Flano
JF-Expert Member
- Aug 7, 2019
- 5,842
- 16,292
Mimi binafsi nnashangaa hizi chuki zote kwa Ronaldo zinatokea wapi?Ronaldo hawezi kuanzia bench. Yani mpaka Ronaldo anasaini mkataba bila shaka moja ya vitu wamezingatia ni yeye kupata muda wa kutosha kucheza hata mshahara wake ni wa mtu anayetakiwa kucheza.
Mimi naamini Ronaldo kuwa chini ya kiwango inachangiwa na wachezaji wanaomzunguka. Ronaldo huyuhuyu ukimpeleka City utatamani awe kwenye timu yako. Manchester United matokeo yake mengi yanaamuliwa na individual brilliance na siyo kama team rejea mechi za UCL mpaka tulipofika ni kwasababu ya Ronaldo.
Kama Manchester United ingekuwa inacheza jinsi a proper football club should play usingeona madhaifu ya Ronaldo au kusingekuwa kabisa na huu mjadala. Kucheza kama team ni pamoja na kufukia makosa ya mwenzio na hicho kitu tunakikosa. Club kama Leeds au Brentford zina average players wengi lakini wanacheza kwa umoja.
Changamoto iliyopo sasa ni kwa wachezaji wote kwenye timu ukimuondoa kipa.
Anachopitia Ronaldo hakina tofauti na alichokua anapitia Messi kwenye timu ya taifa mpaka akataka kutundika daruga.
Hatuko imara kwenye beki, viungo wala washambuliaji.
Upandae wa kocha nae mpaka leo hii haijulikani anatumia mfumo gani.
Nnasisitiza tena hawa wageni wetu RR na CR wazidi kupewa muda.
Kingine Ronaldo usuper star wake usimfanye akajiona yeye ni mkubwa kuliko timu kwa hilo hatutamvumilia, pamoja na usuper star wake nidhamu yake ndio itaongeza mapenzi kwa mashabiki, ila akituletea dharau zake atajuta kutufahamu mashabiki wa United.
