Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

It seems Van Gaal anaumia sana hakufukuzwa Man united kiasi amelialia kwa miaka yote hiyo.

Ni vyema akatulia sasa akalea wajukuu huku kulialia hakutabadilisha uhalisia kuwa Alifaili pale united.

Ole at the wheel
Van Gaal was the perfect coach to replace SAF.

Alitakiwa atengeneze filosofia ya Man Utd upya.

Ed Woodward ndo kirisi pale.
 
Van Gaal was the perfect coach to replace SAF.

Alitakiwa atengeneze filosofia ya Man Utd upya.

Ed Woodward ndo kirisi pale.
Nakubaliana na wewe juzi nilikuwa naangalia marudio ya FA mech zake mbili za mwisho everton ns crystal palace mpira ulikuwa unachezwa mzur sana vipi kama angepata watu aliokuwa akiwataka? Alitumia wachezaj wengi wadogo toka kwenye academy
 
Unaweza kutuambia Van Gaal alimtaka nani akamkosa kisha akaletewa Dimaria ?
kipindi kile tetesi nyingi zilimuhusisha arjen robben akiwa na miaka yake 31, pengine hoja ya umri ndio ilileta ugumu kwa united kutumia rasilimali fedha kufanikisha dili hilo ndio maana waliamua kuelekeza nguvu kwa angel di maria aliyekuwa na miaka 27.

pengine louis aliamini mfumo wake wa 3-5-2 unamuhitaji zaidi arjen robben kuliko chaguo jengine.
alileta wachezaji 13 na kati ya hao ni wachezaji watatu ndio wameendelea kuwepo kwenye kikosi
 
Tetesi katika club ya man united ni nyingi sana na ni ngumu sana kusema hii ni ya kweli na hii si ya kweli mpaka unapoona mchezaji kanunuliwa.

Kipindi cha Ferguson kuna wachezaji wengi sana aliwataka bahati mbaya hakuwapata na mara nyingi amekuwa akiweka wazi kuwa alimhitaji mchezaji huyu lakini sikumpata nikampata yule mathalani issue ya Eden Hazard na Lucas Moura, Ferguson aliamua kumnunua Shinji Kagawa.

Club pia pamoja na kwamba kocha anahitaji wachezaji fulani lakini lazima yawe mahitaji realistic na yenye maslahi kwa Club, Bayern isingemwachia Thomas Muller na Arjen Roben kwa urahisi namna ile huku Roben akiwa na miaka 31.

Mimi nachokiona wazi alichokosea Van Gaal alifanya squad overhaul unreasonable usingeweza kuuza wachezaji wengi vile halafu ukategemea maingizo mapya yakupatie kikosi cha ushindani, mbaya zaidi wachezaji wengi alionunua walitoka nje ya epl hivyo walihitaji muda kuzoea ligi.

Ni kweli kwamba uongozi wa man united kwenye suala la transfer una mapungufu yake lakini Van Gaal alipewa support kubwa sana kulinganisha na makocha wengine.

Kuendelea kulialia hakutaondoa uhalisia kuwa alishindwa kuitransform man united kama alivyotaka.
 
Back
Top Bottom