So sad Manchester United sio timu ya uwanjani tena mkuu, sasa hivi ni business na mastermind wa hii michongo ni Ed.
Ed hataki kutoa hiyo hela kwa Telles kwasababu anajua miezi michache mbele anaweza kumpata Telles tena bure so kinachofanyika ni kuwapiga Porto chenga ya mwili wao watakomaa na 18 ila United wao wanawavuta ili kuwatoa mchezoni, kwakuwa hakuna upinzani mkubwa Ed anajitahidi awavute Porto mpaka dk za mwisho wakikosa mteja lazima watakubali maana Porto hatakubali abaki na mchezaji ambaye anaweza asikubali kuongeza mkataba na akaondoka bure mkataba wake wa mwanzo ukiisha. Na ikifikia siku ya mwisho hajauzwa inaweza kuwa win kwa Ed kama mchezaji ana interest na Man. Utd means atakuja bure mwisho wa siku na hapo ndipo Glazers wanapozidisha mahaba kwa Ed.
Na kuhusu Sancho pia naamini ni michezo ya kibiashara ya Ed mpaka sasa naamini Sancho anaweza kuja United na atakuja akiwa ametengenezewa popularity kubwa sana na official announcement ikitoka ita-trend sana na kupelekea mashabiki wengi kuzama mfukoni kununua matambara yao kuwafaidisha Adidas ili wazidi kumwaga mpunga wa sponsorship United.
Sasa ili Adidas wafurahi zaidi ndiyo mtu kama Solskjær anaingia hapa kwakuwa hamsumbui kichwa Ed kazi yake ni kuhakikisha anapata tiketi ya UEFA tu, kama unavyojua kila tukienda UEFA Adidas kuna asilimia anatoa.
Kitu kikubwa ni mapato na plan za mapato ndiyo hizi zinazofanyika, United wakitaka kurudi kwenye ubora wao ni madirisha mawili tu ila ni mpaka Glazers wauze ile timu.