Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Kama hawawekwi wazi sisi tunapata wapi uhakika kuwa Van Gaal alikuwa hawahitaji aliletewa tu ?
Moyes huyo hapo chini nae




David Moyes took over Manchester United in the summer of 2013 after Alex Ferguson called it a career as the manager of the club. It went awry from the start with many of Moyes' targets in that transfer window moving elsewhere. He told BeInSports just how close he came to signing the likes of Kroos, Bale and Fabregas for United.
That summer, they ended up with Marouane Fellaini and Moyes says he was just one of many players they wanted to sign and concedes the Belgian wasn't his first target.
"We thought we had a chance of getting Gareth Bale," he said. "We hoped we could talk Bale out of going to Real Madrid because it was already, kind of, half done. We offered more money, we tried to entice him."
Moyes was asked by Richard Keyes is they had a helicopter and says they did. United were trying to swoop for the Welsh attacker but lost out in the end.
"Cesc Fabregas was very close" too and Moyes says "I spoke to him and I hoped to bring him from Barcelona" but says every manager has situations like that and "hard luck stories" without wanting to focus on the close calls.
"I had met Toni Kroos, during the season, and agreed he would come to Man United before he went to Real Madrid but somewhere in there I lost my job and it meant that Toni went elsewhere," he said.
 
Moyes huyo hapo chini nae




David Moyes took over Manchester United in the summer of 2013 after Alex Ferguson called it a career as the manager of the club. It went awry from the start with many of Moyes' targets in that transfer window moving elsewhere. He told BeInSports just how close he came to signing the likes of Kroos, Bale and Fabregas for United.
That summer, they ended up with Marouane Fellaini and Moyes says he was just one of many players they wanted to sign and concedes the Belgian wasn't his first target.
"We thought we had a chance of getting Gareth Bale," he said. "We hoped we could talk Bale out of going to Real Madrid because it was already, kind of, half done. We offered more money, we tried to entice him."
Moyes was asked by Richard Keyes is they had a helicopter and says they did. United were trying to swoop for the Welsh attacker but lost out in the end.
"Cesc Fabregas was very close" too and Moyes says "I spoke to him and I hoped to bring him from Barcelona" but says every manager has situations like that and "hard luck stories" without wanting to focus on the close calls.
"I had met Toni Kroos, during the season, and agreed he would come to Man United before he went to Real Madrid but somewhere in there I lost my job and it meant that Toni went elsewhere," he said.
Kwa Moyes naweza kubali kuwa hakupewa mahitaji yake sawa sawa kwa sababu hatukufanya transfer sawa sawa.

Ila nadhani pia alirithi kikosi kikubwa sana ambacho hatuhitaji Rocket Science kujua kuwa kikosi kile ungempa Mourinho angepata ubingwa tena.

Kilichomnyima kufanya vizuri Moyes ni kwamba hakujua what it takes to be a manchester united manager.

Hata kama ungekuwa wewe ni Woodward aje kocha katika kikosi ambacho kimetoka kutwaa ubingwa kila kitu akwambie nahitaji kumsajili Gareth Bale Cesc Fabregas lazima uwe reluctant kufanya squad rebuild unarebuild nini ?
 
MANCHESTER UNITED WALIVYOTENGENEZA BONGE LA TIMU KWENYE TETESI.


TANGU Sir Alex Ferguson alipoondoka Manchester United mwaka 2013 na timu hiyo kupita chini ya makocha kibao kuanzia David Moyes, Louis van Gaal, Jose Mourinho na sasa Ole Gunnar Solskjaer kumekuwa na kundi kubwa la wachezaji wamekuwa wakihusishwa na timu hiyo.
Wapo wale walifanikiwa kunaswa na miamba hiyo ya Old Trafford, lakini wapo wengine ambao wamekuwa wakiishia tu kwenye tetesi kwamba wanasakwa na Man United.
Wakati dirisha la majira ya kiangazi la uhamisho wa wachezaji kwa mwaka huu likikaribia kuanza, hiki kama kikosi cha mastaa wanaotengeneza kikosi cha tetesi cha wale wanaosakwa na Man United, ambapo timu hii itatumia mfumo wa 4-2-3-1. Hii timu ingenaswa, basi wapinzani wangejuta kujifahamu.



Jan Oblak, kipa
Klabu: Atletico Madrid
Makisio ada: Pauni 80milioni
Kwa muda mrefu sana, Manchester United imekuwa ikikuna kichwa ni kipa gani atakuja kuchukua mikoba ya David De Gea atakapoamua kuondoka kwenye kikosi hicho. Hata kabla ya kuondoka, lakini Man United wanataka kipa mwingine atakayekuja kumpa De Gea upinzani mkali kwenye kugombea namba baada ya kuona Sergio Romero kushindwa kufanya hivyo. Kutokana na hilo, kwa muda mrefu wamekuwa wakihusishwa na mpango wa kumsajili kipa wa Atletico Madrid, Jan Oblak, ambaye bila ya shaka saini yake itawagharimu mkwanja usiopungua Pauni 80 milioni. Oblak akienda Man United basi kutakuwa na vita kubwa ya namba, la kama De Dea atafungua mlango wa kuondoka.



Dayot Upamecano, beki wa kulia
Klabu: RB Leipzig
Makisio ada: Pauni 50milioni
Kiasili, Dayot Upamecano ni beki wa kati, lakini ana uwezo pia wa kucheza beki wa kulia na hilo ndilo linalomfanya kupata nafasi kwenye kikosi hiki cha mastaa wanaovumishwa kutakiwa na Manchester United. Huduma yake anayotoa msimu huu huko kwenye kikosi cha RB Leipzig imezifanya timu nyingi kutaka saini yake ikiwamo Arsenal, Manchester City na Real Madrid, lakini Man United ni miongoni mwa vigogo hao wanaohitaji huduma ya staa huyo. Ripoti za karibuni zilidai kwamba beki huyo amepanga kusaini dili jipya la kuendelea kukipiga kwenye kikosi cha Leipzig, licha ya taarifa nyingine kudai kwamba itawekwa mezani pesa ya maana, basi suala la kunasa saini ya Dayot haitakuwa mjadala.



Ben Chilwell, beki wa kushoto
Klabu: Leicester City
Makisio ada: Pauni 50milioni
Huduma ya beki wa kushoto, Ben Chilwell imekuwa ikisakwa na timu nyingi kwenye Ligi Kuu England, ikiwamo mahasimu wawili wa Manchester, Manchester United na Manchester City. Timu hizo mbili ndizo mara kadhaa zimetajwa kusaka saini ya beki huyo wa Leicester City, ambaye anadaiwa kwamba saini yake inaweza kugharimu mkwanja usiopungua Pauni 50 milioni. Chelsea nao walitajwa kutaka saini yake kwa wakati fulani, lakini ukweli ni kwamba katika kupambana kuimarisha beki ya kushoto kwenda kuwapa changamoto ya namba wachezaji Luke Shaw na Brandon Williams. Chilwell ni moja ya mabeki wa kushoto wachache kabisa walionyesha ubora mkubwa kwenye Ligi Kuu England msimu huu na Man United inamtaka ikiamini kwamba atakwenda kuimarisha ukuta wao kwenye upande huo, wakati ule wa kulia atasimama Aaron Wan-Bissaka.



Milan Skriniar, beki wa kati
Klabu: Inter Mila
Makisio ada: Pauni 85milioni
Tangu Manchester United ilipokuwa chini ya kocha Jose Mourinho amekuwa ikihusishwa na mpango wa kumsajili beki wa kati, Milan Skriniar. Huduma ya beki huyo imekuwa ikiwatoa udenda Man United kwa muda mrefu na sasa msimu huu wamerudi tena kwenye mchakamchaka wa kuhitaji saini ya beki huyo. Man United wanataka kutumia uhusiano wao mzuri na kocha Antonio Conte, ambaye walimuuzia mshambuliaji Romelu Lukaku na kuwapa kwa mkopo mshambuliaji Alexis Sanchez kwenye dili la kunasa saini ya beki huyo wa kati akatengeneze pacha matata kabisa na Harry Maguire kwenye kikosi hicho cha Old Trafford kupiga mzigo. Skriniar ni staa mwingine kwenye tetesi za Man United.



Kalidou Koulibaly, beki wa kati
Klabu: Napoli
Makisio ada: Pauni 72milioni
Amehusishwa sana na mpango wa kujiunga na Manchester United. Saini ya beki huyo wa kati Msenegali imekuwa ikiwasumbua Man United kwa muda mrefu tangu walipokuwa chini ya Jose Mourinho. Kocha, Ole Gunnar Solskjaer alipotua kwenye kikosi hicho mwaka jana alifanya usajili wa beki Harry Maguire, hivyo anahitaji pacha wake wa kuja kucheza na beki huyo Mwingereza kwenye safu yake ya ulinzi. Lakini, Napoli walikuwa wakiweka ngumu kwa maana ya kung’ang’ania kumuuza Koulibaly kwa mkwanja usiopungua Pauni 100milioni, lakini kutokana na janga la corona miamba hiyo ya Italia imekubali kushusha bei na pengine saini yake inaweza kupatikana kwa mkwanja usiozidi Pauni 72 milioni.



Miralem Pjanic, kiungo wa kati
Klabu: Juventus
Makisio ada: Pauni 70milioni
Ripoti za karibuni ni kwamba Manchester United imekuwa ikihusishwa na mpango wa kumsajili kiungo wa kati wa Juventus, Miralem Pjanic katika dili linaloweza kumhusisha kiungo Paul Pogba. Thamani ya mchezaji huyo inatajwa kuwa ni Pauni 70 milioni na kama atatua kwenye kikosi hicho cha Old Trafford, basi kwenye timu hii ya mastaa wanaovumishwa kutakuwa na Man United, atacheza kwenye sehemu ya kiungo sambamba na Saul Niguez. Kulikuwa na ripoti nyingine zinazomhusisha mchezaji huyo na Barcelona, kwamba kuna dili jingine la kubadilishana wachezaji linaweza kufanyika baisna ya klabu hizo. Lakini, Man United imeripotiwa kwamba ipo tayari kumchukua Pjanic hata kama kwa pesa ili kwenda kuimarisha sehemu ya katikati ya uwanja katika kikosi hicho na kufanya kuwapo kwa ushindani wa namba kwenye safu ya kiungo.



Saul Niguez, kiungo wa kati
Klabu: Atletico Madrid
Makisio ada: Pauni 70milioni
Saul kwa ripoti mpya za sasa ni kwamba kiungo huyo ameripotiwa kukaribia kabisa kujiunga na Manchester United kwa ada isiyozidi Pauni 70 milioni. Kinachoelezwa ni kwamba klabu yake ya Atletico Madrid imeshafikia makubaliano na Man United na kinachosubiriwa ni dirisha la uhamisho tu wa wachezaji lifunguliwe mambo yakamilishwe. Kocha Ole Gunnar Solskjear amekuwa akidaiwa kuhitaji saini ya mchezaji huyo na kinachoripotiwa ni kwamba kocha Diego Simeone ametoa baraka zake kwa staa huyo wa Kihispaniola kwenda kupiga kazi huko Old Trafford. Kama hilo litafanyika itakuwa vyema, lakini Saul ni staa mwingine wa kwenye tetesi, ambaye amekuwa akihusishwa na Man United hasa mwaka huu kwamba saini yake imebakiza mambo machache tu kunasa na Mashetani Wekundu wa Manchester akakipige kwenye Ligi Kuu England.



Jadon Sancho, kiungo wa kulia
Klabu: Borussia Dortmund
Makisio ada: Pauni 100milioni
Kwa muda mrefu sana, Jadon Sancho amekuwa akiripotiwa kuwa kwenye rada za Manchester United na huku ikielezwa kwamba mchezaji huyo ni chaguo kubwa la kocha Ole Gunnar Solskjaer akihitaji saini yake katika dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi. Hata hivyo, Real Madrid nao wanahitaji saini yake, huku mtihani pekee unaowakabili Man United ili kufanikisha kunasa saini ya Sancho basi ni kuhakikisha kwanza wanafuzu kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya. Dortmund wao wanaamini mchezaji wao hatahama kwenye dirisha hili la majira ya kiangazi, lakini kama kutawekwa mezani mkwanja wa maana basi biashara inaweza kufanyika. Huduma ya Sancho inaweza kuwagharimu Pauni 100 milioni hasa katika kipindi hiki cha janga la virusi vya corona ambalo limeziathiri timu kwa kiasi kikubwa sana kiuchumi.



Jack Grealish, kiungo wa kushoto
Klabu: Aston Villa
Makisio ada: Pauni 80milioni
Aston Villa imesisitiza kwamba haitashusha bei ya staa wao, Jack Grealish hata kama watashuka daraja na kucheza Championship msimu ujao. Kwa muda mrefu ndani ya msimu huu, Manchester United wamekuwa wakihusishwa na mpango wa kumsajili Mwingereza huyo mwenye uwezo wa kucheza kiungo ya kushoto na kama atakuja katika chama hilo la Old Trafford, basi kocha Ole Gunnar Solskjaer atampanga kwenye upande huo. Hata hivyo, huduma yake inaweza kuwagharimu Man United, Pauni 80 milioni, licha ya kuamini kwamba Aston Villa wakishuka daraja na ukichanganya na janga la corona basi wanaamini wanaweza kumnasa Grealish kwa mkwanja usiozidi Pauni 72 milioni. Kuna wakati Grealish alihusishwa pia na klabu ya Real Madrid.



Pierre-Emerick Aubameyang, mshambuliaji
Klabu: Arsenal
Makisio ada: Pauni 60milioni
Kuna mengi yanayosemwa kuhusu straika Pierre-Emerick Aubameyang na uwezekano wa kuiga nyayo za staa wa zamani wa The Gunners, Robin van Persie kuhusu kwenda kujiunga na Manchester United. Aubameyang ni moja ya wachezaji wanataka kwenda kujiunga na timu itakayompa nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya. Siku za karibuni, amekuwa akihusishwa na Real Madrid na Barcelona, lakini mpango wa kwenda huko hauonekani kama utakamilika huku Man United ikipewa nafasi kubwa kama na yenyewe itakamatia tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao. Arsenal wao wanaweza kulazimika kumuuza kwenye dirisha lijalo kwa ajili ya hofu ya kumpoteza bure mwakani kutokana na mkataba wake kutarajia kufika mwisho na hana mpango wa kusaini dili jipya.



Harry Kane, mshambuliaji
Klabu: Tottenham
Makisio ada: Pauni 100milioni
Staa wa Tottenham, Kane ni moja ya wachezaji ambao majina yao hayakauki kwenye tetesi za kuhusishwa na Manchester United. Tangu dirisha la majira ya kiangazi la mwaka jana, fowadi huyo amekuwa akihusishwa na Man United hasa baada ya kumpiga bei Romelu Lukaku. Katika kuelekea dirisha lijalo, Man United wameripotiwa kuhitaji mshambuliaji mwingine mpya, hivyo wanaweza kutua kwa Kane hasa baada ya kuelezwa kwamba Spurs watakuwa tayari kufanya biashara. Straika huyo anaweza kuwagharimu Man United mkwanja kiasi cha Pauni 100 milioni hasa katika kipindi hiki cha mtikisiko wa uchumi kutokana na janga la virusi vya corona huku bei yake ya awali ilitajwa kuwa ni Pauni 200 milioni.



Wachezaji wa akiba
Orodha ni ndefu kiasi kwamba wachezaji hao wanaweza kutengeneza kikosi cha kwanza na wengine wakiwa kwenye benchi, kama vile Moussa Dembele (Olympique Lyon, Pauni 50m), James Maddison (Leicester City, Pauni 85m), Mauro Icardi (Inter, Pauni 70m), Adrien Rabiot (Juventus, bure),Declan Rice (West Ham United, Pauni 80m) na Sergej Milinkovic-Savic (Lazio, Pauni 82m).




Credit: mwanaspotiapp

Sent using Jamii Forums mobile app
 
M ASHABIKI wa Manchester United wamepagawa kwa furaha baada ya kuona picha inayowaonyesha viungo wawili wenye ufundi mkubwa wanapokuwa uwanjani Paul Pogba na Bruno Fernandes wakifanya mazoezi pamoja kwa mara ya kwanza.
Viungo hao wawili walionekana wakifanya mazoezi kwa karibu huko Carrington katika makundi ya wachezaji wachache, huku kocha Ole Gunnar Solskjaer akiwapanga pamoja ili kutengeneza muunganiko mzuri kabla ya kuanza kukipiga pamoja kwenye mechi. Fernandes amekuwa kwenye kiwango bora Man United tangu alipojiunga kwa ada ya Pauni 48 milioni akitokea Sporting Lisbon kwenye dirisha la Januari mwaka huu. Katika kikosi hicho cha Old Trafford, kiungo huyo Mreno amefunga mabao matatu na kuasisti mara nne kwenye Ligi Kuu England kabla ya ligi hiyo kusimamishwa kutokana na janga la corona.
Lakini, mashabiki walikuwa hawajawahi kuona wawili hao wakiwa pamoja kwa sababu Pogba muda mwingi alikuwa majeruhi. Na sasa picha hiyo iliyopigwa kwenye uwanja wa mazoezi wa Carrington imewapagawisha mashabiki na wanasubiri kwa hamu kuona watakavyowasha moto pamoja.
Kwenye moja ya picha hizo, ilimwonyesha Pogba akimtazama Fernandes wakati walipokuwa wakifanya mazoezi ya kunyoosha viungo.
Shabiki mmoja aliandika kwenye Twitter, akisema: “Hatimaye tumeona picha za Paul Pogba na Bruno Fernandes wakijifua pamoja. Ligi bora ianze tu.”
Mwingine aliongeza: “Hatimaye, tuna picha tamu kabisa ya Bruno Fernandes akwia na Paul Pogba...”

Akiambatanisha na umoji kibao za kuonyesha mahaba, shabiki mwingine alisema: “Ona jinsi Pogba anavyomshangaa Fernandes.”
Kocha Solskjaer ameshathibitisha kwamba Pogba atakuwa fiti kukipiga wakati ligi itakaporejea. Siku za karibuni, kiungo huyo amekuwa akihusishwa na mpango wa kuondoka Old Trafford, lakini Juventus wanaomtaka wanaweza kuingia mitini kutokana na mchezaji huyo kuhitaji mshahara mkubwa. Kutokana na hilo Pogba bado yupo sana tu Old Trafford, anakolipwa Pauni 290,000 kwa wiki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom