kuhusu mlinzi wa kati anaweza kumtumia hata eric dier kama timu itakumbana na tatizo la majeruhi kwa wachezaji wa kikosi cha kwanza. Nyakati zile alipokuwa real madrid au chelsea mara nyingi aliweza kucheza msimu mzima huku akitegemea walinzi watatu tu wa kati wenye uzoefu (ramos, pepe, carvalho, terry, del horno, varane akiwa bado kinda). Uzuri zaidi walinzi wote hao uliowataja hawana takwimu mbovu za kiafya kama ilivyo kwetu (marcos rojo, phil jones, eric bailly)
Ishu muhimu zaidi inayomsubiri mourinho kuitekeleza ni kupigania mikataba ya wachezaji wake muhimu kama nilivyoeleza comment iliopita kwa sababu jan vertoghen, toby arderweireld eriksen,na rose mikataba yao huenda inamalizika msimu huu (sina uhakika).
kwa bajeti ya usajili tulioizoea pale tottenham hotspurs halitokuwa jambo jepesi kiupande wake kupewa paundi millioni 100 au zaidi kwa lengo la kuziba mapengo ya wachezaji hao kama wataondoka wakiwa huru, kibaya zaidi jose mourinho si muumini mkubwa sana wa kupandisha young players kutoka academy na kuwapa nafasi ya kucheza kama alivyokuwa akifanya mauricio pochettino.