Ananukiaaaa
Screenshot_2020-01-17-20-48-41-2131169281.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
issue sio ubahiri, usajili una mambo mengi sana. muda mwingine jiulize kwa nini usajili wa mchezaji fulani timu nyingine zimejiweka kando mmeachwa peke yenu mnapambana?

mbona haaland haikuwa hivyo? juve, mara madrid
de light timu kibao na akaenda juve.

ila huyu hata arsenal tu hawana time naye ni nyie tu man utd.

ni mzuri sana eeeh?

Sent using Jamii Forums mobile app
Huyo jamaa ni mzuri mkuu, Halafu usajiri sio kama kununua nyanya sokoni

Usajiri ni process ,ni Agreement kati ya klabu na klabu , klabu na mchezaji .
 
Nitajie timu ulizosikia zinataka kumsajili Messi? Kumbe ni mbovu?
issue sio ubahiri, usajili una mambo mengi sana. muda mwingine jiulize kwa nini usajili wa mchezaji fulani timu nyingine zimejiweka kando mmeachwa peke yenu mnapambana?

mbona haaland haikuwa hivyo? juve, mara madrid
de light timu kibao na akaenda juve.

ila huyu hata arsenal tu hawana time naye ni nyie tu man utd.

ni mzuri sana eeeh?

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
UNALIJUA tatizo la Manchester United? Ni eneo la kiungo kukosa ubunifu. Wenyewe wameshtukia hilo ndiyo maana wanatumia muda mwingi kutafuta fundi wa kuweka mambo sawa.
Ukiangalia utagundua kwamba asilimia kubwa ya wachezaji wanaosakwa na Man United ni viungo wachezeshaji ili waje kulainisha eneo la kiungo la timu hiyo ambalo limekosa udambwi.
Ndiyo maana baada ya kuzunguka sana kutafuta mchezaji wa kuimarisha eneo hilo sasa inaonekana kocha Ole Gunner Solskjaer ameamua kukomaa na kiungo fundi wa Sporting Lisbon, Bruno Fernandes.
Baada ya kumkosa katika dirisha la usajili lililopita inaonekana sasa Man United imepania kumchukua Januari na kwa mujibu wa taarifa kutoka Manchester wakati wowote kutoka sasa Fernandes anatua Old Trafford.
Swali ni je, Fernandes anaongeza kile ambacho Man United imekuwa ikikikosa katikati ya uwanja? Jibu la swali hili linakuwa jepesi kama ukilijibu kwa kuangalia takwimu za Bruno kisha kulinganisha na za viungo waliopo Trafford.


Bruno Fernandes, Mechi 15
Akiwa na kikosi cha Sporting Lisbon msimu huu Fernandes amecheza mechi 15, katika mechi hizo ametumia dakika 1349 uwanjani, huku akihusika moja kwa moja katika mabao 15 ya Sporting Lisbon hii ni baada ya kufunga mabao nane na kupiga pasi za mabao saba na kutengeneza nafasi 55 za kufunga. Takwimu hizi si haba kwa mchezaji wa kiungo si ajabu kuona Ed Woodward akipambana kumpeleka Old Trafford.


Daniel James, Mechi 21
Akiwa na miezi sita tu kwenye kikosi cha Man United, James ameibuka kuwa mchezaji muhimu sana katika timu hiyo, akishambulia kutokea pembeni staa huyo amecheza mechi 21 za michuano yote msimu huu, sawa na dakika 1667 na kuhusika moja kwa moja katika mabao tisa ya timu hiyo, akifunga matatu na kutoa pasi za mabao sita, huku akitengeneza nafasi 23 za kufunga.


Andreas Pereira, Mechi 19
Kwa sasa Pereira ndiyo amekuwa akitumika nyuma ya washambuliaji akiwa na jukumu la kutengeneza nafasi na kufunga anapopata nafasi, katika mechi 19 alizocheza, dakika 1251 amehusika kwenye mabao manne tu, akifunga moja na kutoa pasi za mabao tatu huku akitengeneza nafasi za kufunga 29.


Fred, Mechi 18
Inawezekana nafasi na majukumu yake ndiyo sababu kubwa ya kutokuwa na takwimu za kuvutia mbele ya goli. Katika mechi 18 alizocheza, yaani dakika 1408, msimu huu Fred hajahusika hata kwenye bao moja la Man United, huku akitengeneza nafasi 24 tu katika mechi hizo.


Jesse Lingard, Mechi 18
Huyu ni mmoja wa wachezaji ambao kwa kiasi kikubwa wamechangia kikubwa Man United iingie sokoni kutafuta kiungo mchezeshaji. Licha ya kutumika kama kiungo mchezeshaji takwimu za Lingard zinakatisha tamaa. Unaambiwa katika dakika 868 alizocheza hajafunga wala kutoa pasi ya bao, huku akitengeneza nafasi 19 tu, akizidiwa hata na Fred ambaye anacheza chini zaidi uwanjani.


Scott McTominay, Mechi 17
Inaaminika majeraha aliyoyapata ni moja ya sababu za Man United kuingia sokoni kutafuta kiungo, katika dakika 1453 alizocheza msimu huu, McTominay ambaye amekuwa akitumika zaidi kama kiungo wa boksi kwa boksi amehusika kwenye mabao manne, akifunga matatu na kutoa pasi ya bao 1, huku akitengeneza nafasi 15, na kuwa na mchango mkubwa sana katika kuzuia.


Juan Mata, Mechi 13
Katika ubora wake Mata ni mmoja kati ya viungo bora sana wa ushambuliaji, lakini kila siku anaonekana kuzidi kupoteza makali yake kwenye eneo hilo. Msimu huu amecheza dakika 521 tu na katika muda huo amehusika katika mabao mawili ya Man United, kutokana na kupiga pasi za mwisho mbili na kutengeneza nafasi 12.


Paul Pogba, Mechi 7
Majeraha na nia yake ya kutaka kuondoka Man United kwa kiasi kikubwa sana ndiyo sababu za timu hiyo kumfuata Fernandes ili aje kuziba pengo lake na kuongeza nguvu kwenye safu ya kiungo ya timu hiyo. Msimu huu Pogba amecheza mechi saba tu, sawa na dakika 521 na kuhusika kwenye mabao mawili ya timu hiyo kutokana na kupiga pasi za mwisho mbili huku akitengeneza nafasi 16 za kufunga.


Nemanja Matic, Mechi 6
Umri na majukumu yake uwanjani vinamfanya asihusike sana kwenye ushambuliaji ndiyo maana takwimu zake kwenye kushambulia si nzuri kabisa, katika dakika 421 alizocheza, Matic hajahusika hata na bao moja la Man United, na kutengeneza nafasi moja tu katika mechi sita.


Tahith Chong, Mechi 2
Chong ndiyo anapandishwa kikosi cha kwanza cha Man United akitokea timu ya vijana ya klabu hiyo, bado hajaanza kupata nafasi ya kudumu ndiyo maana amecheza dakika 24 tu msimu huu akiwa hajahusika kwenye bao lolote la Man United na wala hajawahi kutengeneza nafasi ya kufunga.


Angel Gomes, Mechi 2
Kama ilivyo kwa Chong, Gomes naye bado kinda na bado hajana na nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza ambapo katika dakika 19 alizocheza msimu huu ametengeneza nafasi mbili tu za kufunga akiwa hajawahi kupiga pasi ya bao wala hajawahi kufunga.


James Garner, Mechi 1
Kinda mwingine kwenye kikosi cha Man United, Garner msimu huu kacheza dakika nane tu na hajawahi kufunga, kupiga pasi ya bao wala kutengeneza nafasi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
MANCHESTER United imedaiwa kukamilisha dili la kumsajili beki wa kati wa Napoli, Kalidou Koulibaly kwa mkwanja unaozidi Pauni 60 milioni.
Koulibaly amehusishwa pia na Tottenham na Arsenal, lakini kwa mujibu wa taarifa za kutoka Italia, Man United imefanya haraka kuinasa saini yake. Hata hivyo, beki huyo hatajiunga na timu yake mpya Januari, atasubiri hadi mwishoni mwa msimu, huku saini yake ikidaiwa itakuwa kitu muhimu kwenye kuimarisha beki ya wababe hao wa Old Trafford.
Mwandishi wa habari wa Italia, Fabio Santini amefichua taarifa hizo alipozungumza kwenye kipindi cha televisheni cha Il Processo aliposema Napoli itampiga bei Koulibaly kwenda Man United kwa ada ya kati ya Euro 70 milioni hadi Euro 75 milioni na kinachoonekana dili limeshafika patamu.
Kwa muda mrefu sasa mashabiki wa Man United wamekuwa wakilialia kutaka timu yao ijasajili beki mwingine wa kati wa kiwango cha dunia kwenda kuungana na beki wao Harry Maguire.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom