Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Sawa ni kocha mzuri, alivyorudi kwa mara ya pili alikwama wapi?
 
Kwa sasa United ina wachezaji ambao wakipata kocha mzuri timu itasonga mbele ,ukileta kocha ambae ni yes man (like OGS) hiyo rebuild itachukua hata miaka 20.Wachezaji wengi viwango vyao vimebaki pale pale sababu kocha anayewafundisha hakuwa na ubavu wa kuwaeleza ukweli (Shaw,Bissaka,Maguire,Martial,Pogba,Rashford,McTominay ) wanahitaji kocha wa kuwa-push

Lampard alikuwa anatumia mfumo tofauti na Tuchel kaja na mfumo tofauti lakini progress inaonekana
 
Ole Gunnar Solskjaer anatarajiwa kuiongoza tena manchester united siku ya Jumamosi dhidi ya tottenham hotspurs.
mambo anayopaswa kuyapigania ni pamoja na:
  1. kurudisha umoja ndani ya timu
  2. kuondoa ubaguzi au upendeleo kwa baadhi ya wachezaji
  3. mbinu za kiuchezaji
 
ila wakati chelsea wanatafuta kocha waliangalia wachezaji wao na kutafuta nani ana connection nzuri zaid, Tuchel amemfundisha silva, Rudigger german connection, havertz na werner wajerumani. toka wanatafuta kocha tetesi tayari walikuwa wanataka kocha ambaye atanusuru investment zao, hivyo ilibidi kocha awe angalau anajua kijerumani
source halisi hapa ila ni paid article

nagelsmann alikuwa pia kwenye Shortlist ila sababu Bayern walikuwa na mazungumzo nae hakuja.
 
Aisee hii timu hii,team rebuild imekuwa ni kazi Sana kwetu,kujenga timu ni kazi sanaaa huwa ndo Mana kila siku nawapongeza Sana Bayern Munich wale jamaa wanajua wanachokifanya Tena ni kwa miaka mingi Sana...
Pep aliiharibu Buyern ndio majuzi tu imerudi kwenye ile style yake.
 
Mkuuu nimekuambia uwe unaangalia Ronaldo akicheza kwa jicho la tatu.. Ronaldo ni mzigo kwenye team.. tena mzigo mkubwa.. kama jana amefanya nn cha maana... Ronaldo games zake n za Norwich City.. Newcastle City.. Burnley.. etc
Afanye cha maana kwani anacheza peke yake uwanjani.Timu nzima imelemewa wewe unamwona ronaldo tu.Man hakua na muinganiko wowote ndo maana hakuna move ya maana waliyoifanya sasa huyo ronaldo ataonekanaje.
 

So now sababu ni lugha na sio mfumo wa kocha ?

Conte alichukua ubingwa Inter na wachezaji walionekana magalasa hapa United (Young,Darmian,Sanchez,Lukaku) Perisic

Roman yupo aggresive anachoangalia ni perfomance kama usipo-deliver anakufukuza regardleas atakulipa kiasi gani
 
Conte pia amespend sana Inter mpaka club ina deni kubwa sana.

Kwa miaka 5 iliopita Conte anashika nafasi ya 3 duniani kwa Spendings kubwa Nyuma ya Pep Na velverde. Amespend Takriban Euro 677 million, Roughly Euro milioni 120 kila msimu, hivyo si kweli kwamba anatumia Magarasa. Amesajili watu Kama Lukaku, Achraf Hakimi, Barella, Eriksen, Vidal, Godin etc wote hawa wapo regarded kama mastaa.

Na Abramovich pia amejitahidi sana kuleta mpira unaovutia Chelsea ila kila kocha wa ushambuliaji anazingua Chelsea kuanzia kina Scolari miaka hio mpaka sarri na Lampard, makocha walioipa Ubingwa Chelsea Uefa ni Di Matteo na Tuchel, ligi wenye Mafanikio ni Mou na Conte, wote hawa ni watu wanaoprioritize defense kwanza kabla ya ushambuliaji, na Ndio DNA ya Chelsea miaka na Miaka ukabaji ndio eneo ambalo Chelsea wanajivuania Kuanzia Makelele Hadi Kante.

Hivyo Mkuu DNA ni muhimu ni vyema kuangalia Strength zetu zipo wapi na aje Mtu kutokana na uwezo wetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…