Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Kwa ninavyoona mimi Pogba moyo wake haupo kwetu kwa sasa na kama atabaki ni tutakuwa tumempa tu ofa nzuri sana.

Natamani Pogba auzwe tusuke kiungo kitakachokuwa na balance nzuri..Pogba+Fernandes haijaworkout kusema ukweli.

Tunaweza kupata kiungo mwenye uwiano nzuri wa kukaba na kushambulia..na hapa ndo tutakapopata balance nzuri.
 
Ila akiondoka bila kusajili replacement tutakuwa hovyo sana japokuwa Donny yupo ila kwa majeraha aliyonayo sidhani kama atakuwa fit kucheza
wiki tano hizi zilizobakia tutasikia tetesi nyingi sana zinazohusu wachezaji wanaocheza eneo la kiungo na ishu kubwa sana si tu thamani ya mchezaji husika tutakayohitaji kulipa bali ni ku-analyse ubora wake na madhaifu yake,

nje ya mustakabali wa paul pogba tayari tulishaweka mipango ya kusajili kiungo wa kuongezea nguvu atakayevuka ubora wa mcfred na scouts wamefika hadi afrika kutafuta mchezaji husika hii ina maana ya kwamba klabu ipo serious na sasa imeongezeka ishu ya pogba japokuwa taarifa rasmi za kutosaini mkataba mpya hazijazungumzwa na waandishi wenye nguvu
 
Pamoja na kwamba haijathibitika kama hatakuwa sehemu ya kikosi cha united msimu ujao bado napendelea Paulo Pogba aondoshwe kikosini ili tutengeneze timu isiyomtegemea. Kwa kipindi cha miaka 5 aliyokaa united hajaweza kufikia kilele cha ubora wake ambao wengi tulitegemea kuuona bali vipindi vya ubora kidogo na kucheza chini ya kiwango muda mrefu.
Yamesemwa mengi kwanini haufikii ubora wake akiwa na united ikiwa ni pamoja na uhafifu wa wachezaji wanaomzunguka (bruno alifanya vema akiwa na kundi hilo hilo la wachezaji),hapangwi nafasi sahihi uwanjani (kacheza namba 6,8,wing wa kushoto pamoja na 10). Pia mfumo umehusishwa ( tumecheza mifumo karibia yote kumtosheleza huyu bwana lakini hakuwahi kunivutia kama mchezaji mahiri). Mechi ninayoikumbuka kuuona ubora wa PP ni msimu juzi dhidi ya city round ya 2 tukifanya comeback kuja kushinda 2-3.

United imewahi kucheza kipindi kirefu cha msimu wa 2019/2020 bila uwepo wa pogba (alikuwa majeruhi) na timu ilikuwa ikifanya vizuri sana ingawa yeye ndio alikuwa anachukuliwa akama mchezaji bora wa kikosi chetu. Timu kama city,chelsea,liverpool zimefanya vizuri bila uwepo wa pogba. Tutafute mbadala wa pogba,kocha aweke ufundi wake tunyanyue kwapa 2022.

Pogba hana uwiano mzuri kwenye kushambulia na kurudi kukaba hasa anapocheza kwenye kiungo cha chini yeye huwa anakuwa weak link kwa timu pinzani kutokana na ugoigoi wake. Ni wakati wa Ole kutengeneza timu bila uwepo wa pogba kwa kusajili mtu anayeweza kufanya majukumu yake kikamilifu uwanjani.
Kwa mtizamo wangu,sikuwahi kumkubali pogba kama mchezaji mahiri wa united bali alibeba na ajenda za kibiashara na mtoto wa nyumbani kuliko thamani ya kiwango chake kiuchezaji kilichomleta united tokea juventus.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…