Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Nimemshangaa sana jamaa anahoji kwa team ipi eti
 
RANGNICK KUMBAKIZA CAVANI


MKUU wa benchi la ufundi la Manchester United, Ralf Rangnick, amesema anataka kuona straika mkongwe, Edinson Cavani, akimaliza msimu huu akiwa klabuni hapo.

Cavani (34), amekuwa akihusihwa na mpango wa kuondoka Old Trafford kupitia usajili wa dirisha dogo la Januari, mwakani.

Licha ya kuanza vizuri katika siku za mwanzoni mwa kibarua chake Old Trafford, Cavani alijikuta akipoteza nafasi ya kucheza, hasa baada ya usajili wa Cristiano Ronaldo.

Barcelona imekuwa mstari wa mbele kuifukuzia saini ya Cavani lakini Rangnick haoneshi kuwa anataka kumwachia nyota huyo.
 
Man U wana vyuma sana kwenye academy, wanaotusumbua ni watoto wa Cobham tu kule chelsea ila ndani ya miaka 3 tutakuwa nao
 
Atawauwa huyu jamaaa hahaha sipati picha huko mazoezini kama wako JKT.
sure, ila ninapata wasiwasi jamaa ni mkali sana, sababu kawaka sana kwamba kipindi cha pili na young boys "they didn't follow his instruction", imepelekea VBK kaomba msamaha kwa kuchomesha timu.

patamu ni pale watakapofuata instructions na bado wafungwe.
 
Ndo inatakiwa wapo nyoronyoro sana lazima wachangamshwe kidogo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…