U mr yes man wa Ole utamcost kazi yake mwenyewe sidhani kama Ole ataendelea kuwa na matokeo mabovu namna hii sidhani kama shekhe Woodward ataendelea kumvumilia
kwa mujibu wa ratiba mwezi wa december utakuwa ni mgumu sana kwake.
jambo linaloleta matumaini kiupande wetu ni kutokupoteza mechi kubwa yeyote tuliocheza msimu huu.

aston villa + tottenham + man city + everton + wattford
 
Nadhani huyu jamaa amekuwa guaranteed na bodi ya kutofukuzwa

Ukiangalia maamuzi yake kwenye usajili, utagundua kuwa hana haraka ya kufanya vizuri, he is so reluxed
 
Japo matokeo ya mechi za mwishoni yalipaswa kumfanya Ed ajiulize mara mbili mbili, alipaswa kupewa mkataba baada ya msimu kuisha

Kwa Ed/Glazers it was the cheapest option
 
Maguire yupo fiti, Lindelof yupo fiti, Axel yupo fiti, nadhani utakuwa umenielewa

Anapaswa kuwa makini zaidi, kwani wenzake akina Shaw, Lingard (captain wetu leo) na Lee Grant wote wameenda kucheza, ajiulize yeye kwanini kaachwa/kabaki

Isitoshe kuna watoto akina Teden Mengi, Di Shon wanaweza kucheza mpira mkubwa leo jamaa akasahaulika

Hapo bado sijawataja majeruhi Bailly na Rojo (wanaokaribia kupona) na kaka yao Smalling yupo kwa mkopo huko na anakichafua, sioni future ya Jones na inawezekana mechi ya juzi ikawa ya mwisho kwake
kwahiyo Jones anajiandaa na Aston villa
 
Hana ndoto za mafanikio binafsi pengine kufundisha Man united ndiyo ndoto pekee aliyokuwa amebakiza sasa kaitimiza.

Huwezi kutaka kupigania top four halafu ukawa na squad legelege namna hiyo.

Nadhani huyu jamaa amekuwa guaranteed na bodi ya kutofukuzwa

Ukiangalia maamuzi yake kwenye usajili, utagundua kuwa hana haraka ya kufanya vizuri, he is so reluxed
 
Mkuu naona comments zako nyingi sana unamtetea Pogba

Ukweli ni kwamba Pogba anacheza pale kwa kuwa hatuna creative midfielder mwingine, lakini uwezo wa Pogba ni wa kawaida sana (siongelei kupiga visigino na madoido mengine)

Huyu Pogba hamfikii hata Ericksen wa sasa aliyejikatia tamaa
Ndio maana kuna viungo walinzi na viungo washambuliaji/wachezeshaji. Sasa wewe unataka Pogba acheze namba sita? na kwanini akiwa mzima pamoja na unamuita mlingoti lakini hakai benchi?
 
Japo matokeo ya mechi za mwishoni yalipaswa kumfanya Ed ajiulize mara mbili mbili, alipaswa kupewa mkataba baada ya msimu kuisha

Kwa Ed/Glazers it was the cheapest option
ole alipoteza mechi yake ya kwanza ya ligi kuu dhidi ya arsenal mnamo tarehe 10/ 03.
ole alipewa mkataba mpya tarehe 28 /03.

ole alifanya vibaya kuanzia mwezi april tulipofungwa kwa mara nyengine tena na wolves then wakafuata barcelona.
kwa ufupi miezi miwili ya mwisho OGS alishinda mechi moja tu dhidi ya west ham.

mkuu jaalia upo nafasi ya ed woodward,
je ni kweli ungelisubiria hadi mwisho wa msimu kwa kuangazia yale matokeo tulioyapata mwanzoni?
je kama angelifanya vizuri hadi mwisho wa msimu ungelimpa kandarasi mpya?
 
Suala na majeruhi inabidi pia tuilaumu na department ya recruitment

Kuna wachezaji wana historia ya majeruhi toka walipotoka lakini tukawasajili, Bailly, Dalot
 
Uamuzi sahihi ilikuwa ni kumpa/kutompa mkataba baada ya msimu kuisha

Angemaliza msimu na matokeo mazuri ningeunga mkono 100% (japo sijakata tamaa naye maana ninaamini ana kitu, kutokana na zile mechi za awali)

Kiujumla naamini Ole sio kocha mbovu kiivyo, tatizo ni Mr. Yes Man na ni kocha anayejali kuwafurahisha akina Ed zaidi kuliko mashabiki. Pia ninaamini kuna makocha wazuri zaidi yake, wanaoweza kutufikisha mbali zaidi
 
Lvg alikuwa na majeruhi Wengi kuliko hata Ole msimu wa kwanza tulipata majeruhi hadi 39, Even carrick mchezaji ambae alikuwa kila msimu anamaliza mechi zote akawa ni pancha.

Same kwa mourinho kina Baily, Herrera, martial na wengine wengi mechi 1 uwanjani nyengine majeruhi, japo kipindi chake kulikuwa na ka uafadhali fulani ila still ilikuwa ni majanga kwa majeruhi, same kwa ole history inaendelea, hili ni tatizo la muda mrefu lililojichimbia mizizi.

Kuhusu mfumo mimi naamini ole si mjinga kuacha mfumo wake uliompa ushindi mfululizo issue ni kwamba hana wachezaji tena wa kucheza huo mfumo tangu Herrera aondoke. Mfumo wetu wa sasa 4-2-3-1 pia tunaonekana tuna mapengo hasa no 10 na wing ya kulia na striker incase katika wachezaji wetu tunaowategemea mmoja anaumia.

Na philosophy yake mbona inajionyesha mkuu na tactic wise amethibitisha ubora wake against top teams zote msimu huu, chelsea mara 2, Liverpool, Arsenal wote tuliwazidi maarifa kimchezo tatizo letu tunakosa tu uzoefu wa kumaliza mechi tunapoongoza.

Philisophy ya ku press, counter, kupromote academy, kuhakikisha opponents hawatukimbizi zaidi yetu, attitude na discipline kwa wachezaji etc

Na kama unakumbuka mwanzo wa msimu tulikuwa hatufungi magoli mengi ila mechi nyingi kama Norwich, brighton, Europa, sheffield etc tunafunga Goli 3

Tumpe ole muda hata kama hatachukua hayo makombe angalau atajenga timu na Kumtengenezea njia kocha anayekuja.
 
Mkuu issue hapo sio kumchagua Right back, issue ni kwamba alipofika spurs alipokelewa na poch then poch akaanza kumueleza malengo yao kifupi wameongea maneno ya kimpira zaidi.

Ila kuja man U hakuna aliemtambua yeye ni nani (japo ana appointment) na maswali aliyoulizwa ni ya kiofisi zaidi kama vile anaajiriwa mhasibu, mfano hapo anamuuliza jina lako nani, timu unayotoka, umecheza mechi ngapi etc ndio maana agent akakasirika na kuondoka.

Na ndio tatizo la kuajiri watu wa bank wahandle mambo ya mpira.
 
Na huu ni uzembe wa Ole
Kuondoka kwa Herrera sio uzembe wa Ole,

kabla ya Ole kupewa kandarasi, kulikuwa hakuna mawasiliano (ya kuongeza mkataba) kati ya Herrera camp na Man u.
Na hili Herrera mwenyewe amelisema .

Ole kaja ,tayari ishakuwa complicated, PSG washaweka donge nono, mazungumzo yakawa magumu.

Hadi hapo utaelewa uzembe ni wa nani.
 
Suala la majeruh ni kawaida kabisa , hlo hata hatakiwi kulaumu, makocha wengi wanajua kuelekea katikat ya msimu timu lazima isumbuliwe na majeruh tuu, hvyo replacement hufanyika mapema kwenye usajili, Guardiola ana timu mbili kias kwamba anayeondoka na anayeingia tofaut yake ni ndog Sana, Kwa kocha mzoefu hili linajulikana Sana...Ole sio mzoefu na hajui rafu zilizopo kwenye tasnia ya management....!!! Timu inakabiliwa na tournament karbia nne , utaweza kurun zote ukiwa na mchezaji tegemeo mmoja mmoja kila namba.....???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…