Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Cavani na Scot ni majeruhi hivyo hawatacheza kesho.

Tuna mechi ngumu sana kesho hasa ukizingatia record ya chelsea recently.

Kikubwa tujitahidi kutumia nafasi chache tutakazozipata lakini tuombe Matic na Fred wawe form kidogo kuwalinda mapazia yetu kule nyuma.

I would opt for 3 centre backs lakini wing ya kulia tumtumie Daniel James kumzuia Marco's Alonso asipande sana.

Kushoto I would opt for Telles halafu Shaw aje aunde 3 centre backs.

Katikati Fred and Matic ni lazima watakuwepo kwa sababu wengine wote ni majeruhi.

Left wing acheze Rashford ili Reece James asipande sana na Kovacic awe busy kuweka cover shadow badala ya kudictate game.
 
Mechi ya kesho inauwezekano mkubwa sana wa kutoa sare.
 
Ole vs PSG 4 games 2 Wins.
Ole vs Man City 8 games 3 wins 3 defeats 1 draw.

Ole vs Liverpool 5 games 2 defeats 2 draws 1 win

Ole vs Chelsea 5 games 1 defeat 3 Win one draw.

Total wins 9
Defeats 8
Draws 4.

Takwimu zake against big games siyo mbaya kama unachotaka kuonyesha.

Msimu huu alone ndiyo hana record nzuri against big teams lakini nazo kafungwa mara moja tu na Man city kwenye kombe la EFL
 
Hizi ndiyo mechi tulizopotezea mwelekeo.

Timu yetu ikifanya vizuri mechi mbili wachezaji wanarelax tunapoteza wanaanza upya tena.

Last season nilisema tunapoteza mechi kwa sababu ya laissez faire attitude ya mwalimu.
 
Kipindi season inaanza Mimi sikuwa na matarajio ya Man U kupambania ubingwa.

ManU alipokuwa kileleni kwa tofauti ya Pointi 3. Bado sikuwaza United inaweza kuchukua ubingwa.

Nilitegemea Man City au Liverpool mmoja akae juu ya msimamo Kisha Man U iwe second.
Ila Sasa kitu kinachouzi ni unawezaje kupoteza point tano dhidi ya timu zinashika mkia(Shelfield + West Brom)
Ingekuwa ni mechi moja tungesema ni a bad day in the office
Kweli unafungwa na timu ambayo katika mechi 20, imeshinda mechi 1, tena kwa goli la penalty.
Kwa kiasi kikubwa defence ndio imetuangusha, haiwezekani tufungwe goli 32.
Hata timu iliyonafasi ya kumi huko imefungwa idadi ndogo kuliko sisi.
 
Majeruhi hayamwangushi peke yake, mpaka mimi shabiki wake yana niathiri.

Pata picha angekua yuko fiti msimu mzima, akina Maguar & Lindelof wangekua wanagombea nambamba tu.
Uko kwao Ivory coast wanamloga na ukizingatia na uracist wa Ole ndo kabisa kiwango kinaporomoka.
 
kujadili mwenendo wa manchester united ni sawa kurejea kitabu ulichokwisha kisoma zaidi ya mara moja.
ari na hamasa kwangu imeondoka, ni bora niwe msomaji zaidi
Hili timu ni litakataka mkuu wala lisikupe presha za kijinga ..leo hili jitu litakufa..
#CFC
 
Ukiyakuta ma fan boys ya manure yanavyochambua timu lao
Sasa utadhani ni bonge la timu ..kumbe ni matapishi matupu..
Sasa angalieni tunavyowaonesha leo kuwa hii timu ni matapishi tu
#CFC
 
Tetesi zipo hivi;

United walikataa kuweka kipengele cha kumuuza Lingard kwenye mkataba wake wa mkopo ambayo ilikuwa ni kwa £15M kwa makusudi akipata form yake wapige cha juu, kwa sasa Lingard thamani yake ni £20M.

Inasemekana United wanataka kumshusha Declan Rice mwenye thamani isiyopungua £50M na ikiwezekana kufanya swap deal na West Ham United kukamilisha usajili huo. Wakimuacha Lingard West Ham na kuna uwezekano akaongezwa Matic na Jones kwenye dili hilo.

Anthony Martial huenda huu ukawa msimu wake wa mwisho akiwa United, ni wazi akiuzwa United watakamilisha dili la Sancho kwa ada ya uhamisho isiyopungua £50M wala kuzidi £80M.

United pia wanataka kununua CB kutoka Sevilla, Jules Kounde. Pia RB kutoka Norwich City, Max Aarons mwenye thamani ya £35M anafukuziwa na United pamoja na Everton na Bayern Munich.

Msimu huu tunaweza kutoka hivi:

Buy
RICE - DM
SANCHO - RW
KOUNDE - CB
AARONS - RB

Sell
LINGARD
MATA
POGBA
MATIC
JONES

Siioni United ikimuuza Fred ambaye yupo on form na muhimu katika maslahi ya kikosi kipana cha United, zaidi naona Pogba akiondoka na kuachia nafasi kwa watu kama VDB. Kuondoka kwa Pogba hakutaathiri sana kikosi chetu kama tukikamilisha usajili wa DM.
Tukimpata Kounde na Aarons itakuwa tumefanya sajili muhimu sana katika eneo la ulinzi, Kounde siyo mwenye kimo kirefu wala kasi kubwa sana ila ni moja ya mabeki wa kati hatari.
Aarons ni one of the best attacking RB, huyu jamaa ataleta challenge kwa Bissaka. Jamaa anajua kupandisha mashumbulizi vizuri na kumwaga maji vizuri bila kusahau defending skills nzuri.

Mpaka hapo tukiongezea na Sancho tutakuwa tumemaliza kazi, Siioni United ikinunua striker kwa sasa kutokana mahitaji yetu muhimu. Cavani akiongeza mkataba tutakuwa vizuri bila Martial huku tukiwa na options za Rashford na Sancho kwenye wings pamoja na Greenwood kama ST nikiamini msimu ujao utakuwa wa kuanza kuitetea namba hiyo endapo Martial atauzwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…