Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Huko duniani kuna tetesi kuwa Man united inamhitaji winger wa Shaktar Donetsk anaitwa Kenny Tete.

Kuna ukweli wowote wa taarifa hizi?

Je kiwango cha huyu dogo kikoje ?

Sent using Jamii Forums mobile app
Hii sidhani kama ni kweli Man U wana nia nae. Ila ninachojua huyu dogo alisema anatamani sana kuchezea Man U au Liverpool. Sijui ni dream ya namna gani hii! Kiwango chake si haba sana ila si kama Sancho. Hata wing ya Martial naona ni nzuri zaidi yake. Ila kwa kifupi ni promising star,hasa ukizingatia ni Bado Mdogo mana ni under 20
 
Wakuu mpaka sasa naona swala la Sancho na Glearish kwa pamoja limekua serious sana kuja OT kuliko usajiri wa Kane.

Jamie Rednap alikua anaojiwa akasema anatamani Sancho ajiunge na Liverpool ila anajisikia vibaya kuona kila dalili inaonyesha dogo akielekea Manchester United na ukijumlisha chats za Sancho na Rashford naona deal done

Kwa navyomfaham woodward mzee wa kupenda wachezaji wa kuuza jezi, jezi #7 inamsubiri dogo pale stretford end
About Kane ile price tag ya daniel levy + age + injury prone sioni woodward atakubali deal kufanyika
Pia naona Ighalo akiongezewa mkataba, pia naona Greenwood akipewa nafasi sana kuongoza mashambulizi mbele akisaidiana na bishoo martial uku rashford akitokea kushoto
Pogba anaiitaji Man United kuliko Man united inavyomuitaji, 27 years old now, naona akiongeza mkataba mnono wa 4years + 1year extended options

Chriss Smaling kule Roma kaimalika mno, namuona akirejea kupambania namba na kina wemzake kina Linderof/bailly/tuanzebe

GGMU

Hahaha wasisahau na kusajili straika tu.
Jimenez.
Harry Kane

Wote poa tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahaha wasisahau na kusajili straika tu.
Jimenez.
Harry Kane

Wote poa tu

Sent using Jamii Forums mobile app
Kane ile price tag ya pounds 150 - 200 mil sioni deal likifanyika + age + injury na hali ya uchumi wa corona Man utd ngumu kusajiri Sancho na Kane kwa dirisha moja, uyo Jimenez sawa ila itategemea OGS kama atamua kumpa mkataba Ighalo au lah

All in all tutashuhudia damu yetu greenwood akipewa nafasi sana next season, uwepo wa pobga na bruno huyu dogo atashangaza watu sana next season

Solskjaer anaweza kupata option nyingi kwenye kikosi kwa ujio wa Sancho kuliko Kane.
Nafikiri Sancho ni muhimu zaid ya Kane kwa sasa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Binafsi ningependa Harry Kane awe chaguo #1 ktk watu wanaopaswa kuja kuiweka sawa timu yetu hao wengine wawe ni fallback plan tu baada ya dili la Harry kubuma. Tunahitaji kuweka mezani Pound Sterling 100M take-it-or-leave-it Deal, baada ya hili janga la Covid-19 hakuna timu itakayo kuwa tayari kutanua bajeti kizembe zembe kama sio hitaji la msingi na timu pekee duniani yenye uhitaji wa mshambualiaji na yenye pesa ni Manchester United tu.

Daniel Levy analitambua hili and he's just bluffing. Sisi ndio wateja pekee wa Harry sokoni kwa sasa sema jamaa ana-take advantage ukilaza wa Ed Woodward ku-inflate thamani halisi. Kwa mtu anayetizama beyond the smoke sisi ndio tumeshika mpini.

Spurs wanatuhitaji sisi na pesa yetu zaidi kuliko sisi tunavyomuhitaji Harry Kane kwa sasa. Kwa kifupi hawana pesa hata kabla ya Covid-19 walianza ku-struggle financially kiasi kikubwa kiliwekezwa ktk uwanja wao mpya.
 
Wakuu mpaka sasa naona swala la Sancho na Glearish kwa pamoja limekua serious sana kuja OT kuliko usajiri wa Kane.

Jamie Rednap alikua anaojiwa akasema anatamani Sancho ajiunge na Liverpool ila anajisikia vibaya kuona kila dalili inaonyesha dogo akielekea Manchester United na ukijumlisha chats za Sancho na Rashford naona deal done

Kwa navyomfaham woodward mzee wa kupenda wachezaji wa kuuza jezi, jezi #7 inamsubiri dogo pale stretford end
About Kane ile price tag ya daniel levy + age + injury prone sioni woodward atakubali deal kufanyika
Pia naona Ighalo akiongezewa mkataba, pia naona Greenwood akipewa nafasi sana kuongoza mashambulizi mbele akisaidiana na bishoo martial uku rashford akitokea kushoto
Pogba anaiitaji Man United kuliko Man united inavyomuitaji, 27 years old now, naona akiongeza mkataba mnono wa 4years + 1year extended options

Chriss Smaling kule Roma kaimalika mno, namuona akirejea kupambania namba na kina wemzake kina Linderof/bailly/tuanzebe

GGMU

Sent using Jamii Forums mobile app
Timu yetu inavyokuwaga na matetesi mengi sijaisahau mkuu ha ha ha ha. Unaweza kuta ni magazeti na media nyingine tu ndio ziko serious na usajili wa Sancho na wenzake na si ED Woodward na genge lake. Leo imeanza kuibuka nyingine ya kumuhitaji Joao Felix!
 
Binafsi ningependa Harry Kane awe chaguo #1 ktk watu wanaopaswa kuja kuiweka sawa timu yetu hao wengine wawe ni fallback plan tu baada ya dili la Harry kubuma. Tunahitaji kuweka mezani Pound Sterling 100M take-it-or-leave-it Deal, baada ya hili janga la Covid-19 hakuna timu itakayo kuwa tayari kutanua bajeti kizembe zembe kama sio hitaji la msingi na timu pekee duniani yenye uhitaji wa mshambualiaji na yenye pesa ni Manchester United tu.
nakubaliana na hoja yako,
harry kane ni aina ya mchezaji ambaye pindi anapokuwepo sokoni huhitaji kujiuliza mara mbili ili ufanye uamuzi wa kumsajili, ndio maana baadhi yetu humu ndani tumekuwa tukisisitiza kwa nyakati tofauti ya kwamba halitakuwa jambo rahisi kwa klabu kufanya biashara mbili za gharama kubwa kwa dirisha moja (usajili wa harry kane na mchezaji mwengine wa kiingereza either maddison, grealish au jadon sancho).

cha kufanya ni kupiga hesabu kwa umakini zaidi ili kuweza kufahamu eneo lipi ni muhimu zaidi kulifanyia uwekezaji (mshambuliaji au winga wa kulia tatizo ambalo tunalo kwa takribani miaka 8), wengine wanashauri usajili wa gharama uelekezwe kwa mshambuliaji kama ulivyoeleza hapo juu na wengine tunashauri usajili wa gharama uelekezwe zaidi kwa winga mfano wa jadon sancho.

Pia wengine wanaamini usajili muhimu unapaswa uelekezwe kwa mchezaji atakayetupa faida zaidi ya moja atapokuwepo uwanjani (mfano jack grealish, james maddison wote wana uwezo wa kufiti nafasi na mfumo zaidi ya mmoja).

nafahamu kama tunahitaji depth squad basi uamuzi utakaofanyika hauhitaji kuangalia zaidi taathira zitakazowapata wachezaji fulani tunaopenda kuwaona wakiendelea kupewa nafasi... lakini itapendeza zaidi endapo sadaka tutakayoitoa isiwaumize na kuwavunja moyo na morali vijana wetu wenye ndoto za kuongoza jahazi la mapambano siku za mbeleni

usajili wa jadon sancho:
usajili huu utakuja kupunguza dakika za kucheza alizokuwa akipewa mason greenwood msimu huu., kupitia mechi za msimu huu tumeshuhudia mechi nyingi sana alizokuwa akicheza greenwood alikuwa anatokea zaidi upande wa kulia kuliko eneo la striker eneo ambalo siku za mwishoni za romelu lukaku alikuwa akichezeshwa kabla ya kuhama kwake. Kiupande wangu naendelea kuamini ya kwamba mason greenwood hapaswi kuwa mchezaji tegemezi kwenye kikosi chetu hivyo basi tunahitaji mchezaji mwengine mwenye uzoefu na kiwango kikubwa zaidi ya mason ili awe namba 7 wetu wa kudumu, namuona jadon akiwa ni mchezaji sahihi kama atakuja na kiwango kile tunachokishuhudia borussia dortmund.

Pia usajili wa mchezaji aina ya jadon utapelekea kuzibwa au kupungua kwa nafasi ya daniel james kwenye kikosi cha kwanza, tukumbuke mechi nyingi sana za msimu huu baada ya rashford kurudishwa upande wa kushoto tulishuhudia daniel james akichezeshwa upande wa kulia...Hii ina maana ya kwamba daniel james atakwenda kugombania namba na marcus rashford upande wa kushoto (ni challenge ngumu sana kwake lakini haiepukiki)

kwa nini Ighalo?
si mshambuliaji bora mbele ya kane, jimenez na wengineo lakini uwepo wake ndani ya kikosi utakuwa ni tofauti na hao wengineo kwa sababu tayari ameshajiandaa kuishi maisha ya kuwa mchezaji asiyehitajika mara kwa mara kwenye kikosi cha kwanza. Litakuwa ni pigo kubwa sana kiupande wetu kwa sababu tutaendelea kumtegemea goigoi anthony martial lakini itakuwa ni faida kubwa sana kwa wachezaji wengineo mfano mason greenwood.....upo utofauti mkubwa sana pindi unapogombania namba dhidi ya kane au ighalo.

pia uwepo wa Ighalo utasaidia zaidi kutuepusha na panic transfer,utatuwezesha kumonitor au kuangalia tena mwenendo wa anthony martial (tukumbuke huu ndio kwanza msimu wake wa kwanza martial kucheza eneo la striker mechi nyingi zaidi lakini takwimu zake zinaonyesha kufunga zaidi magoli kuliko washambuliaji wengine) pamoja na mason greenwood ambaye bado hatujajua ubora wake kama striker wa team kubwa,

wakati huo huo uwepo wa ighalo utasaidia katika harakati zetu za kutafuta na kuwachunguza washambuliaji wengine watakaokuja kuziba nafasi yake kama vile haaland kama ataendelea kuwepo dortmund, martinez kama atakuwepo inter milan, levit kama ataendelea kuwepo everton n.k.

sancho + bruno fernandez + pogba= martial na rashford watakuwa na uhakika wa kutupa magoli 20 kwa kila mmoja.

striker tunaovumishwa kuwahitaji msimu huu dhidi ya martial

Martial - 14 goals in 26 games (msimu wake wa kwanza kucheza eneo la ushambuliaji mechi nyingi)
Jimenez - 16 goals in 35 games
Dembele - 17 goals in 32 games (anacheza French league)
Edouard - 28 goals in 43 games (anacheza Scottish league)
Maxi Gomez - 6 goals in 22 games
Calvert Lewin - 13 goals in 23 games (everton)
===========================================
 
jambo jengine nililojifunza inaonekana ole gunnar anavutiwa sana na mshambuliaji anayetumia mguu wa kushoto (jaribu kurejea tetesi za dyabala, alexander Sorloth kutoka trabzonspor ya uturuki na haaland) na kama ndicho anachokifikiria basi sidhani kama tutaelekeza nguvu zetu kwa harry kane kama chaguo la kwanza na la muda mrefu.

  1. kabla mahusiano ya lukaku hayajavurugika alimhitaji lukaku awe mchezaji anayetembea na mechi, kwa maana ya kwamba asiwe mshambuliaji anayesubiri kuhudumiwa bali atokee upande wa kulia kama ilivyo kwa greenwood then awe ana cut inside.
  2. kwa mifumo ya 4-2-3-1 na 4-3-3 inapendeza zaidi kama utakuwa unatumia strikers in wide positions kama vile greenwood na marcus rashford, ukija kwenye mfumo wa 3-5-2 inapendeza zaidi kama washambuliaji wako wawili watakuwa na uwezo wa kutumia miguu tofauti.
  3. kwa sasa ndani ya team tuna mshambuliaji mmoja tu anayetumia kwa usahihi mguu wake wa kushoto (mason greenwood), nadhani kuna umuhimu wa kutafuta mshambuliaji mwengine mahiri anayetumia mguu wa kushoto ili kuwa na balance ya kikosi.
pia huenda tukamrudisha alex sanchez
 
Alex sanchez nimekuwa namfatilia huko inter jamaa ni uchafu tu anatuaibisha man u huko italia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna comment nimesoma nimeshangazwa kidogo, kuna watu hawaangalii takwimu za wachezaji. Nimeona watu wanasema Harry Kane ni injury prone hii kitu si kweli.

Harry ameanza kucheza rasmi Spurs kama regular player kuanzia 2014/2015 kabla ya hapo alicheza mechi 11 muda mwingi amekuwa nje kwa mkopo. Amecheza mechi 187 kati ya mechi 219 mpaka msimu huu tulioshia mechi 29 na amefunga magoli 133. Amecheza mechi nyingi kuliko mchezaji yeyote wa Manchester United ukimuondoa David Degea ndani ya misimu sita.

Sasa twende taratibu 2014/2015 - 2019/2020 mchezaji aliyecheza mechi 187 kati ya 219 na kufunga magoli 133 ni injury prone? Katika misimu yote sita ni miwili miwili tu uliopita na msimu huu amecheza mechi chini ya 30 na sehemu kubwa yeye amekuwa hapumzishwi na hana mbadala pale Spurs ndio maana amekuwa akipata majeraha ya mara kwa mara siku za karibuni.

Kuhusu umri, c'mon guys he's 26 years old. Hii ndio peak age kwa mchezaji yeyote yule yaani ana misimu mitano ya kucheza competitive games. Kwangu mimi sioni mshambualiaji yeyote hapa ulimwenguni aliye sokoni ambaye ni sure bet kuja kucheza Manchester United nje ya Harry, the best part chini ya moyo wake jamaa anaipenda sana Manchester United. Ni aina ya mchezaji kama Scott McTominay atakuja kucheza timu ambayo ana mahaba nayo pia.
 
Back
Top Bottom