Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Hatuna timu wakuu..

Very inconsistent players..non -aggressive..

Stamina sifuri kabisa..

De Gea tu ndo anajua anafanya nini uwanjani.

Mishahara mikubwa ndo kitu tunachoweza..
Tukampigie magoti sosha
 
Kwani na ARV umesha tumia?
 
Ngoja wanao zidi kumtetea kocha na kutupilia lawama Kwa wachezaji kwamba wote wauzwe kocha achukue wachezaji anao wahitaji.Hawajiulizi Mourinho aliwezaje kuchukua Europa league maana kikosi ni kilekile hata kama ni mabadiliko ni machache Sana.

Kuna mtu kasema Rafl nafasi yake ni utendaji na ushauri kuliko ukocha naona Yuko sahihi maana anaongea theories nzuri saana kuliko action.

Mourinho aheshimiwe.Yeye aliwezaje akiwa na kina Rashiford wanao tupiliwa lawama kipindi hiki.

Kwanini Ralf ???Ingali kikosi ni kizuri na mwanzo wa msimu kilitegemewa kutoa challenge kwenye title lakini Sasa holaa.
 
Man U ni kigenge cha Wahuni tu,huo ndio ukweli,povu ruksa
na magwaya angecheza hiyo mechi,lawama zingekuwa Kwa magwaya kwamba kwanini kashindwa kuzuia magolii wakati yeye ni beki wa MWISHO.Mashabiki wa man u bwana
.

Gusia useme tatizo ni kocha uone,wao wanataka kocha apewe wachezaji wake hawa waliopo hawajui kitu wakati hao walinyanyua kombe la yuropa Ligi kipindi Cha Mourinho
.Na kufika fainali yuropa Ligi kipindi Cha Sosha.
 
sehemu sahihi ya ralf ni ushauri, tumekuwa na rekodi mbovu sana ya kufanya maamuzi ya ovyo hivyo tunamuhitaji zaidi kwa kazi hiyo. murtough na fletcher kuwategemea peke yao ni kujidanganya.
Ralf awe mshauri kabisa maana anaongea vitu vizuri munoo afu asajiriwe kocha ambaye atageuza ushauri wa Ralf kuwa kwenye action.
 
Hilo siyo kweli
United ilihusishwa kusajili wachezaji hawa.
1. Robert Lewandoski
2. Ikay Gundogan
3. Eden Hazard
4. Fabinho
5. Thiago Alcantara
6.Thomas Mounier
7. Jude Bellingham
8. Sven Botman
10. Mathias De light
Na wengine wengi ambao vipaji vyao vinaonekana wazi katika vilabu vingine.

Ukiangalia kwenye academy yetu pale EPL United ndiyo inawachezaji wenye vipaji vikubwa zaidi kuliko vilabu vingine wanapatikanaje ?

Suala linalokwamisha ni katika maamuzi ya mwisho nani asajiliwe.

Yawezekana labda wachezaji wetu wanasumbuliwa na mambo mengi ya nje ya uwanja ndiyo maana hawafanyi vizuri
 
Kitu cha kwanza anachotakiwa kufanya kocha ni kuipandisha morali ya timu watu wacheze huku wana hamu na ushindi.

Ole alishindwa hilo.

Ralf pia anashindwa hilo. Wiki nyuma zilikuja ripoti za wachezaji kujigawa leo tunaona Ralf kaanzisha bifu na Martial na hana miezi minne klabuni.

Huyu Ralf ataua timu uwanjani na kichwani. fuentte huyu ni kocha wa kugewa maamuzi 100%?
 
Naomba kujulishwa kama yule mtaalamu aliyeletwa kwa sababu ya kufundisha mipira iliyokufa kama bado anafanya kazi united au aliondoka pamoja na Ole?
United tumecheza kona 100 mpaka mechi ya jana lakini hawajafunga goli hata moja kupitia kona hizo licha ya uwepo wa wachezaji zaidi ya sita wenye historia ya kufunga magoli mengi kwenye mipira ya kona.
 
Man United inahitaji a pragmatic coach na siyo football philosopher.
 
nyie

Sent from my PBBM00 using JamiiForums mobile app
 
ni kwa sababu haamini kwenye unafiki na uchawa, ukifuatilia interview zake amejitanabahisha kuwa ni mtu asiyependa kujibu maswali kwa kujizungusha kama kocha aliyepita. tabia yake ina faida na hasara zake. mfano leo aulizwe swali juu ya utendaji kazi wa familia ya glazer ukilinganisha na familia sheikh mansour bila ya shaka atawaponda familia ya glazer haliyakuwa ndio waliomuajiri. kwa misimamo yake sidhani kama ataweza kumaliza miaka miwili ya ushauri ikiwa hatosikilizwa. ralf na bielsa ni ndugu wawili wasiojuana
 
Mou akikuletea misimamo yake unamvumilia kwa kuangalia rekodi yake. Kwa Ralf unaangalia nini kitakachofanya umvumilie?

Mou aliondoka kwa kusemwa anaigawa dressing room, United mlihitaji kocha kama Gasperini kama ishu ni unafiki. Haendi kulalamika kwenye media anakufuata kukukaripia unapokosea na anachotarajia ukifanye ukijifanye jeuri anakubonda.

Morali haipandi kwa kutangaza ishu kwenye media. Mchezaji na kocha hua wanaongea wenyewe huko ndani wakitoka tunajua hawa ni wamoja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…