Mtu yoyote anayesema Ole hana mbinu simuelewi kabisa kusema kweli.
Hivi kocha asie na mbinu anaweza kumpiga Pep na makocha wengine top 6 kirahisi vile? Kila tukicheza na timu kubwa anapanga formation za ajabu ajabu mara 4-3-1-2 mara 3-5-2 mara diamond na formation nyengine, kwa asilimia kubwa tunawakamata na tunawafunga kirahisi mapema kabisa tunamaliza mechi.
Tulidrop round ya kwanza msimu uliopita sababu ya majeruhi ila round ya pili tulishinda mfululizo tulipokuwa na kikosi kamili, si wakubwa si wadogo tukafika hadi nafasi ya 3.
Msimu huu Ole amefanya kazi nzuri kuongeza Depth kwa Vdb, Cavani na Telles, wanatupa option zisizokuwepo msimu uliopita, wakati kama Huu shaw kaumia ndio tulikuwa tuna William panga pangua.
Leo hii ole amefanya Sub kipindi cha pili kilivyoanza tu hamna anaempa credit ila ni individual brilliance tu za wachezaji?