Mkuu naona upo upande wa MSIMAMO, jaribu kuwa flexible kwa kuangalia uhalisia
Sijui kwanini leo ghafla Chelsea imeonekana ni kipimo kinachotudanganya
Hivi ni kweli Chelsea ni wabovu kiasi hicho
Tulishinda mechi zote za Australia, watu wa kasema is just preseason, tukashinda dhidi ya Inter kisha Spurs ikaonekana is just pre season. Jana tumempiga Chelsea inaonekana ni timu dhaifu
kama nitakua sahihi mara ya mwisho kwa timu yetu kucheza dakika 90 bila ya kuruhusu goli ilikuwa ni mwezi februari hivyo basi kitendo cha kumaliza dakika 90 bila ya kufungwa goli haijalishi tunacheza na mbeya city kiupande wangu pia ni matokeo yalionifurahisha sana.
kivyovyote matokeo yale pia yamechangiwa kiupande fulani na mabadiliko tulioyafanya kwenye safu yetu ya ulinzi (ujio wa maguire na bissaka) kwa asilimia 50 bila ya kusahau ubora ule tuliouzoea kuushuhudia machoni mwetu mara kwa mara kutoka kwa
david degea ambao msimu uliopita hatukuweza kuushuhudia
daniel james pia anaonekana yupo vizuri kiupande fulani na pengine inatokanwa zaidi na zawadi aliyopewa na muumba ya kujaaliwa speed and acceleration anapokuwa na mpira na hata asipokuwa na mpira, pace yake iliwapa tabu sana japo kwa muda mfupi mabeki wa chelsea jambo lililopelekea mlinzi mmoja apewe kadi ya njano, kikubwa anachopaswa kukifanyia kazi ni utulivu ili afikie level za
gareth bale, kama ataendelea kukosa utulivu mwisho wa siku atajikuta anafuata nyayo za
aron lennon, wright phillips au
theo walcott.
jambo kubwa linalonifanya nisifurahishwe sana na hali iliopo sasa (kuendelea kuwa na msimamo) kwenye klabu yetu ni ikitendo cha klabu kuipoteza nafasi adhimu ya kujenga timu imara kwa kutumia dirisha moja tu la usajili kama wanavyofanya au walivyowahi kufanya baadhi ya wapinzani wetu (rejea usajili wa man city miaka miwili iliopita, liverpool mwaka uliopita, usajili wa spurs na real madrid msimu huu)
hata ukizisoma comment za wadau wengi humu ndani hata wale wanaosifia kiwango hicho kizuri tulichokionyesha kama inavyosemwa kwenye mechi ya chelsea pia utagundua ya kwamba wengi wao baadae wanarudi tena maeneo yale yale tunayoyalalamikia tokea msimu uliopita si ajabu utakuta mchangiaji ana andika:
midfield bado ipo ovyo inahitaji mabadiliko
bado hatupo vizuri kwenye eneo la umaliziaji kwani tunakosa utulivu tukifika mbele (clinicalness)
tunakosa kiungo wa kuongeza wigo wa ubunifu kama alionao pogba
bado hatupo vizuri eneo la kiungo ukabaji tunaruhusu ovyo
luke shaw anampa kazi kubwa sana maguire ya kumlinda n.k
ukiangalia kwa umakini matatizo mengi yanayoelezwa unajifunza ya kwamba kumbe kunahitajika jitihada kubwa sana kupitia benchi la ufundi pamoja na wachezaji wenyewe kuyatatua jambo ambalo si rahisi kuyatatua na kama ingelikuwa ni rahisi basi yangelikwisha tatuliwa tokea msimu uliopita alioanza kazi OGS au tokea mwezi uliopita (yalipoanza mazoezi na preseason) ndio maana naendelea kuwa na msimamo wa kuamini ya kwamba njia pekee ya kutatua baadhi ya matatizo hayo ni kufanya usajili ambao kwa makusudi tumeupotezea.
ninavyoamini mimi ni rahisi kumsajili bruno fernandez kwa dau kubwa baadae ukamsubiri ayazoee mazingira ya uingereza kuliko kuendelea kumsubiri andreas perreira abadilishe kiwango chake cha uchezaji mpaka kuwa na kiwango kinachokaribiana na bruno fernandez
ninavyoamini mimi ni rahisi kumsajili kiungo mfano wa james madison kwa dau kubwa baadae ukamsubiri aizoee style ya uchezaji ya klabu yetu kuliko kuendelea kumsubiri jesse lingard abadilishe style yake ya uchezaji ya kutoka kiungo asiyetengeneza nafasi ya goli mpaka kuwa kiungo anayetengeneza angalau nafasi 50 za magoli kwa msimu ukilinganisha na nafasi 100 alizotengeneza james maddison msimu uliopita akiwa na leicester city. Kama tungelifanikisha mfano wa target mbili hizi basi tungelikuwa na jeuri ya kucheza na timu kubwa yeyote duniani.
halafu mkuu situations iliopo chelsea msimu huu ndio inayopelekea baadhi yetu tuamini ya kwamba chelsea si kipimo tosha cha kuifanyia tathimini klabu yetu kiubora. Naamini laiti kama chelsea wangelipata nafasi hii adhimu ya kusajili wachezaji kwenye dirisha lililoisha basi wangelifanya mabadiliko makubwa sana ya wachezaji kuliko tulivyofanya sisi kufuatia kuondoka kwa wachezaji wao muhimu mfano hazard, morata, david luiz, majeruhi ya wachezaji, bila ya kusahau kuondoka kwa gary cahill aliyemaliza mkataba wake.
nimeanza kuwa na majonzi kwa yale ninayoyashuhudia kwenye hii thread kuanzia siku chache zilizopita, nimeanza kunusa harufu ya kulazimisha uwepo wa mijadala inayofanana na ndege aina ya kasuku, ndege huyu inasemekana amejaaliwa uwezo wa kuweza kunukuu yale yanayozungumzwa na wengineo bila ya kuyafanyia tafakari ya kina, kwa sisi binadamu kuiga tabia hiyo tutakuwa tunabomoa na si kujenga endapo tutalazimisha sote tuwe na mawazo sawa humu ndani.
Naomba hii tabia ya ukasuku ibaki kule kwenye jukwaa la siasa na si humu ndani, jukwaa la siasa ndio utakutana na mpenzi wa chadema kwa zuri na baya vile vile utakutana na mshabiki wa ccm kwa zuri na baya lenye athari kwa wenzake.
GGMU