapo ni

Kununua mastaa wenye ego, from di maria, falcao, to Pogba, Ronaldo, Sancho unategemea nini?.

TIMU INAYOWEZA KUFANYA POA NI ILE AMBAYO INATENGENEZA MASTAA NA SIO INAYONUNU MASTAA.

Simple as that


Ila Mkuu why unahisi namchukia Ronaldo?
Huoni nikiwaongelea Maguire, Rashford, Glazers, pundits ambao ni janga la MAN U.

Okay ngoja niweke wazi msimamo.

Pale United nashabikia timu inaitwa Manchester United. Nataka iwe na ushindani, iwe na mataji, legacy of theater of dreams iendelee.

Haijalishi ni mchezaji gani, akisaidia ushindi i have to appreciate, but MAN U FIRST.
 
Nipe ushahidi unaoonesha kwamba cr7 anacheza kwa ajili ya tunzo binafsi, lkn hata kama anacheza kwa ajili hiyo huoni kama anatupa faida kutokana na ku fight kwake? Acheni kukariri hakuna mchezaji asiyependa tunzo binafsi.
Duh! Okay boss yaishe please naona hunielewi kabisa.
 
hapa me naona pogba anamaana nyengine hasa hii picha ya mkono kama wakuaga
Screenshot_20220416-205333_Twitter.jpg
 
Back
Top Bottom