Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Nafikiri academy nyingi haziwekezi nguvu nyingi kuzalisha natural strikers badala yake zinazalisha Attacking players hasa ujio wa tiktack ya Barcelona na Spain ulionyesha wazi kuwa unaweza kupata ushindi bila striker na kuanzia hapo Strikers wazuri hawapatikani tena Central and Western Europe.

Hata ukiangalia kwenye vilabu vingi unakuta attackers wengi siyo natural strikers ila ni wingers, au attacking midfielders wenye uwezo wa kufunga tu.

Liverpool amepata ubingwa bila natural striker.

Man city msimu huu kafanya hivyo hivyo ukiondoa mechi chache za Gabriel Jesus.
 
upo sahihi na hiyo mifano yako ulioaiambatanisha, lakini kwetu sisi ni tofauti kwa sababu tumeshamsikia ole akizungumza juu ya suala la DNA.

ninavyofahamu Ole anapoizungumzia DNA huilenga zaidi ile iliojengwa na sir alex kwa miaka 20 ya mafanikio yake ambayo iliongozwa na mshambuliaji wa asili kwa takribani misimu yote, hivyo basi sidhani kama tutacopy mifumo mengineo ilioasisiwa na baadhi ya makocha kama hao uliowataja licha ya kwamba inaweza kutupa mafanikio
 
OFFICIAL: Will Fish has joined Stockport County on a season-long loan from Manchester United.

nadhani hii ni sababu nyengine kubwa inayochangia zaidi wachezaji wetu kutokuuzika kwa sababu ya kuwaandalia mazingira yasio ridhisha ya kumvutia mteja wa nje. Tupunguze hii tabia ya kuwapeleka kwa mkopo wachezaji kwenye ligi za chini na tunapaswa kuliangalia zaidi soko la nje ya nchi kama tunakhofu ya wachezaji wetu kutokuweza kupata nafasi kwenye vilabu vya daraja la premier.

nchi mfano wa germany, spain, italy, uholanzi na hata ureno wana ligi nzuri na zenye ushindani zitakazoweza kuwajenga wachezaji wetu kimbinu na uzoefu endapo watapambana.

ethan laird, teden mengi na wachezaji wengineo wenye future nzuri wanapaswa wapelekwe huko na si kuwapeleka portsmouth, derby, QPR n.k
 
Hiyo Stockport County iko daraja la ngapi ?
 
Uyo dogo kuna watu wanamchukulia poa kwakuwa ni mweusi.
adui wa amad ni daniel james na si rangi yake, kuondoka kwa james itakuwa ni faida kubwa kwa amad kwa sababu atapata dakika nyingi za kucheza, kinyume na hapo namuona akitolewa kwa mkopo msimu huu azidi kuwa mkakamavu

brighton wameshaonyesha nia ya kumuhitaji daniel james ila tatizo ni maafikiano ya bei
 
James a.k.a mkimbia hovyo.
 
Shida huwa inakuja utd inapotaka kusajili basi inatajiwa dau nono lkn ikitaka kuuza watu wanaweka ofa mbuzi, nawachora sn huu upuuzi.
matokeo yetu mabovu kwa takribani miaka 8 ukijumlisha na uongozi mbovu unaosimamia timu ndio chanzo cha yote hayo, takribani timu zote hutumia udhaifu huo kwani huamini pindi tunapokuwa sokoni iwe ni kwa kuuza au kununua huongozwa zaidi na hali ya uhitaji wa huduma uliokithiri
  1. tunataka kupigwa kwenye dili la varane kwa sababu ya uhitaji wetu mkubwa wa beki wa kati, madrid wanajifanya kuzigomea euro millioni 45 kwa mchezaji aliyebakiza mwaka mmoja
  2. baadae tutafanyiwa uhuni kwenye dili la kiungo
  3. tukiuza sisi kwa sababu ya kupunguza kundi la wachezaji tusiowahitaji vilabu husika watakuja na ofa mbovu (wakitaka watatupa lingard au perreira, wasipotaka wataendelea kuwalipa mishahara ya gharama)
 
Timu ya kifala sana ,sasa sancho anamaajabu gani ?

Game tu ya kwanza na Leeds united mtakula kipigo cha mbwa koko kudadekiiiiii
 
Shida huwa inakuja utd inapotaka kusajili basi inatajiwa dau nono lkn ikitaka kuuza watu wanaweka ofa mbuzi, nawachora sn huu upuuzi.
United huwa hainunui wachezaji kwa bei halisi huwa tunapigwa.

Linapokuja suala la wachezaji wetu kuhitajika tunaona kama wameweka mpunga kidogo kitu ambacho siyo kweli.

Bei halisi ya Pogba wa sasa ni ngapi ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…