Forgotten
JF-Expert Member
- Jul 20, 2018
- 3,630
- 11,096
Bruno na Martial walishangilia goli la pili kwa kukumbatiana wakiwa nje ya uwanja (ilikuwa the best scene kwangu) ushindi ukisindikizwa na kimvua.Scott alifunga goli zuri sana dhidi ya city mwaka jana assist ya Ederson Moraes bonge la goli hii mech ilikuwa tamu sana kipindi bruno ndio mpyaaaa
Kumfunga City ni raha sana kwasababu huwa tunakuwa underrated sana dhidi yao ila katika misimu hii miwili City kaambulia point moja tu, pia mashabiki wake ni wachache ila wanakera jinsi wanavyoongea maneno ya shombo huku timu yao ikiwa haipo hata robo ya mafanikio ya United.
Liverpool ndiyo wapinzani halisi wa United, msimu huu niliombea kama timu yangu isipobeba ubingwa wa EPL basi abebe City ila siyo Liverpool. Mbungi ya North West Derby inakutana miamba ya soka la Uingereza, Manchester Derby inakuwa na ukubwa kwasababu za ubora wa City wa sasa ila North West Derby hata Liverpool awe mbovu vipi anaweza asitoe points 3 kwa United.
"★
