Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Man Utd kwa sasa wana kikosi bora kabisa, tatizo ni mwalimu na mbinu zake za uchezaji. Man Utd iliyokuwa inafungwa na Sevila ni ile mbovu iliyokuwa imejaa wazee walioflop, kwa uwekezaji uliofanyika haya ni matokeo mabovu.
Mbinu gani unataka aweke tena,, au unataka aje na mbinu ya kupaki basi
 
Kwanini asiwe Dries Mertens au Raul Jimenez?
 
Wachezaji waliopo wanamuangusha kocha thats why tumpe kocha anaowataka..

Mfano mdogo tu..Midfield imetengeneza zaidi ya nafasi 30 kwny mechi mbili zilizopita lakini tumefunga magoli mawili TENA YA PENALTY !!! Huoni pale mbele kuna ujinga mwingi!?

Tumoe kocha sancho na Striker alaf uone kwny nafasi 30 zitakazotengenezwa watafunga magoli mangapi
 
Watakwambia tuliupiga mwingi..tumpe kocha muda


Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
 
Kumbuka huyo mtangulizi wake(morinyo) alitupa
.Fa
.Europa
.Community shield.

Lakini akaondoka kabla hata hajapewa wachezaji ANAOWATAKA..

Morinyo hakumtaka LINDERLOF wala FRED ila WOODWARD alimkazia..

Hii timu inajiua yenyewe..
 
Yah kwenye suala la captain na suggest tumpe Bruno anaonesha ni kiongozi mzuri uwanjani, alafu kuna hawa watoto huwa nasema kila siku tusitegemee makubwa kutoka kwao (Martial & Rashford) hawa co wa kuwategemea kabisa hawako perfect yn inapaswa wawe wanatokea sub, ofcz wakiwa watu wa kuingia itakuwa poa, yn pale utd kuna utitiri wa average players wanaokula pesa za bure tu.
 
PTER,
Kwanini asiwe Dries Mertens au Raul Jimenez?

Nimemchagua Edin Dzeko kwa sababu namuona kama ni mshambuliaji mzoefu aliye sawa kwa sasa na anaweza kupatikana. Pia Edin ni mshindi, ni mchezaji anayeweza kucheza mahala penye pressure na panapohitaji makombe.

Edin, pia anaweza kuwa mwalimu wa hawa wapuuzi wawili (Marcus Rashford & Anthony Martial). Sioni kama tunaweza kuwa-offload tumejifunga nao kimikataba, so the best way forward ni kuwa-train tu wawe wazuri japokuwa so far sina imani nao tena tumewapa nafasi ila wametuangusha wana ujinga mwingi sana.

Hofu yangu kubwa sana watamfundisha hata Mason Greenwood kuwa mchezaji average kama wao. Kijana bado ana umri mdogo (18) anajifunza kutoka kwa wakubwa wake, kama una wakubwa wapumbavu ni kheri umtafute mkubwa mwenye akili ili aje kuwa role model kwa kijana huku akitusaidia ku-buy time muda tunatafuta mbadala wa kueleweka.
 

Kuna baadhi ya Wachezaji kocha asipopewa huwezi kuifanya ni excuse kuwa kocha hakupewa wachezaji anaowataka.

Mfano Ole asipopewa Sancho huwezi kulaumu hata kidogo! Sancho £108m sio jambo la kusema tu ukapewa! Wako wachezaji ambao ni affordable ambao ni very talented let's say wa £50M hapo unawezasema kocha hakupewa wachezaji anaowataka.

Lakini kocha hawezi kusema niletee, Neymar, Sancho, Salah, VVD na Coitinho, asipoletewa ukalalamika kuwa hakupewa wachezaji anaowataka hapo utakuwa hujui nini mpira.
 
Aiseeeeee Nimecheka Sana daaaaaaah ila niliwaambia humu siku za nyuma Anthony Martial sio mchezaji wa kucheza man utd hata kidogo angalia strikers waliopita RVP, rooney, tevez berbatov then mlinganishe na uyo dogo ovyo kabisa
 
Nmekuelewa sn mkuu, pia ss nafurahi kuona man u wenzangu mmeanza kuniunga mkono kwa hawa watoto wawili I have been singing about these overrated players now everyone can see.
 

Pia kwa kuanza kupewa Maguire, Bisaka na Bruno si hatua ndogo kwa kuanzia ingawa Watu wanabeza hilo, Klopp alianza na Mane tu, Akaja akaongezwa tena mmoja ambaye ni Salah, baadae akapewa tena mmoja VVD, mwisho ndiyo akapewa Keita, Kipa na Fabinho. Usidhani wachezaji wote alipewa kwa kipindi kimoja! Hiyo ilimchukuwa miaka 4 kupewa hao ambapo hajui atapewa tena lini Mchezaji mwengine.
 
The best 007,

Just imagine vilaza kama hawa wawili (Marcus Rashford & Anthony Martial) tunawalipa zaidi ya $200k/weekly. Je tunaweza ku-accommodate kipaji kingine cha kueleweka bila kudai mshahara mkubwa?

Kuna vitu vingi sana behind the scenes vinafanya timu kubwa kama Manchester kujaza wachezaji wasio na sifa za kucheza timu yetu, mojawapo ni timu kushindwa kuwa na wachezaji wengi wazuri kwa wakati mmoja tayari watu wanatuona kama sisi prime target ya kupigwa pesa sio mishahara wala bei za kununulia. Wanajua timu inaongozwa na mtu mwenye uwezo mdogo ni rahisi kumpiga pesa hasa hasa akipewa pressure na mashabiki.

Amini hii kauli yangu, Jadon Sancho tutamsajili ila tutapigwa pesa. Borussia wana-delay hili dili wanajua fika wana-negotiate na mtu average kichwani wanasubiri muda sahihi tu to rip him off, same tactics tulizofanyiwa kwa Harry Maguire . Na tutamlipa mshahara zaidi ya $250k/weekly.
 
Hii kitu huwa inaninyima sn raha unajua Sancho km angekuwa anatakiwa na Bayern au Barca pesa icngekuwa juu ya 80 ukizngatia na corona hii, hii dunia ya soka nmekuja kugundua tm mbili tu huwa znapigwa sn pesa nazo ni man u na Madrid.
 
OGS alikuwa na hiyo nafasi akaona Ighalo kutoka China anamfaa akamsajili kwa mkopo then permanent

Sent from my Redmi 8A using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…