Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Hawa Man si wakamchukue Samatta Genk?Hakuna wafungaji pale,hakuna viungo wabunifu.Timu hii ni ya kushika nafasi za kati kwenye msimamo wa ligi
 
Belo, wanavyosema wenye timu yao humu ndani ni kwamba huu mfumo wa 4-2-3-1 ndio uliokuwa unatupa mafanikio kwenye mechi zetu za kujipima nguvu ikiwemo dhidi ya milan brothers, spurs na wengineo hivyo basi kuna uwezekano mkubwa wa kuendelea kutumika kwa mfumo huu. badala ya ule tuliouzoea wa 4-3-3 kwa takribani misimu mitatu iliopita.

unajua kwa kiasi kikubwa sana wengi wetu hatufahamu lolote linalotendeka ndani ya klabu kwa sababu hatuna uwezo wa kuaccess taarifa nyeti zinazoihusu klabu matokeo tumeishia kuwa watabiri kwa yale yanayo na yatakayotendeka mbeleni kwa kufuata zaidi mdundo wa vyombo vya habari.
  • kwa kutumia huu utabiri acha niamini ya kwamba bwana OGS alitegemea ingizo la kiungo mwengine mshambualiaji mfano wa eriksen, bruno fernandez au maddison atakayekuja kucheza namba 10 eneo ambalo tunamtumia jesse lingard kwa msimu huu baada ya kuswitch mfumo wa 4-2-3-1 tokea preseason, lakini ndio hivyo kama kawaida kwa mara nyengine tena ed woodward na rafiki yake matt judge walishindwa kufanikisha usajili wowote wa kiungo huku wakifahamu fika tumempoteza ander herrera na marouanne fellaini.
  • kwa kutumia utabiri huo huo acha pia niamini ya kwamba OGS huenda ndiye aliyefelisha baadhi ya sajili za wachezaji mfano wa bruno fernandez kwa hoja ya kukosa DNA zitakazomwezesha kuipigania klabu kwa jasho lake haijalishi kama atalipwa hela ndogo na kumuona jesse lingard ndiye kiungo sahihi zaidi kucheza namba 10 huku paul na scott wakicheza deep midfields eneo ambalo tumekwishazoea tukiwatumia herrera na nemanja matic.
kuna mwanadamu mmoja tu ambaye huenda akambadilisha fikra bwana ole ili arudishe tena mfumo wa 4-3-3 ambao unamwezesha paul pogba kucheza juu zaidi akitokea upande wa kushoto ambao ndio upande tunaoutegemea zaidi kupika mashambulizi na si mwengine isipokuwa ni fred the red.
kama fred atacheza vizuri pindi atakapopewa nafasi basi tutaswitch mfumo wa 4-3-3 kwa sababu OGS hana uwezo wa kumweka nje paul pogba ili apate kuendeleza mfumo wake wa 4-2-3-1.

pia tufahamu si nemanja matic, perreira wala fred atakeyekuwa na uthubutu wa kumfanya OGS abadilishe msimamo wa kifikra kwa kumweka nje scott mctominay kwenye eneo la kiungo mkabaji kwa sababu hao wote hawana DNA za kimanchester ukilingansha na scott hivyo basi wapenzi wa nemanja matic kwa msimu huu mujiandae kisaikolojia.
OGS na benchi lake wanamuona scott mctominay kama ndiye roy keane wetu mpya.​

  • fred ndiye aliyeshikilia ufunguo utakaomwezesha OGS abadili style ya kiuchezaji mara kwa mara msimu huu.
  • fred ndiye aliyeshikilia ufunguo wake mwenyewe utakaomwezesha kufungua au kufunga chumba chake cha kuhifadhia vifaa pale AON complex a.k.a carrington, kama atacheza vizuri basi msimu ujao ataendelea kuwepo klabuni ila kama ataendelea kucheza ovyo kwa ninavyomtazama solskajer na hii recruitment yake ya karne ya 20 aliyokuja nayo huenda nafasi yake rasmi akapewa gardner au yule mjinga anayetokea newcastle united anayeitwa sean longstaff
 
Dah na mimi ninechoka Mkuu, yaani boko ametoa Pogba lawama wanapewa wenzake eti sio world class players. Na Pogba sio mara ya kwanza kupoteza mpira either ukai cost timu au ukakaribia kui cost timu.

Na kutokana na hilo mimi naona it's not a good idea kumchezesha Pogba nyuma yeye na Scot, achezeshwe kule mbele kama ilivyokuwa msimu uliopita OGS alipopewa timu. Kuchezeshwa nyuma, inasababisha anapopoteza mpira kuwa na risk zaidi ya kufungwa goli kuliko akichezeshwa mbele

Lingard pia anapaswa kubadilika especially kwenye kuimprove his attacking ability (creating chances and scoring goals). Kutokana na uwezo wa Gomes au Mata katika kutengeneza nafasi kuliko Lingard, na kutokana na Cristal Palace kutokuwa timu kubwa yenye kuleta hatari sana, sikuona sababu ya kumuanzisha Lingard na ukawaacha wachezaji creative zaidi yake.

Lukaku was still clinical compared to Tony na Rashy. Ninakubali huko duniani wapo kweli wachezaji clinical kuliko Rom lakini si wengi kama watu wanavyosema. Hata yule Inaki wa Bilbao sio clinical kiivyo, na asingeweza kufanya jambo tofauti sana na akina Tony. Kwa sasa duniani sidhani kama kuna ma strikers zaidi ya 15 wanaomzidi Lukaku uwezo wa ku score.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…