Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Sijapenda hii abadilike sasa na ni kazi ya management kumbadilisha huyu
IMG-20210601-WA0045.jpg
 
★OFFICIAL: The nominees for the 2020/21 Premier League Player of the season:

https://www.premierleague.com/news/2160555★

#GGMU

manutd |
IMG_20210602_001736_913.jpeg
 
  1. yaonekana Rashford si majeruhi na kucheza kwake chini ya kiwango hakuhusiani kabisa na afya yake, kama rashford anasumbuliwa na injury kwa miaka miwili kwa nini ameshindwa kuchukua hatua ya kujiondoa timu ya taifa?
England boss Southgate on Rashford's fitness: "Marcus we haven't seen on the grass but I've spoken with him and he assures me he's happy with where he's at so we go from there with that one"
 
Hivi tatizo letu la winger wa uhakika wa kulia litamalizika msimu huu au ndiyo hivyo tuendelee kuwa na matumaini na Amad Diallo ?
Amad Diallo hana uwezo wa kuingia kwenye kikosi cha kwanza msimu ujao na sababu kubwa ni kukosa kwake muda wa kucheza jambo lillilochangiwa zaidi na mwalimu kushindwa kumpa nafasi.
Pia yaonekana Ole hajaridhishwa na makuaji yake ya kisoka ndio maana huenda aliingiwa na ugumu wa kumpa nafasi (aliendelea kumuamini zaidi mason greenwood).

Usajili wa Amad ni kamari la mazingaombwe kwani uamuzi wa kulipata jawabu sahihi upo chini ya macho yako, nikiwa na maana usajili wake utakuwa ni bora sana na wenye unafuu ikiwa benchi la ufundi litaweza kumtengeza Amad na kuwa mchezaji hatari kama kilivyo kipaji chake, kinyume chake usajili wake utatuachia maumivu makubwa sana endapo tutashindwa kumtengeneza na kuwa mchezaji muhimu kikosini. Tukumbuke usajili wake tulikurukupa siku ya mwishoni na kulipa paundi millioni 30 kwa mchezaji anayecheza reserve team ya Atlanta (kabla ya hapo Atlanta walitaka kumtoa kwa mkopo pale pale Italy ili apate dakika za kucheza)

usajili wa Amad unafanana na usajili wa cristiano ronaldo au bebe, sir alex alilipa paundi millioni 15 kwa ronaldo, kiasi ambacho timu nyingi zilizomuona mwanzoni ikiwemo Arsenal zilishindwa kulipa ada hiyo kwa kuhofia makuaji yake ya kisoka kuwa na udhaifu (hakuwa na nafasi ya kudumu huko sporting), mwishowe sir alex akacheza kamari na hatimaye akaibuka mshindi wa kihistoria.

Sir alex huyo huyo alilipa paundi millioni 7 kwa mchezaji wa mchangani anayeitwa Bebe, si sir alex wala scouts aliyewahi kumshuhudia bebe akicheza soka la ushindani ila imani yake dhidi ya mtu fulani(nadhani alikuwa ni carlos quiroz) ndio ilimfanya akubali kulipa kitita cha paundi millioni 7, hatimaye historia imeendelea kumtaja bebe kama mchezaji wa ovyo kusajiliwa na mwanadamu mwenye uzoefu wa soka la ushindani.

si Amad, daniel james, mata wala greenwood atakayezuia usajili wa winga mwenye ubora zaidi ya hao tulionao,kutokufanya hivyo tutakuwa tunajichimbia shimo wenyewe na hatimaye kurejea hadithi hizo kwa hizo.
======================

Mechi ya juzi laiti kama tungelikuwa na winga mzuri wa kulia (si greenwood), full back hodari wa kulia (si wan bissaka) na kiungo hodari zaidi anayecheza upande wa kulia (si scott) tulikuwa na uwezo wa kuwamaliza villareal ndani ya dakika 90. Ole aliwadhibiti vizuri sana villareal kiasi ambacho walikuwa hawawezi kujenga mashambulizi kwa kuanzia upande wao wa kushoto (wan bissaka alikuwa anakaba juu, scott anaziba nafasi ya wan bissaka, greenwood anatembea na parejo, bailly anamlazimisha bacca asogee kulia).

changamoto kubwa ilijitokeza baada ya kuwapokonya mpira ndani ya half yao sisi tulishindwa kubypass ukuta wao(upande wetu wa kushoto ulidhibitiwa, shaw alimuogopa sana moreno akawa haingii ndani, bruno alishindwa kutembea kwa sababu defence line ya villareal haikuruhusu space dhidi yake na upande wetu wa kulia kama kawaida yake only mason ndiye mwenye uwezo wa kutembea na kubreaks down shape ya villareal)

si ajabu ile mechi ndio manaa shots on target zilikuwa ni chache kwa sababu makocha wote hawakuwa na plan B baada ya kila mmoja kumdhibiti mwenzake kwa plan yake aliyoiandaa.

tuachane na hilo mimi mpaka leo sielewi ni kipi kilichotuzuia
  • kuwafunga west bromwich kwa takribani dakika 50 baada ya kuwarudishia goli uwanjani kwao
  • kuwarudishia goli sheffield zikiwa zimebaki takribani dakika 30
  • kushindwa kupata dawa ya kuwadhibiti leicester city ndani ya msimu huu, kwenye mechi zetu 3 wamepata alama 7 na pia walicheza vizuri zaidi ndani ya uwanja kuliko sisi
  • kushindwa kupata dawa ya kuwafunga crystal palace mechi zote mbili
  • kushindwa kupata dawa ya kucheza vizuri dhidi ya liverpool haliyakuwa msimu huu walikuwa ovyo
  • kuendelea kusumbuliwa na wolves kiuchezaji bila ya kujali matokeo tunayoyapata

labda mwalimu wetu anaonekana ana udhaifu wa kiusimamizi pindi mkakati wake unaposhindwa kuzaa matunda, au labda huenda sababu ni kukosa kwake wachezaji sahihi watakaomuwezesha kubadili plan huku mechi ikiwa inaendelea. Naamini yote hayo tutayafahamu msimu ujao ambao utakuwa ni mwaka wake wa tatu na wa mwisho ndani ya mkataba wake.

sitomuelewa kabisa kama atakuja na hadithi za tupo kwenye progress nzuri za kurudisha ubora wetu uliozoeleka huku matokeo yetu yakiwa ni mabaya
 
  1. yaonekana Rashford si majeruhi na kucheza kwake chini ya kiwango hakuhusiani kabisa na afya yake, kama rashford anasumbuliwa na injury kwa miaka miwili kwa nini ameshindwa kuchukua hatua ya kujiondoa timu ya taifa?
England boss Southgate on Rashford's fitness: "Marcus we haven't seen on the grass but I've spoken with him and he assures me he's happy with where he's at so we go from there with that one"
Bwana Rashford uwezo wake umeishia hapa hawezi kuwa hatari zaidi ya hapa maana ameridhika
 
Back
Top Bottom