Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Bruno ana impact ndio lakini fahamu pia amekuta wachezaji wapo form ie.fred,matic,shaw pia usajili wake haukua na big expectations sana hii ilimsadia kutuliza akili.
Ni makosa makubwa kusema mchezaji mmoja anaamua future ya kocha utafikiri unazungumzia masumbwi
Kaka P hayo sifaham, nachojua ni kua Bruno kashika kura ya Ole!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwan Kaka anayefanya saiv united ionekane ni timu ni nani kama siyo bruno?

Bruno apewe wiki 8 tu uone mtifuano utakaokuwepo!

Anayeaminisha kula kwa ole saiv ni Bruno.
Timu ina cleen sheet nyingi..so unataka kusema na hili Bruno ndo kachangia??..

Lazima tukubali wachezaji wetu pia walikuwa wameanza kurudi kwenye form zao..mfano Shaw na Matic..

Ole ndo aliyemsajili Bruno,kwahiyo hata timu ikiimprove kisa yeye(kama unavyosema wewe) bado Ole ina stahili kupewa sifa..

Tukumbushane tu kuwa Mourinho yupo Spurs,kama kuna mtu anampenda sana anaweza kuhama naye..
 
wamfuate Mou eh

Ligi ifutwe tuanze upya Liverpool hawatakiwi kupata ubingwa aisee.

Tupewe certificate of participation tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Je premier league wako tayari wapate loss ?

Hii league itaendelea hata kwa mechi kuchezwa bila mashabiki
Uzuri ni euro ishakuwa postponed so kwa namna yeyote ile league zitaisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mnaosema ligi ifutwe, tuanze upya.

Kumbukeni itatubidi tucheze Europa tena. Halafu Arsenal acheze Champions league .

Beggars can't be choosers
 
CORONA YAISHIKA PABAYA MAN UNITED

THAMANI ya Manchester United kwenye soko la hisa la Marekani imeporomoka kwa Pauni 1 bilioni kutokana na mlipuko wa virusi vya corona unaozidi kuitikisa duniani kwa sasa.
Michuano kibao ya soka duniani, ikiwemo Ligi Kuu England na Ligi ya Mabingwa Ulaya imesimama kutokana na mlipuko wa Corona ambao hadi sasa umesababisha vifo vya watu 7,900.
Inaelezwa mlipuko huo umesababisha mtikisiko kwenye soko la hisa la Marekani na thamani ya Manchester United imeshuka kutoka Pauni 3 bilioni hadi Pauni 2 bilioni.
Mwezi mmoja uliopita miamba hiyo ya England ilikuwa na thamani ya Pauni 3 bilioni, lakini tangu mlipuko wa Corona hisa hizo zimeshuka thamani kwa kasi kubwa sana, hisa moja imeshuka hadi Pauni 9.99 kutoka 16.53 mwanzo wa mwaka huu.
Man United ilinunuliwa na family ya Glazer mwaka 2005 kwa thamani ya Pauni 790 milioni ambayo imepanda licha ya wamiliki hao kupingwa sana na mashabiki kutokana namna wanavyoendesha klabu hiyo.
Tangu mwaka jana, Mwana Mfalme wa Saudi Arabia, Mohammed bin Salman amekuwa akijaribu kuinunua timu hiyo huku wamiliki familia ya Glazer ikiweka wazi inataka Pauni 3 bilioni ndiyo iuze klabu hiyo.
Kama wakifanikiwa kuuza kwa bei hiyo watapata faida mara zaidi ya tatu ya kile ambacho baba yao Malcolm Glazer alitumia wakati akiinunua timu hiyo.
Lakini, wakati huu ambao timu hiyo imecheza mechi 11 bila kufungwa, mlipuko wa virusi vya Corona unaonekana kuharibu mambo Old Trafford.
Inaelezwa nahodha mpya wa timu hiyo, Harry Maguire ndiyo amerudisha umoja ndani ya klabu hiyo kutokana na kuanzisha vipindi vya kuzungumza usiku kila baada ya mazoezi.
Wakati huo huo; Mlipuko wa virusi vya corona unazidi kuleta majanga kwenye timu za Ligi Kuu England na sasa kuna taarifa kuwa vituo vya televisheni vya Sky Sports na BT Sport vimepanga kuvishitaki vilabu hivyo kama msimu hautaisha.
Inaelezwa kampuni hizo mbili za televisheni zitazipiga faini ya Pauni 750 milioni klabu za ligi kuu kama msimu usipoisha kwa kuvunja makubaliano ya kimkataba.
Taarifa kutoka England zinadai mkataba wa vituo hivyo na klabu za ligi kuu unaeleza wazi vituo hivyo vimenunua haki ya televisheni ya msimu mzima hivyo kama msimu ukiishia nusu ni kuvunja makubaliano ya kimkataba.
Hata hivyo, kwa jumla madai ya vituo hivyo vya televisheni yatapelekwa kwenye vyombo vya sheria ikiwa tu hiyo Aprili 4, ligi itashindwa kuendelea kama ilivyokuwa imepangwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mnaosema ligi ifutwe, tuanze upya.

Kumbukeni itatubidi tucheze Europa tena. Halafu Arsenal acheze Champions league .

Beggars can't be choosers
Arsenal atachezaje Champions League?

Si msimu huu tulikuwa naye Europa na juzi kati alitolewa na Olympiacos hatua ya 32 bora?
 
Arsenal atachezaje Champions League?

Si msimu huu tulikuwa naye Europa na juzi kati alitolewa na Olympiacos hatua ya 32 bora?
Msimu huu ukifutwa, si itabidi zipatikane timu za kwenda Champions League na Europa League.
Si watachukua msimamo wa msimu uliopita(msimu uliokamilika).
Maana msimamo wa msimu huu, league itakuwa imefutwa.
Arsenal alimaliza nafasi ya tano. Kutegemeana na ban ya Man city. Arsenal anaingia CL.

Ni mawazo yangu tuu.

Beggars can't be choosers
 
POGBA ANAUZWA KWA MILION 100

Manchester United imeripotiwa kutangaza dau la pauni 100 milioni kwa klabu itakayo mtaka kiungo wake Paul Pogba.
Kwa mujibu wa jarida la The Sun, imeelezwa kua pande zote mbili zimefikia uamuzi huo huku ukiwa umebakia mwaka mmoja kwenye mkataba wenye kipengele cha nyongeza ya mwaka mmoja mwengine.
Awali mwaka jana Manchester United ilikataa ofa ya pauni 150 milioni wakati ambao ulibakia mwaka mmoja kwenye mkataba wa kiungo huyo.
Pogba ambaye amekuwa akisumbuliwa na majeruhi jambo lililomfanya kutoonekana uwanjani tangu Septemba mwaka jana. alishindwa kukamilisha dili la kuelekea Real Madrid kwenye dirisha kubwa la usajili na kwa sasa inaelezwa kuwa, klabu za Juventus na Real Madrid zinachuana vikali kuipata saini yake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uwe unaweka source ya magazeti yako humu

Sio April 4 tena, mpaka April 30 ndio kuna uwezekano wa kuona EPL tena
skysports___B96pqcAIpM-___.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom