Kikosi cha ku-compete na kutupa matokeo kipo ila ili upate mafanikio zaidi katika msimu wa soka unahitaji kuwa na squad depth na consistency. Kitu ambacho United hamna.
Ukimtoa Martial hakuna Striker mwingine tunayemtegemea kuipa timu ushindi.
Pogba now ana Corona, Bruno ataanza kwa kasi ila kutokana na mashindano mengi atahitaji msaada. Hakuna option nyingine kufikia viwango vya Bruno kwenye kiungo zaidi ya Pogba ambaye hatujui atapona lini.
James ni squad player, Greenwood ameonyesha uwezo mkubwa katika nafasi ya winga lakini kwa umri wake sidhani kama ana uwezo wa kutoboa msimu mzima katika kiwango kilekile. Ukizingatia sasa hivi ameitwa timu ya taifa.
Rashford ndio huyo leo atakufurahisha kesho atakukera, no consistency btn games and games.
Manchester United ina timu nzuri ila ya kupambania ubingwa wa ligi bado tunahitaji watu zaidi.