Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

kwako wewe ishu ni uingereza au uwezo wake, angalau ungelitumia hoja ya umri wake na majeruhi ingeleta mantiki kwa harry kane. dunia pia ina uhaba wa washambuliaji, chelsea wanatamani kumuondoa lukaku ila what next.
Hiyo gharama ya kumleta Kane bora tutafute kwingine au tubaki na CR7.

Ni kichaa pekee atakaetoa £150M kwa mchezaji wa kingereza. Kwa hiyo hela tunaweza leta wachezaji wazuri hata wanne.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
namuona akivuliwa kinga ya unahodha na baada ya hapo atagombania namba. kwa performance yake ya msimu huu hakuna timu ya maana itakayomuhitaji kwa bei nzuri.
Huyu bozo anatugharimu sana. Hafai hata kugombea namba.

ETH itambidi angalau apunguze wachezaji 6 wenye mikataba ukiondoa wale 6 wanaomaliza mikataba yao (Pogba, Cavani, Lingard, Chong, Mata).

Tunahitaji kupunguza wachezaji wasiopungua 12 mpaka mwezi wa 6. Tuna kundi kubwa sana la wachezaji ila wengi ni hovyo sana.
 
Kheri tule hasara ila tujenge timu yenye ushindani angalau ndani ya misimu miwili ijayo.

Wachezaji kama Martial, Rashford, Bissaka, Maguire, Fred tutajichelewesha zaidi tukiendelea kubaki nao.

Nemanja Matic kawa muungwana kaamua kujitoa mwenyewe ningependa kuona wengine wakiungana nae.
 
baada ya kufunga hatrick yake ya 50, CR7 alimzawadia mpira alejandro garnacho.
img_1_1650132370827.jpg
 
Sababu mojawapo ni

Kununua mastaa wenye ego, from di maria, falcao, to Pogba, Ronaldo, Sancho unategemea nini?.

TIMU INAYOWEZA KUFANYA POA NI ILE AMBAYO INATENGENEZA MASTAA NA SIO INAYONUNU MASTAA.

Simple as that


Ila Mkuu why unahisi namchukia Ronaldo?
Huoni nikiwaongelea Maguire, Rashford, Glazers, pundits ambao ni janga la MAN U.

Okay ngoja niweke wazi msimamo.

Pale United nashabikia timu inaitwa Manchester United. Nataka iwe na ushindani, iwe na mataji, legacy of theater of dreams iendelee.

Haijalishi ni mchezaji gani, akisaidia ushindi i have to appreciate, but MAN U FIRST.
We jamaa hata hueleweki,
 
Back
Top Bottom