Sheffield VS Man Utd
Sheffield atakuwa nyumbani dhidi ya United wa Manchester
Katika mechi 5 za mwisho Sheffield hajapoteza game hata 1, game 3 ame draw na 2 kashinda zote akiwa nyumbani
Tangu SAF astaafu, katika mechi 19 ugenini dhidi ya timu za wapanda daraja, United ameshinda mechi 11, ame draw mechi 2 na kufungwa mechi 6
Katika mechi 7 za mwisho, the Blades (Sheffield) dhidi ya United, the Blades amepigwa mechi zote kwa jumla ya magoli 14 kwa 1.
Wachezaji muhimu ambao hawatakuwepo. United watamkosa Tominay, Pogba, pengine na Matic, Tuanzebe na Shaw kwa kukosa match fitness
Wakati huo huo the Blades watawakosa wachezaji 2 mmoja amepata majeraha kwenye National Team na namba 1 wao Dean Henderson ambaye ni golikipa wa United anayekipiga pale Bramal Lane kwa mkopo
Wachezaji chipukizi wanaoweza kupata nafasi kwa United kutokana na majeraha ya first teamers ni James Garner na Dylan Levit (midfielders) na Brandon Williams (left back)
Mechi itapigwa saa 1:30 usiku pale Bramal Lane