hakuna chanzo chochote cha habari za uhakika kilichoripoti taarifa za CR7 kutohitajiwa na kocha ajaye, kwa kuwa hii habari imetokea upande wa ten hag nilitegemea vyanzo viwili vya habari zinazohusu uholanzi hususan klabu ya AJAX wangelitupa tetesi hii lakini mpaka muda huu wapo kimya, kwa taarifa za uhakika zinazohusu ajax na ten hag chanzo kikuu aminifu ni MIKE VERWEIJ na hata jana katika interview ya ten hag akizungumzia maandalizi ya fainali itakayochezwa hapo kesho huyu jamaa alikuwa anamchokonoa sana ten hag kwa maswali yake yanayohusu zaidi tetesi za man utd kuliko maandalizi ya ajax kuelekea fainali. Kwa asiyefahamu huyu bwana ndiye mtu wa mwanzoni kuja na taarifa zinazohusu ten hag kuwa mstari wa mbele kutakiwa na man utd na hata ishu ya ten hag kufanyiwa mahojiano na man utd ndio chanzo cha mapema kuripoti kwa waandishi wasioripoti habari za man utd, vyanzo vyengine muhimu kwa taarifa za man utd ni james ducker wa telegraph, laurie whitwell wa the athletic , david ornstein wa the athletic na simon stone wa bbc (huyu pia anaripoti habari za man city). Kati ya hao ni yupi alieripoti taarifa ya ronaldo kutohitajiwa na ten hag?... Basi hata hawa akina mark ogden wa espn,mwanadada charlotte ducker wa goal.com nao hawana ubuyu huu walionao daily...... pekee wakitiwa nguvu na sky sports?