Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Tetesi katika club ya man united ni nyingi sana na ni ngumu sana kusema hii ni ya kweli na hii si ya kweli mpaka unapoona mchezaji kanunuliwa.

Kipindi cha Ferguson kuna wachezaji wengi sana aliwataka bahati mbaya hakuwapata na mara nyingi amekuwa akiweka wazi kuwa alimhitaji mchezaji huyu lakini sikumpata nikampata yule mathalani issue ya Eden Hazard na Lucas Moura, Ferguson aliamua kumnunua Shinji Kagawa.

Club pia pamoja na kwamba kocha anahitaji wachezaji fulani lakini lazima yawe mahitaji realistic na yenye maslahi kwa Club, Bayern isingemwachia Thomas Muller na Arjen Roben kwa urahisi namna ile huku Roben akiwa na miaka 31.

Mimi nachokiona wazi alichokosea Van Gaal alifanya squad overhaul unreasonable usingeweza kuuza wachezaji wengi vile halafu ukategemea maingizo mapya yakupatie kikosi cha ushindani, mbaya zaidi wachezaji wengi alionunua walitoka nje ya epl hivyo walihitaji muda kuzoea ligi.

Ni kweli kwamba uongozi wa man united kwenye suala la transfer una mapungufu yake lakini Van Gaal alipewa support kubwa sana kulinganisha na makocha wengine.

Kuendelea kulialia hakutaondoa uhalisia kuwa alishindwa kuitransform man united kama alivyotaka.
alifanya overhaul yenye nia njema ila takribani wachezaji wote aliowaleta hawakuendana na mpira wa kiingereza (waliiondoka walikuwa ni bora kuliko walioletwa).

jambo hilo ukichanganya na ishu ya majeruhi lilipelekea ajifiche kwenye sera ya kuwapa nafasi vijana kutoka academy ambao hawakuwa tayari kwa mapambano ya ligi (kwa nyakati tofauti alijaribu kuwatumia paddy mcnair, fosu mensah, varela, blacket) na kuna nyakati alihitaji kumtumia mchezaji mfano wa wilson kama ni backup striker na hii ilionyesha dhahiri ya kwamba mzee hakuipa heshima yake premier league.

kati ya makocha watatu waliotangulia naweza kusema louis ndiye kocha pekee aliyekuja na system yenye kueleweka kiuchezaji japokuwa ilileta dhoruba kubwa sana (tactics zake zilimpa mafanikio makubwa sana dhidi ya timu kubwa lakini hatukupata matokeo mazuri dhidi ya timu nyenginezo, alihitaji timu iwe ni kama shirika fulani linatoa huduma kwa raia kwa kila mchezaji kushiriki kwenye process ya kujilinda na hata kushambulia, tuwe na mpira au tusiwe na mpira.

unluckily miaka yake miwili alishindwa kutibu tatizo la umaliziaji na ndilo lililomuangusha. Nakumbuka team ilikuwa inamilika mpira kwa 75% au zaidi lakini tulikuwa hatuwezi kufunga goli.

  • style yake ya kiuchezaji ilitusaidia kwa mechi chache sana
  • sera yake ya usajili ilikuwa ni dhaifu
  • alitupa burudani kwenye mechi kubwa
  • aligeuka kituko kwenye mechi ndogo
  • alinifanya niache kuangalia mechi za man utd baada ya kupoteza kwa magoli matano dhidi ya leicester city (mechi iliniumiza sana, tunacheza mpira mkubwa sana lakini wapinzani wakija kwetu wanatufunga magoli)
 
Lilikuwa ni jambo la ajabu sana kumruhusu Robin Van Persie na Chacharito waondoke hili kwa vyovyote vile lingeathiri sana safu ya ushambuliaji.

Ni kweli philosophy yake timu ilikuwa inacheza vizuri inaposses mpira sana changamoto ilikuwa timu inacheza taratibu sana na ikawa too predictable ndiyo maana tuliadhibiwa na kila timu iliyotaka matokeo kutoka kwetu.
 
huyu mzee anafanya ishu gani kipindi hiki?
namkusudia louis van gaal

tulikuwa tunatabirika kama ole na mechi zake za mwanzoni (ukiweka 2 block una uhakika wa draw)
 
ed woodward aliwatajirisha sana hawa mafala kwa kuwapa mikataba ya gharama baadae anawavunjia mikataba yao.
Woodward alikuwa anapawaya sana kwenye hizi appointments zake za makocha.

Chacharito kasema lilikuwa kosa kumpa kazi Moyes kuwa kocha wa United.

Huenda hata wachezaji wenyewe walikuwa hawako tayari kufanya kazi na hao watu.
 
yule fala alikuja kuharibu kila kitu kwa kujifanya mjuaji, nawalaumu wazungu kwa kuruhusu mfumo huru bila ya kuangalia taathira zake... david hakuwa na sifa kama alizonazo guardiola na makocha wengineo wanaofahamika kiheshima na si kimajina.
hivyo basi halikuwa jambo sahihi kumruhusu ahamie nyumbani kwetu na kila kitu chake matokeo yake alikuja nyumbani na godoro lenye kunguni.

hatukuwa na team bora kama ilivyo barcelona lakini tulikuwa na msingi bora uliohitaji kuongezewa nondo kidogo...
 
Hahaha ni kweli hata ile kuja na benchi lake lote la ufundi ulikuwa ni upofu wa hali ya juu sana.

Alichokifanya ni kuharibu hata msingi wa timu ikalazimika tuanze upya tena kwa kujitaji marekebisho makubwa.

Hata hivyo kosa linaweza lisiwe na Moyes mwenyewe bali liwe la mamlaka iliyompa kazi maana hakustahili hata kuwa kwenye top ten ya orodha ya makocha wanaoweza kupewa ile kazi.
 
KOCHA wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer ameripotiwa kushika usukani kwenye mbio za kufukuzia huduma ya staa moto kabisa kwenye soka la Ujerumani kwa sasa, Kai Havertz.
Man United wanamtazama staa huyo wa Bayer Leverkusen kuwa ni mwenye kipaji cha kutosha cha kwenda kucheza kwenye kikosi chao wakiamini kwamba atakuwa mchezaji wa daraja la juu sana siku chache zijazo.
Kocha Solskjaer amepanga kuua ndege wawili kwa mpigo huko Ujerumani, akimtaka pia staa wa Borussia Dortmund, Jadon Sancho, ambaye usiku wa juzi Jumapili alipiga hat-trick, wakati timu yake ilipoichapa Paderborn 6-1 kwenye Bundesliga.
Mpango namba moja ni kumsajili Sancho, lakini baada ya hapo watamnasa pia Havertz, ambaye wanaamini wasipofanya hivyo mwaka huu basi thamani yake itakuwa kubwa zaidi mwakani.
Kwa kuanzia, Man United imepeleka ofa ya Pauni 50 milioni ya kunasa saini ya Havertz, huku wakiamini mkwanja huo utatosha kabisa kwenye kupata huduma ya mchezaji huyo wanayemsaka kwa nguvu zote.
Havertz amekuwa akiwindwa na vigogo msimu huu baada ya kufunga mabao 15 katika michuano yote. Man United wameshafahamu watamtumiaje, ikiwa ni pamoja na kumchezesha kwenye wingi moja au akitokea kwenye kiungo ya kati.
Mpango ni kwamba Havertz atacheza kulia, kushoto atakuwapo Sancho na Marcus Rashford atasimama katikati. Hata hivyo, huduma ya Sancho haiwezi kupatikana kirahisi, lazima mkwanja unaoanzia Pauni 100 milioni na kuendelea.
Aidha, United imekubaliana na klabu ya Shanghai Shenhua ya China kubaki na Odion Ighalo hadi Januari 2021.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aisee
 
MTAPOTEANA UWANJANI: BENCHI VIFAA NDANI VIFAA, OLE KAPANIA

MANCHESTER United imeripotiwa kwamba inataka kutumia janga la virusi vya corona kama fursa ya kuzilalia klabu nyingine na kunasa mastaa wao kwa bei nafuu wakakipige Old Trafford msimu ujao.
Kinachoelezwa ni kwamba Man United wanasubiri tu dirisha la usajili wa majira ya kiangazi lifunguliwe ili kuanza kufukuzia dili zake huku wakiamini itanasa wachezaji inaowataka kwa pesa ndogo kutokana na timu nyingi huko Ulaya kwa sasa kutikiswa kiuchumi kutokana na janga la corona.
Kuna wachezaji wawili wamekuwa wakihusishwa sana na Man United, Saul Niguez na Jadon Sancho, huku kinachoripotiwa ni kwamba dili za wachezaji hao ni kama zimeshakamilika na kinachosubiriwa dirisha lifunguliwe tu.
Man United inaweza kunasa huduma ya wachezaji hao wawili kwa Pauni 130 milioni, wakiamini wataokoa Pauni 100 milioni kwenye bajeti yao ya usajili waliyopanga kutumia kwenye dirisha lijalo la usajili kama si corona ingeleta shida.
Usajili wa Saul na Sancho ukikamilika, basi kocha Ole Gunnar Solskjaer atakuwa ametengeneza kikosi matata kabisa kuja kuwashika wapinzani msimu ujao.
Kama dili hizo mbili zikitiki, kikosi cha kwanza cha Man United kwa msimu ujao kitakuwa hivi, ambapo golini ni kipa David de Gea, beki wa kushoto ni Luke Shaw, beki wa kulia ni Aaron Wan-Bissaka na mabeki wa kati watakuwa Harry Maguire na Victor Lindelof.
Kwenye sehemu ya kiungo katika kikosi hicho kitakachotumia fomesheni ya 4-2-3-1, Saul atacheza na Paul Pogba, wakati mbele yao, kwenye safu ya wachezaji watatu watakaocheza nyuma ya mshambuliaji wa kati, Anthony Martial, kulia atakuwa Sancho, kushoto Marcus Rashford na namba 10 ni Bruno Fernandes.
Kutokana na janga la corona, Man United imeripotiwa kwamba inataka kukamilisha dili hizo tu mbili kwenye dirisha lijalo huku wakimzuia Pogba kuondoka wakiamini kwamba watakuwa wametengeneza timu itakayokuwa na uwezo mkubwa wa kupunguza pengo la ubora lililopo baina yao na wapinzani wake kwenye Ligi Kuu England kama Liverpool na Manchester City.

mwanaspotiapp

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom