Greenwood sio winga na wala hajawahi kuwa Winga, hapa mna compare wachezaji wawili tofauti. Quality za Greenwood zote ni za finisher,
1. Greenwood average pass ni 16 kwa mechi
2. Greenwood average dribble ni 0.7
3. Greenwood average key pass ni 0.5
Hizo ni quality muhimu za kiungo wa pembeni Ajue kumchukua mtu na kumtoka, Ajue kutengeneza Magoli, ajue kupiga pasi etc zote Greenwood hana.
Greenwood ni striker, mwanzo mwisho ndio maana qualities zake ni za kiufungaji zaidi, Anashoot kulia na kushoto, mashuti yake ni ya Chini, anajua kufinya na Kufunga etc.
Man United kunahitajika Mtu wa maana kulia Anaejua kufunga, kutoa pasi za magoli na kutupa dimension nyengine ili tusitabirike.