Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Nadhani sasa mmeona rashford na martial wameanza kutengenezewa mazingira ya kupigania namba, the rebuilding takes the progress, tutakuja kuwa tishio baadae.
 
Kumuuza Diogo Dalot na kuanza kumuwania Max Arons kunaweka doa kwenye benchi la ufundi. Hakuna tofauti na kuuza Lukaku kisha kuanza kuhangaika na akina Ighalo na Cavani.
 

Yupo kwenye timu ya level yake ww ndio umeshindwa kutambua hana cha kupoteza kule wala pressure
 
Kwa mwenendo huu wa Rashford pamoja na mwenzake Martial,nadhani ni wakati muafaka wa kuirudisha mezani hoja ya uwezo sahihi wa hao madogo wawili kama kweli wanaweza kutubeba msimu ujao au tunaendelea kucheza kamari na kumuachia Pep atuadhilishe atakavyo.

Ningependa kuona madhaifu ya mwalimu yanafichwa na ubora wa wachezaji wake kama alivyofanya Zidane na Madrid yake kabla CR7 hajawa historia pale bernabeu,lakini mapenzi ya Ole kwa hawa vijana ndio yatamfukuzisha pale OT.
 
Mkuu tupe muono wako kwenye kikosi kilicho na pogba pamoja na bruno (haijalishi nafasi wanazocheza) tunapocheza big game hasa kwenye uwiano wa kiulinzi.
 

Na striker kwa mfumo wa sosha panahitajika striker pia scott ni mzur shida yake anakaa sana na mipira anataka kumiliki katikati wakat hana uwezo huo fred si mzur kwenye pasi hata kwa scott hivyo hivyo ndio maana timu inahangaika sana ila kwenye kukaba wapo vizur timu inahitaj wapiga pasi za chap kama carick na scholes walivyokuwa
 
sijaangalia takwimu zinazoangazia mechi alizocheza juan mata kwa hii miaka minne iliopita ila sidhani kama anafikisha mechi 50 alizocheza za ligi kuu. Nafikiri uwepo wa juan mata klabuni unatokanwa zaidi na sababu za kiuongozi kuliko sababu za kiuchezaji. Juan mata anaonekana kuwa ni mwanadamu mwenye taswira ya upole, uvumilivu, aliyeridhika, mpinga fitna(hajawahi kuanzisha mgogoro wowote dhidi ya mwalimu), mwingi wa ihsan na ikhlaq nafsini mwake.

Naweza kusema huu ni msimu wa nne kumshuhudia Juan akikosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza lakini sijawahi kukutana na malalamiko yeyote kutoka kwake kupitia media tofauti ukilinganisha na wachezaji wengineo wenye changamoto inayoshabihiana na ya kwake kwa kuanzia utawala wa mourinho ambaye tuliamini havutiwi na uchezaji wa mata (rejea sakata lake pale chelsea) mpaka huu utawala wa Ole gunnar. Si hivyo tu pia juan amekuwa akichezeshwa nafasi asiyoipendelea kiuchezaji tokea asajiliwe manchester united lakini ameendelea kujitolea kwa moyo wake wote pindi anapopewa nafasi

Nafikiri Ole anamtumia juan mata kama ni mfano kwa wachezaji vijana na hata wale wapya walioshindwa kuingia kwenye mfumo wawe wavumilivu licha ya kukosa dakika nyingi za kucheza, hakuna umuhimu wa kuwatumia mawakala kuleta vitisho vya mikataba na wala hakuna umuhimu wa kuongelea mambo ya klabu kwenye media.

Sitoshangaa endapo juan mata atapewa tena mkataba iwe wa mwaka mmoja au miwili (najua atakubali), nafikiri klabu ina mpango wa kumtumia juan mata siku za mbeleni kuwa ni balozi wa klabu ndio maana wanazidi kumweka karibu.

si hivyo tu pia nimeona vugu vugu kubwa la usajili wa wachezaji vijana kutoka Spain kwa miaka hii ya karibuni kama vile:
  • alvaro fernandez: mlinzi wa kushoto kutoka real madrid na amepandishwa timu ya miaka 23 licha ya kuwa na miaka 17.
  • marc jurado: anatokea barcelona, amezaliwa miaka 16 iliopita
  • armau puigmal: anacheza timu ya miaka 23
  • Mateo Mejia
  • alejandro ganacho: miaka 16 na amesajiliwa kutoka atletico madrid
uwepo wa mata utaweza kuwa ni kichocheo cha kuendeleza huu mkakati wa kusajili vijana kutoka spain, vijana watamchukulia juan kama ni mlezi wao pale Manchester kutokana na uzoefu wake na haiba yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…