Johnny Sins
JF-Expert Member
- Nov 4, 2019
- 2,538
- 3,828
Wanabishanaswadakta
kwa mwendo huu tunaoendelea kutembea nao kwenye hii safari yetu ya kurudisha ubora wetu huenda ikatuchukua mpaka world cup ya qatar ndipo kidogo tutakuwa na uwezo wa kugombania ubingwa
Chief-Mkwawa wewe ni miongoni mwa wadau wanaofuatilia mambo kiundani sana humu ndani pengine kuliko mchangiaji yeyote ndani ya thread hii hususani linapokuja suala la takwimu , ishu za ndani zinazohusu masuala ya kifedha na repoti za usajili na kwa hilo nakupa hongera sana kaka yangu , labda mkuu unaweza kutupa uthibisho wowote juu ya hayo madai yako nilioyanukuu hapo juu ya kwamba OGS mwenyewe alihitaji wachezaji hao wanne waungane na wale watatu kwenye dirisha hili la usajili na si maneno ya watu (uvumi)Hebu Tu assume ole amepewa target zake zote
1. Hio namba 10 badala ya kucheza lingard ama perreira angekuwa dybala
2. Striker angekuja kama alivyotaka
3. Midfield angekuja pia mechi kama ya Shefield tusimchezeshe perreira midfield.
4. Winga wa kulia.
Je timu yetu ingekuwa wapi sasa hivi.
yes ole anasuka timu na kila mtu anaona jitihada zake kuanzia kuwapa nafasi graduates kutoka academies bila ya kujali kukosa kwao uzoefu kwenye mashindano makubwa, maisha yote uzoefu kwa mchezaji husika unapatikana akiwa ndani ya uwanja na si kwenye benchi la wachezaji wa hakiba (kwa hili namsifu sana)Hivyo ole anaisuka timu mimi bado nina imani nae na naamini ni mtu sahihi kuwa pale, sababu pekee ambayo nitakubaliana nayo kwamba ole aondoke ni kama Ed ataachia ngazi aje DOF wa michezo na Alete kocha wake atakaefanya kazi, bila Hivyo akiondoka Ole hata aje nani tunarudia tu cycle ya Moyes, LVG, Mou.
Mkuu issue ya Dybala ilikuwa ni deal done imekwamishwa na Imaging right, Dybala ameuza haki zake za matangazo na akiondoka juve inabidi awalipe hao jamaa na Ed amekataa kutoa hicho kiasi (kiliwekwa kama Agent fee).Chief-Mkwawa wewe ni miongoni mwa wadau wanaofuatilia mambo kiundani sana humu ndani pengine kuliko mchangiaji yeyote ndani ya thread hii hususani linapokuja suala la takwimu , ishu za ndani zinazohusu masuala ya kifedha na repoti za na kwa hilo nakupa hongera sana kaka yangu , labda mkuu unaweza kutupa uthibisho wowote juu ya hayo madai yako nilioyanukuu hapo juu ya kwamba OGS mwenyewe alihitaji wachezaji hao wanne waungane na wale watatu kwenye dirisha hili la usajili na si maneno ya watu (uvumi)
ed woodward anasema ya kwamba ishu zote za usajili msimu huu zimeongozwa na crew husika yenye kujielewa ndani ya klabu, swali langu inawezekana vipi tushindwe kusajili angalau target mbili kati ya nne hizo?
- namba 10 mfano dyabala au maddison
- striker baada ya kumuondoa lukaku mfano dembele
- midfield mfano wa bruno fernandez, longstaff, declan rice
- winga wa kulia mfano sancho
There is a myth that we have non-football people making football decisions," he said. "I think that is insulting to the brilliant people who work on the football side in this club."
mwezi uliopita ed woodward kupitia interview ya jarida la United We Stand alizungumza hivi
We want players to come in who respect their teammates, the club, the history,”
“They must understand that they are creating a legacy by coming to Manchester United. Nobody is bigger than the club.
“There should be both a humbleness and an arrogance. Humble when you are on the team coach and you wear the club suit, you do up your top button and wear your tie, you represent the club in the right way. Then you sign autographs for the people who pay your wages.
Whatever manager we have has to buy into that philosophy and Ole is a walking, talking version of that. Let’s let this play out with Ole in terms of the culture reboot.”
nikisema ogs mwenyewe ndiye aliyefelisha baadhi ya target hizo ambazo sisi mashabiki tungelipenda kuzishuhudia zikivaa uzi mwekundu nitakuwa nakosea?
nafahamu ya kwamba ole aliongea maneno hayo kwa nyakati tofauti lakini sidhani kama ndicho alichokuwa akimaanisha kwenye ubongo wake hususani anapokuwa mbali na waandishi wa habari.Hivyo ole anamhusudu huyu jamaa ama False 9 yoyote ndio maana unaona Hata martial sasa hivi anapewa hii role.
Na kuhusu usajili ole mwenyewe akiongea na waandishi wa habari amekiri anataka striker, tena mara nyingi ameongea maneno haya.
hio kauli ya kutaka striker aliitoa dirisha lilivyofungwa tu hata kabla hatujaanza kupoteza hivyo hilo suala la ole kuataka striker sababu timu inafanya vibaya si kweli. kifupi ole hataki mtu wa kusimama pale mbele, anataka mtu mwenye movement na kulink na wenzake. na greenwood hata hio premier league hachezi sana. akipatikana mtu hata hii January anaweza kuja, ngoja tuone huyu mtoto wa Salzburg itakuwaje.nafahamu ya kwamba ole aliongea maneno hayo kwa nyakati tofauti lakini sidhani kama ndicho alichokuwa akimaanisha kwenye ubongo wake hususani anapokuwa mbali na waandishi wa habari.
kwa mtazamo wangu
ole alikuwa na uwezo wa kutafuta kwanza mshambuliaji mpya kabla ya kumuuza romelu lukaku ambaye hakuwa tena kwenye mipango yake ya kuwa mshambuliaji namba moja tokea msimu uliopita.
hiki kinachotokezea nyakati hizi ndicho kilichokuwepo kwenye ubongo wa OGS, bwana ole alihitaji kuona antony martial, rashford na greenwood ndio wanakuwa waendashaji jahazi la safu ya ushambuliaji na si ujio wa mshambuliaji mpya.
kufeli kwa wanadamu hao watatu kwa sasa (kushindwa kufunga magoli mengi kwa pamoja) ndio kumeibua tena hoja ya kutafuta mshambuliaji mwengine japo kwa njia ya mkopo, ujio wa mshambuliaji kwa mfano mandzukic hakutawawazibia riziki hawa ndugu watatu hususani greenwood.
kinyume chake kufanya vizuri kwa rashford, greenwood na anthony martial ndiyo kuzikwa kwa hoja ya kutafuta mshambuliaji mwengine atakayeziba pengo la lukaku, ikitokezea utatu wetu ukawa unafunga magoli mengi hutozisikia tetesi za kutafutwa mshambuliaji mpya
kiupande wangu naamini OGS hakuwa na dhamira ya kutafuta mshambuliaji mpya nyakati za usajili kwa sababu tayari alishafanya maamuzi ya kuwakabidhi majukumu ndugu watatu tokea mechi za kirafiki.
huo ndio mtazamo wangu
Hebu Tu assume ole amepewa target zake zote
1. Hio namba 10 badala ya kucheza lingard ama perreira angekuwa dybala
2. Striker angekuja kama alivyotaka
3. Midfield angekuja pia mechi kama ya Shefield tusimchezeshe perreira midfield.
4. Winga wa kulia.
Je timu yetu ingekuwa wapi sasa hivi.
Niwakumbushe tu mashabiki wenzangu wa Man U matatizo ya msimu uliopita.
1. Timu zilikuwa zinatukimbiza tulikuwa tunashika nafasi ya 18 linapokuja suala la kukimbia uwanjani ila sasa hivi tunakubaliana hili tatizo limetatulika mechi nyingi tunawazidi wapinzani.
2. Tulikuwa na tatizo la beki, sasa hivi hali ime improve zaidi japo bado tatizo lipo hasa upande wa kushoto ila kulia na kati tupo njema.
3. Mishahara mikubwa,
4.umoja wa kitimu, ni nadra sasa hivi kukuta kuna tatizo dressing room, wachezaji wote ni kitu kimoja na unawaona wanakuwa kitimu zaidi.
Hivyo ole anaisuka timu mimi bado nina imani nae na naamini ni mtu sahihi kuwa pale, sababu pekee ambayo nitakubaliana nayo kwamba ole aondoke ni kama Ed ataachia ngazi aje DOF wa michezo na Alete kocha wake atakaefanya kazi, bila Hivyo akiondoka Ole hata aje nani tunarudia tu cycle ya Moyes, LVG, Mou.
Tatizo pekee ambalo naona Ole nae linamshinda ni majeruhi, Toka Moyes atutimulie Jopo letu la wataalamu majeruhi man U ni wengi sana, tumekuwa kama Arsenal.
nadhani tatizo kuu linaanzia hapa na hata mimi nakubaliana na wewe kwamba jamaa hakufanya upembuzi yakinifu, inawezekana aliamini kwa kikosi alicho kirithi ukiongezea na maingizo mapya na wahitimu wa academies basi ana uwezo wa kuleta ushindani mkubwa sana kwenye top 4.
kuna sehemu nimesoma nimeona gary neville anasema klabu inapaswa iongeze wachezaji watano wapya nikabaki kucheka, nikikumbuka kejeli na dharau zao walizozionyesha kwa walimu waliopita pindi walipojaribu kuzungumzia udhaifu wa timu yetu eti leo hii kwa kuwa rafiki yao ndio bosi mkuu wa timu wanamtetea kwa hoja zile zile walizozipinga mwanzoni.
They need another centre back, they need a left-back and a couple of central midfielders and a striker or a forward. ‘That’s not going to change and won’t change entirely even after January. But there’s something there.’
mshambuliaji(lukaku) ameuzwa na OGS.
midfield wawili (fellaini na herrera) wameondolewa na OGS bila ya kutafuta wengine
swadakta
kwa mwendo huu tunaoendelea kutembea nao kwenye hii safari yetu ya kurudisha ubora wetu huenda ikatuchukua mpaka world cup ya qatar ndipo kidogo tutakuwa na uwezo wa kugombania ubingwa
upo sahihi
tuna kundi kubwa sana la wachezaji wenye viwango duni, no skills, no football brain jambo linalopelekea timu inapoingia uwanjani inakosa mipango madhubuti ya kumuathiri adui haijalishi tulipokuwa vyumba vya kubadilishia nguo wachezaji wamejifunza mbinu zote za kumuathiri adui husika.
sidhani kama atapewa nafasi ya kucheza jumapili hii.
kuna uwezekano wa kurudishwa kwa mfumo wa 4 - 3 - 3
kumradhi nimekusudia ule mfumo wa kila siku wa kutumia viungo wawili.Tukicheza 4 3 3 nadhani tutateswa sana hatuna wachezaji sahihi wa kucheza huu mfumo kwa sasa.
https://twitter.com/NBCSportsSoccer/status/1198662700320149510https://twitter.com/NBCSportsSoccer/status/1198662700320149510
19 year old Brandon Williams pulls one back for Manchester United
https://twitter.com/intent/like?tweet_id=1198662700320149510
https://twitter.com/NBCSportsSoccer/status/1198663777107005440
laiti kama angelibakishwa Ander Herrera na baadae akaongezwa play maker mfano wa Bruno Fernandez nina uhakika hili tatizo la midfield tusingelikuwa na muda wa kulizungumzia.Andreas Pereira had never looked so counterproductive on the pitch, making constant disappointment Fred look like a world-class midfielder. Rashford and Anthony Martial entered the match at full fitness, but weren’t able to capitalize on exhausting Sheffield’s defense early on because there was such an absence of skill from the aforementioned players. The first half at Bramall Lane was arguably one of United’s worst this campaign, with the squad only registering one shot on goal in 45 minutes.
laiti kama angelibakishwa Ander Herrera na baadae akaongezwa play maker mfano wa Bruno Fernandez nina uhakika hili tatizo la midfield tusingelikuwa na muda wa kulizungumzia.
scott + bruno + herrera
herrera + pogba + bruno
tumezipoteza lulu kwa makusudi
kwa hili anapaswa kuwajibika, sporting wameshamuongezea mkataba mpya bruno fernandez.Na huu ni uzembe wa Ole
katika ubora wako brother,kwenye usajili mkuu tutalaumu sana makocha ila mwisho wa siku mwenye maamuzi ya mwisho ni huyo jamaa unakumbuka tetesi za Bruno na pass accuracy asilimia 75? unafikiri nani ameamua hivyo? jopo letu la usajili lipo hovyo sana, kuna nyepesi nyepesi jamaa mmoja insider anaclaim msimu huu kuna mchezaji right back top player kutoka top club (probably Munier wa psg) alikuja Man utd akakutana na Matt judge, jamaa ni clue less kabisa kaanza kumuuliza unaitwa nani, umecheza timu gani na appearence ngapi? agent wake akakasirika na kumuambia mapokezi waliyopata spurs. source ya video hii hapa dakika 5 za mwanzo video ni ndefu sana
katika ubora wako brother,
hiyo video nitaiangalia japo baadae ili nipate kujifunza zaidi yalio nyuma ya pazia.
acha nijaribu kuchangia hiyo ishu ya right back top player ambaye inasadikika ni thomas mounier na kama itakuwa sipo sahihi naomba unirekebishe kwa mara nyengine tena.
thamani ya wan bissaka ni paundi millioni 50
thamani ya tripper ni paundi millioni 20 kuelekea atletico.
thamani ya thomas mounier inakadiriwa ilikuwa ni 15-30 millioni pound.
kwa fikra zangu mimi zilizojaa udhaifu kwenye dili hili ningeliangalia mambo makuu matatu ambayo ni umri wa mchezaji husika, kiwango chake na thamani yake ya kumnunua.
kwa kuziangalia factors hizo basi thomas mouneir angelifaa zaidi kusajiliwa kuliko trippier au wan bissaka kwa sababu umri wake ni 27, kiwango chake ni bora ukilinganisha na hao wengine na pia thamani yake ni ndogo.
kama matt judge alipuuzia dili la thomas mounier basi kuna uwezekano mkubwa tayari bwana matt alishapelekewa jina rasmi la mchezaji anayehitajika na benchi la ufundi likiongozwa na OGS na si mwengine ni wan bissaka.
kwa dili hili la right back sidhani kama ni sahihi kumuangushia mzigo wa lawama bwana matt judge,
ed na matt wanaifahamu vizuri sana fedha na sidhani kama wangelifanya maamuzi haya ya kulipa 50 millioni badala ya 25 million kwa huduma hiyo hiyo.