M ANCHESTER United imepanga kumpa bonge la dili winga wao Daniel James kisha itamtoa kwa mkopo msimu ujao.
Winga huyo wa kimataifa wa Wales, 22, amecheza mechi 37 msimu huu na kiwango chake kinaweza kuwasukuma Man United kumpa dili la pesa ndefu.
Lakini, watafungua milango ya kutoka kwa mkopo kama Man United itamilisha dili za kuleta mastaa iliyopanga kuwasajili kwenye dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi.
Miamba hiyo ya Old Trafford inapambana kusaka huduma ya winga wa Borussia Dortmund, Jadon Sancho, kiungo wa Aston Villa, Jack Grealish na kiungo wa Bayer Leverkusen, Kai Havertz.
Mastaa hao wote wakija, James atakuwa kwenye wakati mgumu wa kupata namba, hivyo atatolewa kwa mkopo akakomae zaidi. Man United walinasa huduma ya James kutoka Swansea City mwaka jana kwa ada ya Pauni 15 milioni.
Amefunga mabao manne katika mechi 37 alizocheza chini ya Ole Gunnar Solskjaer msimu huu, huku akitarajia kufanya kweli wakati watakapokipiga na Tottenham, ligi itakaporejea Juni 19.
Lakini, Solskjaer moyo wake upo kwenye kumnasa winga wa Dortmund, Mwingereza Sancho, ambaye amekuwa moto kwelikweli msimu huu huko Bundesliga, akifunga mabao 17 na kuasisti mara 17 msimu huu.
Hata hivyo, saini yake itamgharimu Ole kiasi kisichopungua Pauni 100 milioni.
Sent using
Jamii Forums mobile app