Manchester United (Red Devils) | Special Thread

New ferguson in epl
 
kwa hili jibu lako kwa mujibu wa swali alilouliza jamaa pale maana yake tuendelee kujaribu tena mpaka apatikane aliyesahihi??
Nimejaribu tu kumuuliza swali hilo..lakini Nagelsman akija United kwa sasa haiwezi kuwa sawa na Ole aliyetoka cardiff..Leipzig walikuwa semi-finalist wa Uefa msimu uliopita na pia at times wamecheza soka fulani safi huku bajeti ikiwa chini sana.
 
Naangalia Westham vs Shiffield United.
LINGARD kaongeza kitu sana pale Westham
 
Nimejaribu tu kumuuliza swali hilo..lakini Nagelsman akija United kwa sasa haiwezi kuwa sawa na Ole aliyetoka cardiff..Leipzig walikuwa semi-finalist wa Uefa msimu uliopita na pia at times wamecheza soka fulani safi huku bajeti ikiwa chini sana.
Jombaa, Julian Nagelsmann yule ni mtu mwenye akili nyingi sana za kiufundi. Ana silaha kubwa sana tunayoikosa kitu ambacho makocha kama Pep Guardiola na Jurgen Klopp wanacho, GAME MANAGEMENT SKILLS.

Umuhimu wa game management skills Everton wasingeweza kupata sare wakati tunaongoza goli mbili bila siku ile. Tusingefungwa na PSG kabla ya Fred kupewa kadi. Ukiangalia vizuri safu yetu ya ufundi ni kama wanabahatisha bahatisha hawajui nini cha kufanya muda mchezo unapoendelea.

Kusema ukweli kama tutaendelea kuamini Ole atakuja kuwa kocha mzuri tunapoteza muda. Kwa sasa ni heri amalize msimu tupate nafasi ya top 4 msimu mpya aje mwalimu mpya pamoja na mkurugenzi wa ufundi.
 
Hivi bado kuna fans kwenye haya majukwaa wanaendekeza matusi? Nyie si ndio mnajiita watu wazima mmeanza kushabikia mpira toka 90? Naanza kupata mashaka na ushabiki wenu naamini kwa wingi mnaweza kuwadhibiti hawa watoto amvao naamini kwa asilimia 100 bado hawajawa na familia.
 
Mkuu umeongea vema sana. Na mfano mwingine ni Foden pale Man city,wakiwa wameshinda hata goli 3-4 na dogo akatoa assist au naye akatupia kambani maongezi yote kwa foden wakati Gundogan ndio anawaweka mjini kwa sasa.
Inakera sana yani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…