Hv ulishawahi kumuona Ferguson akicheka pale United inapopoteza?Ferguson alikuwa anaonyesha hisia fulani ambazo zilikuwa zinaonyesha wazi amekasirika.Alikuwa mpaka analaumu waamuzi na kutoa lugha kali.Alishawahi kusema kwenye press conference 'nashangaa leo mwamuzi alikuwa hawezi kukimbia kwenda na kasi ya mchezo.Nadhani alikuwa ameshiba sana lunch.'
Alipigwa faini na kufungiwa mechi alipotoa hii kauli.Labda ndio maana watu wengi mpaka leo wanaamini kwamba United ilikuwa inabebwa na waamuzi lakini press conference ndiyo inatoa picha halisi ya aina gani ya kocha aliyepo kwenye timu.
Ole Gunnar Solskjaer jana kwenye press conference alionyesha wazi kwamba anaishukuru 'mizimu 'iliyompa bahati ya kuwa kocha wa timu kubwa kama United.Alisema 'pamoja na kupoteza tulicheza vizuri 'huku akitabasamu.Tena sio kwa tabasamu la kawaida kawaida tu. Tabasamu lile wazungu wanaloita 'genuine smile kama anavyoonekana kwenye picha hapo chini.
Usingeweza kuona kitu kama hiki kutoka kwa Ferguson.Siku ambayo United ingepoteza dhidi ya Arsenal ungemuona tu akiwa amefura macho mekundu 'kwa kweli tulikuwa ovyo sana leo tumeruhusu magoli rahisi sana'.Lakini asingeweza kuongea hivyo huku akiwa anatabasamu wakati ametoka kufungwa na Arsenal.United mara nyingi huifunga Arsenal iwe Emirates au Old Trafford.
Ole Gunnar Solskjaer ana bahati kubwa kuifundisha United. Ni kijana wa Carrington.Ni United 'through and through na anapokaa kwenye bench washabiki wote wanajifeel wapo na mtu mwenye damu ya United Lakini ni muhimu awe halisi na asiwe kama muigizaji mbele ya vyombo vya habari.
View attachment 1309982